Posts

Showing posts from February, 2024

DUA YA UPEPO MKALI

DUA YA UPEPO MKALI [ اللهم إني أسألك خيرها ، وأعوذ بك من شرها ] أخرجه أبو داود 4/326وابن ماجه 2/1228 [Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi nakuomba kheri ya upepo huu, na najikinga kwako na shari yake.]    [Imepokewa na Abuu Daud na Ibnu Maajah.] [ اللهم إني أسألك خيرها ، وخير ما فيها ، وخير ما أُرسلت به ، وأعوذ بك من شرها وشر ما فيها وشر ما أرسلت به ] مسلم 2/616 والبخاري 4/76 [Ewe Mwenyezi Mungu nakuomba kheri yake na kheri  ya kilicho ndani yake, na kheri ya uliyoituma ndani yake, na najikinga kwako kutokana na shari yake na shari iliyoko ndani yake na shari iliyotumwa nao.]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

DUA BAADA YA KUMZIKA MAITI

DUA BAADA YA KUMZIKA MAITI  [اللهم اغفر له اللهم ثبته] [Ewe Mwenyezi Mungu  msamehe, Ewe Mwenyezi Mungu  mfanye awe thabiti] Mtume ﷺ alikuwa akimaliza kuzika anasimama mbele ya kaburi na kisha anasema “Muombeeni msamaha kwa Mwenyezi Mungu  ndugu yenu na muombeeni kuthibitishwa kwani hivi sasa anaulizwa.      [Imepokewa na Abuu Daud na Al-Haakim]

DUA YA KUMUINGIZA MAITI NDANI YA KABURI

DUA YA KUMUINGIZA MAITI NDANI YA KABURI  [ بسم الله وعلى سُنة رسول الله ]  أبو داود 3/314بسند صحيح وأحمد [Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na kwa mwenendo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu.]   [Imepokewa na Abuu Daud na Ahmad.]

DUA YA KUMTAAZI ALIYEFILIWA

DUA YA KUMTAAZI ALIYEFILIWA  إن لله ما أخذ وله ما أعطى . وكل شيء عنده بأجل مُسمى …فلتصبر ولتحتسب :  البخاري 2/80 ومسلم 2/63 [Kwa hakika ni Chake Mwenyezi Mungu Alichokichukua, na ni chake Alichokitoa, na kila kitu Kwake kina muda maalum] (…….kisha Mtume ﷺ akimwambia:)  “basi vumilia na taka malipo kwa Allaah” ]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim.] na akisema:  [ أعظم الله أجرك ، وأحسن عزاءك وغفر لميتك ] [Ayafanye mengi Allaah malipo yako, na Akufanye kuzuri kutaaziwa (kuhaniwa) kwako na Amsamehe maiti wako.] …basi ni bora         [Tazama Al-Adhkaar ya Imam Al-Nnawawiy]

DUA YA MAITI YA MTOTO MCHANGA WAKATI WA KUMSWALIA

DUA YA MAITI YA MTOTO MCHANGA WAKATI WA KUMSWALIA  [اللهم أعذه من عذاب القبر] أخرجه مالك في الموطأ 1/288 وابن أبي شيبه في المصنف 3/ 217 والبيهقي 4/9 [Ewe Mwenyezi Mungu  mlinde na adhabu ya kaburi]        [Imepokewa na Imam Maalik na Ibnu Abiy Shayba na Al-Bayhaqiy.] اللهم اجعله فرطاً وذخراً لوالديه ،وشفيعاً مجاباً .اللهم ثقل به موازينها وأعظم به أجورهما ، وألحقهُ بصالح المؤمنين ، واجعلهُ في كفالة إبراهيم ، وقه برحمتك عذاب الجحيم ، وأبدله داراً خيراً من داره ، وأهلاً خيراً من أهله ، اللهم اغفر لاسلافنا ، وأفراطنا ، ومن سبقنا بالإيمان [Ewe Mwenyezi Mungu mjaaliye kuwa nikitangulizi na akiba kwa wazazi wake na nikiombezi chenye  kukubaliwa dua yake.  Ewe Mwenyezi Mungu kwa ajili yake zifanye nzito mizani za wazazi wake na yafanye mengi malipo yao, na mkutanishe na wema wa waumini na mjaaliye awekatika dhamana ya Ibrahim na umuepushe kwa rehema yako na adhabu ya moto, na mbadlishie nyumba bora kuliko nyumba yake, na jamaa bora kulko jamaa zake. ...

DUA YA KUMUOMBEA MAITI WAKATI ANAPOSWALIWA

DUA YA KUMUOMBEA MAITI WAKATI ANAPOSWALIWA  اللهم اغفر له وارحمه، وعافه ،واعف عنه ،وأكرم نُزُله ، ووسع مُدخلهُ ، واغسله بالماء والثلج والبرد ، ونقه من الخطايا كما ينقى الثوب الأبيض من الدنس ، وأبدله داراً خيراً من داره ، وأهلاً خيراً من أهله وزوجاً خيراً من زوجه، وأدخله الجنة ،وأعذه من عذاب القبر ( ومن عذاب النار مسلم 2/663 [Ewe Mwenyezi Mungu msamehe na umrehemu na umuafu na msamehe na mtukuze kushuka kwake (kaburini) na upanue kuingia kwake, na muoshe na maji na kwa theluji na barafu na mtakase na makosa kama unavyoitakasa  nguo nyeupe kutokana na uchafu, na mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba  yake na jamaa bora kuliko jamaa zake, na mke bora kuliko mke wake, na muingize peponi na mkinge na adhabu ya kaburi (na adhabu ya moto).]        [Imepokewa na Muslim.] اللهم اغفر لحينا وميتنا ، وشاهدنا وغائبنا ، وصغيرنا وكبيرنا ، وذكرنا وأُنثانا ، اللهم من أحييته منا فأحيه على الإسلام ، ومن توفيته منا فتوفه على الإيمان اللهم لا تحرمنا أجره ولا تضلنا بعده ابن...

DUA YA ALIYEPATWA NA MSIBA

DUA YA ALIYEPATWA NA MSIBA   [ إنا لله وإنا إليه راجعون اللهم أجرني في مصيبتي وأخلف لي خيراً منها ] مسلم2/632 [Sisi ni wa Allaah nasi Kwake tutarejea, Ee Allaah  nilipe kwa msiba wangu na unipe badili yake bora kuliko huo.]       [Imepokewa na Muslim.]

DUA YA KUMFUNGA MACHO MAITI

DUA YA KUMFUNGA MACHO MAITI  اللهم اغفر  لفلان ( باسمه) ورفع درجته في المهديين، واخلفه في عقبه في الغابرين، واغفر لنا وله يا رب العالمين ، وافسح له في قبره ونور له فيه        مسلم 2/634 [Ewe Mwenyezi Mungu msamehe (jina la maiti) na ipandishe daraja yake katika wailoongoka, na weka badili yake kwa aliyowacha nyuma na utusamehe sisi na yeye ewe Mola wa viumbe vyote na umkunjulie yeye katika kaburi lake na umtilie mwangaza ndani yake.]       [Imeokewa na Muslim.]

KUMLAKINIA ANAETOKWA NA ROHO

KUMLAKINIA ANAETOKWA NA ROHO  Amesema Mtume ﷺ Mwenye kuwa neno lake la mwisho [لا إلهَ إلاّ اللّه] [Hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki ila ni Mwenyezi Mungu]………. Ataingia peponi         [Imepokewa na Abuu Daud.]

DUA ANAYOOMBA MGONJWA ALIYEKATA TAMAA YA KUPONA

DUA ANAYOOMBA MGONJWA ALIYEKATA TAMAA YA KUPONA  [ اللهم اغفر لي وارحمني والحقني بالرفيق الأعلى ] البخاري 7/10 ومسلم 4/1893 [Ewe Mwenyezi Mungu, nisamehe mimi na unirehemu na unikutanishe na waja walio katika daraja za juu.]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim.] Imepokelewa kutoka kwa Bibi Aisha Radhi za Allah zawe juu yake  amesema: [Mtume ﷺ wakati anakufa alikuwa akiingiza mikono yake ndani ya maji kisha akipangusa kwayo uso wake na akisema: [ لا إله إلا الله إن للموت لسكرات ] [Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu, hakika kifo kina uchungu]    [Imepokewa na Bukhari.] لا إله إلا الله والله أكبر ، لا إله إلا الله وحده ، لا إله إلا الله وحده لا شريك لهُ ، لا إله إلا الله لهُ الملك ولهُ الحمد ، لا إله إلا الله ولا حول ولا قوة إلا بالله أخرجه الترمذي وابن ماجه وصححه الألباني [Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu  ni Mkubwa, Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu...

FADHILA ZA KUMTEMBELEA MGONJWA

 FADHILA ZA KUMTEMBELEA MGONJWA Imepokelewa na Ali Bin Abi Twalib amesema: nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ  akisema : [ Mtu anapomtembelea ndugu yake Muislamu mgonjwa basi hutembelea katika bustani ya peponi mpaka atakapoketi, naanapoketi hufunikwa na rehma ikiwa ni asubuhi wanamtakia rehma malaika sabini elfu mpaka jioni na ikiwa ni jioni wanamtakia rehma malaika sabini elfu mpaka asubuhi. ]   [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy na Ibnu Maajah na Ahmad.]

DUA YA KUMTEMBELEA MGONJWA

DUA YA KUMTEMBELEA MGONJWA  Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ anapoingia kumzuru mgonjwa  akimwambia [ لا بأس طهور إن شاء الله ] [Hakuna neno, (ugonjwa) ni kusafishwa (na madhambi) anapopenda Mwenyezi Mungu. ]    [Imepokewa na Bukhari.]   Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ: Hapana mja yeyote muislamu anaemtembelea mjongwa ambae wakati wake wa kufa bado haujafika na akamuombea mara saba [ أسأل الله العظيم رب العرش العظيم أن يشفيك ] [Namuomba Mwenyezi Mungu  Mtukufu Mola wa Arshi tukufu (akuponyeshe)] Isipokuwa Mwenyezi Mungu  humponyesha mgonjwa huyo.   [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy na Abuu Daud.]

DUA INAYO KINGWA NAYO WATOTO.

DUA INAYO KINGWA NAYO WATOTO.  Imepokelewa  na Ibn Abbas amesema  alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  akiwakinga wajukuu wake (Hassan na Hussein) akisema : [ أعيذكما بكلمات الله التامة ، من كل شيطان وهامة ، ومن كل عينِ لامة ] [Nawakinga kwa maneno ya Mwenyezi Mungu  yaliyotimia awakinge kutokana na kila shetani na uvamizi na kila jicho lenye kudhuru.]      [Imepokewa na Bukhari.]

PONGEZI YA KUPATA MTOTO NA JAWABU YAKE

PONGEZI YA KUPATA MTOTO NA JAWABU YAKE  [ بارك الله لك في الموهوب لك ،وشكرت الواهب، وبلغ أشدهُ، ورزقت برهُ ] [Mwenyezi Mungu  akubariki katika ulichopewa na umshukuru  aliyekupa, na afike kuwa mkubwa na uruzukiwe wema wake] Na aliyepongzwa  atamuombea aliyempongeza kwa kumwambia: [ بارك الله لك وبارك عليك ، وجزاك الله خيراً ، ورزقك الله مثله، وأجزل ثوابك] [Mwenyezi Mungu akubariki na ateremshe baraka juu yako, na Mwenyezi Mungu  akujaze kheri, na Mwenyezi Mungu  akuruzuku mfano wake na afanye nyingi thawabu zako] [Tazama Al-Adhkaar ya Imamu Al-Nnawawiy uk 349]

DUA ANAYOISOMA MTU AKITOKEWA NA JAMBO ASILORIDHIA AU AKISHINDWA KUFANYA JAMBO

DUA ANAYOISOMA MTU AKITOKEWA NA JAMBO ASILORIDHIA AU AKISHINDWA KUFANYA JAMBO Amesema Mtume ﷺ [muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu  kuliko mumini dhaifu, na wote wana kheri.  Fanya pupa kwa kile kitakacho kunufaisha na taka msaada kwa Mwenyezi Mungu   wala usichoke na kikikupata kitu chochote kibaya basi usiseme “lau”  kama ningefanya kadha na kadha  yasingenitokea haya, lakini sema: [ قدر الله وما شاء فعل ] [Amepanga Mwenyezi Mungu  na analolitaka anafanya] …… hakika neno la “lau”  linafungua matendo ya shetani’         [Imepokewa na Muslim.] Hakika Mwenyezi Mungu  analaumu mwenye kukata tamaa, lakini usivunjike moyo na ukishindwa na jambo kabisa sema: [ حسبي الله ونعم الوكيل ] [Mwenyezi Mungu  ananitosheleza, naye ni Mbora wa kutegemewa.]

DUA YA KUMFUKUZA SHETANI NA WASIWASI WAKE

 DUA YA KUMFUKUZA SHETANI NA WASIWASI WAKE Mambo yafuatayo yanatakiwa kufuatwa pindi anapotolewa  shetani: [الاستعاذة بالله منه]   أبو داود 1/206 والترمذي [Kumuomba Mwenyezi Mungu  akuhifadhi nae]         [Imepokewa na Abuu Daud.] [ الأذان ]  مسلم 1/ 291 والبخاري 1/151 Kumuadhinia.       [Imepokewa na Bukhari na Muslim] [ الأذكار وقراءة القرآن ] [Kusoma nyiradi zilizopokewa kutoka kwa Mtume ﷺ nakusoma Qur’ani.

ANALOSEMA ALIYEFANYA DHAMBI

ANALOSEMA ALIYEFANYA DHAMBI   [ ما من عبدٍ يذنب ذنباً فيحسن الطهور ، ثم يقوم فيصلي ركعتين ، ثم يستغفر الله إلا غفر الله لهُ ] أبو داود 2/86 والترمذي 2/257 وصححه الألباني [Hakuna mja yeyote yule anaefanya dhambi kisha akatawadha vizuri na akaswali rakaa mbili, kisha akamtaka Mwenyezi Mungu  msamaha ila atasamehewa]       [Imepokewa na Abuu Daud na Al-Ttirmidhiy na kusahihishwa na Al-Baaniy]

DUA YA AMBAE LIMEKUWA GUMU KWAKE JAMBO

DUA YA AMBAE LIMEKUWA GUMU KWAKE JAMBO   [ اللهم لا سهل إلا ما جعلته سهلاً وأنت تجعل الحزن إذا شئت سهلاً ] رواة ابن حبان في صحيحه برقم 2427 (موارد) وابن السني برقم 351 [Ewe Mwenyezi Mungu hakuna jepesi ila ulilolifanya jepesi, nawe unalifanya gumu jepesi ukitaka.]     [Imepokewa na Ibnu Hibban na Ibnu Sunniy.]

DUA YA ALIYEINGIWA NA WASIWASI KATIKA SWALA YAKE AU KISOMO CHAKE

DUA YA ALIYEINGIWA NA WASIWASI KATIKA SWALA YAKE AU KISOMO CHAKE   أعوذ بالله من الشيطان الرجيم واتفل على يسارك ]   ثلاثاً]  مسلم 4/1729 [Najilinda na Mwenyezi Mungu   kutokana na shetani aliyelaaniwa] Kisha utatema vijimate vichache upande wa kushoto mara tatu. Imepokelewa kutoka kwa Uthman Ibn Al-Ass Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: [Nilimwambia Mtume ﷺ Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika shetani amenikalia kati yangu na kati ya swala yangu na kisomo changu, ananitatiza.  Akasema Mtume ﷺ [Huyo ni shetani aitwae “Khanzab” ukimuhisi amekujia basi muombe hifadhi Mwenyezi Mungu nae, na tema vijimate vichache kushotoni kwako mara tatu] ……nikafanya hivyo Mwenyezi Mungu  akaniondoshea.    [Imepokewa na Muslim.]

DUA YA KULIPA DENI

DUA YA KULIPA DENI  [ اللهم اكفني بحلالك عن حرامك ، وأغنني بفضلك عمن سواك ] الترمذي 5/560 [Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze mimi na halali yako kutokana na haramu, na unitosheleze kwa fadhila zako nisiwahitaji wengine usio Wewe.]        [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy.] [ اللهم إني أعوذ بك من الهم والحزن ، والعجز والكسل ،والبخل والجبن وضلع الدين وغلبة الرجال ] البخاري7/ 158 [Ewe Mwenyezi Mungu  hakika mimi najilinda kwako kutokana na hamu na huzuni na kutoweza na uvivu na ubakhili na uoga na uzito wa deni na kushindwa na watu.]       [Imepokewa na Bukhari.]

DUA ALIYEPATWA NA SHAKA KATIKA IMANI YAKE

DUA ALIYEPATWA NA SHAKA KATIKA IMANI YAKE  [ يستعيذ بالله ] البخاري مع الفتح 6/336 ومسلم 1/120 [Atataka (aombe) hifadhi ya Mwenyezi Mungu]       [Imepokewa na Bukhari na Muslim.] [ ينتهي عما شك فيه ]  البخاري مع الفتح 6/336 ومسلم 1/120 [Aondowe kile kitu alichokifanyia shaka]        [Imepokewa na Bukhari na Muslim] “يقول” آمنت بالله ورسله  مسلم 1/  119 Kisha aseme [Nimemuamini Mwenyezi Mungu  na mitume yake.]       [Imepokewa na Muslim.]   {يقرأ قوله تعالى { هُوَ الْأَوَّلُ وَالْآخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ Kisha asome aya hii katika Qur’ani [Yeye ndiye wa Mwanzo na wa Mwisho, na aliye Wazi, na aliyejificha, naye ni mjuzi wa kila kitu.] [Imepokewa na Abuu Daud.]

DUA YA ANAEWAOGOPA WATU

  DUA YA ANAEWAOGOPA WATU [ اللهم اكفنيهم بما شئت ] مسلم 4/2300 [Ewe Mwenyezi Mungu , nitosheleze kutokana na wao kwa unachotaka.]       [Imepokewa na Muslim.]

KUOMBA DUA DHIDI YA ADUI

KUOMBA DUA DHIDI YA ADUI   [ اللهم منزل الكتاب ، سريع الحساب ، اهزم الأحزاب ، اللهم اهزمهم وزلزلهم ]  مسلم 3/1362 [Ewe Mwenyezi Mungu, Mteremsha wa kitabu, Mwepesi wa kuwahisabu (waja wako) Vishinde vikosi.  Ewe Mwenyezi Mungu, washinde na watetemeshe.]      [Imepokewa na Muslim.]

DUA YA MWENYE KUOGOPA DHULMA YA MWENYE KUTAWALA

DUA YA MWENYE KUOGOPA DHULMA YA MWENYE KUTAWALA  اللهم رب السموات السبع ، ورب العرش العظيم ،كن لي جاراً من فلان بن فلان ، وأحزابه من خلائقك ؛ أن يفرط على أحد منهم أو يطغى ، عز جارك ،وجل ثناؤك ، ولا إله إلا أنت  البخاري في الأدب المفرد برقم 707 وصححه الألباني [Ewe Mwenyezi Mungu  Mola wa mbingu saba, na Mola wa arshi tukufu, kuwa mlinzi wangu kutokana na (fulani bin fulani ) na vikosi vyake miongoni mwa viumbe vyako, kwa kunisaliti mmoja miongoni  mwao, au kunifanyia uadui, amehishimiwa  mwenye kulinda, na zimetukuka sifa zako na hapana mola apasae kuabudiwa kwa uhaki ila Wewe.]        [Imepokewa na Bukhari katika kitabu cha Adabul-Mufrid na Kusahihishwa na Al-Baaniy.] الله أكبر، الله أعز من خلقه جميعاً ، الله أعز مما أخاف وأحذر ،أعوذ بالله الذي لا إله إلا هو ، الممسك السموات السبع أن يقعن على الأرض إلا بإذنه ،من شر عبدك فلان ،وجنوده وأتباعه وأشياعه ، من الجن والأنس ، اللهم كن لي جاراً من شرهم ، جل ثناؤك وعز جارك ، وتبارك اسمك ، ولا إله غيرك...

DUA YA KUPATWA NA JANGA AU BALAA

DUA YA KUPATWA NA JANGA AU BALAA   [لا إلَهَ إلاَّ اللَّهُ الْعَظـيمُ الْحَلِـيمْ، لا إلَهَ إلاَّ اللَّهُ   رَبُّ العَـرْشِ العَظِيـمِ، لا إلَهَ إلاَّ اللَّهُ  رَبُّ السَّمَـوّاتِ ورّبُّ الأَرْضِ ورَبُّ العَرْشِ الكَـريم] البخاري 7/154ومسلم 4/ 2092 [Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu  aliye Mtukufu Mpole, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu  Mola wa Arshi  tukufu, hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki ila ni  Mwenyezi Mungu  Mola wa mbingu na Mola wa ardhi na Mola wa arshi tukufu.]          [Imepokewa na Bukhari na Muslim] [.اللّهُـمَّ رَحْمَتَـكَ أَرْجـوفَلا تَكِلـني إِلى نَفْـسي طَـرْفَةَ عَـيْن، وَأَصْلِـحْ لي شَأْنـي كُلَّـه لَا إِلَهَ إِلَّا أنْـت ] أبو داود 4/324 وأحمد 5/42 وحسنه الألباني في صحيح أبو داود 3/ 959 [Ewe Mwenyezi Mungu  rehema zako nataraji, usinitegemeze  kwenye nafsi yangu japo kwa muda wa upepesa jicho, naunitengenezee mambo yangu yote, ha...

DUA YA ANAEKUTANA NA ADUI AU MWENYE KUTAWALA

 DUA YA ANAEKUTANA NA ADUI AU MWENYE KUTAWALA [ اللهم إنا نجعلك في نحورهم ونعوذ بك من شرورهم ] أبو داود 2/89 وصححه الحاكم ووافقه الذهبي 2/142 [Ewe Mwenyezi Mungu  hakika sisi tunakufanya Wewe uwe katika vifua  vyao na tunajikinga kwako na shari zao.]     [Imepokewa na Abuu Daud na Kusahihishwa na Al-Haakim] [ اللهم أنت عضدي وأنت نصيري ،بك أجول ،وبك أصول ، وبك أُقاتل ]  أبو داود 3/42 والترمذي 5/572 [Ewe Mwenyezi Mungu  Wewe ndie msaidizi wangu nawe ndie mnusura wangu, kwako ninazunguka na kwako ninavamia na kwako ninapigana.]       [Imepokewa na Abuu Daud na Al-Ttirmidhiy.] [ حسبنا الله ونعم الوكيل ]  البخاري 5/172 [Mwenyezi Mungu anatutosheleza, naye ni mbora wa kutegemewa.]        [Imepokewa na Bukhari.]

DUA UKIWA NA HAMU NA HUZUNI

DUA UKIWA NA HAMU NA HUZUNI  اللّهُـمَّ إِنِّي عَبْـدُكَ ابْنُ عَبْـدِكَ ابْنُ أَمَتِـكَ نَاصِيَتِي بِيَـدِكَ، مَاضٍ فِيَّ حُكْمُكَ، عَدْلٌ فِيَّ قَضَاؤكَ أَسْأَلُـكَ بِكُلِّ اسْمٍ هُوَ لَكَ سَمَّـيْتَ بِهِ نَفْسَكَ أِوْ أَنْزَلْتَـهُ فِي كِتَابِكَ، أَوْ عَلَّمْـتَهُ أَحَداً مِنْ خَلْقِـكَ أَوِ اسْتَـأْثَرْتَ بِهِ فِي عِلْمِ الغَيْـبِ عِنْـدَكَ أَنْ تَجْـعَلَ القُرْآنَ رَبِيـعَ قَلْبِـي، وَنورَ صَـدْرِي وجَلَاءَ حُـزْنِي وذَهَابَ هَمِّـي  أحمد 1/391وصححه الألباني [Ewe Mwenyezi Mungu  hakika mimi ni mtumwa wako, mtoto wa mtumwa wako, mtoto wa kijakazi chako, utosi wangu uko mikononi mwako, yaliyopita kwangu yako katika hukumu yako, ni usawa kwangu kunihukumu kwako, nakuomba kwa kila jina ambalo ni Lako ulilojiita kwako mwenyewe au uliloliteremsha katika kitabu chako, au ulilomfundisha yoyote yule kati ya viumbe vyako, au ulilolihifadhi Wewe mwenyewe (na kujihusisha kulijuwa) katika ilimu iliofichika kwako, nakuomba ujaaliye  (uifanye) Qur’ani kuwa ni raha na uchanuzi ...

DUA BAADA YA SALAMU KATIKA SWALA YA WITRI

DUA BAADA YA SALAMU KATIKA SWALA YA WITRI  سُـبْحانَ المَلِكِ القُدّوس]   ثلاث مرات] [Ametakasika Mwenyezi Mungu  Mfalme, Mtakatifu.]   mara tatu. Na mara ya tatu anaisoma kwa sauti kubwa na kwa kuivuta. [ ربِّ الملائكةِ والرّوح رواه النسائي 3/244 والدار قطني وغيرهما [Ewe Mola wa malaika na wa Jibriil.]       [Imepokewa na Al-Nnasaai na Al-Ddarqutnyi]

ANAYOYAFANYA MWENYE KUOTA NDOTO MBAYA

ANAYOYAFANYA MWENYE KUOTA NDOTO MBAYA  ينفث عن يساره]  ثلاثاً] [apulize kushotoni kwake mara tatu.]    يستعيذ بالله من الشيطان ومن شر ما رأى ]     ثلاث مرات] [Kisha atake (aombe) hifadhi kwa Mwenyezi Mungu  na alichokiota na kwa shetani mara tatu.] [لا يحدث بها أحدا] [Kisha hatakiwi kumzungumzia mtu] [ يتحول عن جنبه الذي كان عليه ] [Kisha asilalie ule upande au ubau aliyeootea, bali ageuke ubavu mwingine.] [ يقوم يصلي إن أراد ذلك ] [Atasimama kusali akitaka.] [Imepokewa na Muslim.]

DUA YA QUNUT YA WITR

DUA YA QUNUT YA WITR  اللّهُـمَّ اهْـدِنـي فـيمَنْ هَـدَيْـت، وَعـافِنـي فـيمَنْ عافَـيْت، وَتَوَلَّـني فـيمَنْ تَوَلَّـيْت ، وَبارِكْ لـي فـيما أَعْطَـيْت، وَقِـني شَرَّ ما قَضَـيْت، فَإِنَّـكَ تَقْـضي وَلا يُقْـضى عَلَـيْك إِنَّـهُ لا يَـذِلُّ مَنْ والَـيْت، [ وَلا يَعِـزُّ مَن عـادَيْت ]، تَبـارَكْـتَ رَبَّـنا وَتَعـالَـيْت أخرجه أصحاب السنن الأربعة وأحمد والدرامي والحاكم والبيهقي [Ewe Mwenyezi Mungu  niongoze pamoja na uliowaongoza, na unipe afya njema pamoja na uliowapa afaya njema, na nifanye kuwa ni mpenzi wako pamoja na uliowafanya  wapenzi na nibariki katika ulichonipa na nikinge na shari ya ulilolihukumu kwani Wewe unahukumu wala huhukumiwi.  Hakika hadhaliliki uliemfanya mpenzi (wala hatukuki uliemfanya adui ) Umetakasika Ewe Mola wetu na Umetukuka.]       [Imepokewa Kwenye vitabu vya Hadithi vinne na Ahmad na Al-Ddaarimiy na Hakim na Al-Bayhaqiy] [ اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِرِضـاكَ مِنْ  سَخَطِـك، وَبِمُعـافاتِـكَ مِنْ عُقوبَـت...

DUA YA WASIWASI USINGIZINI AU KUSIKIA UOGA NA MFADHAIKO

 DUA YA WASIWASI USINGIZINI AU KUSIKIA UOGA NA MFADHAIKO [ أعوذ بكلمات الله التَّامَّة من غضبه وعقابه، وشر عباده، ومن همزات الشياطين وأنْ يحضرون ]  أبو داود 4/12 نظر صحيح الترمذي3/ 171 [Najilinda na maneno ya Mwenyezi Mungu  yaliotimia kutokana na hasira zake na adhabu yake na shari ya waja wake na vioja vya mashetani na kunijia kwao.]         [Imepokewa na Abuu Daud na Al-Ttirmidhiy.]

DUA UNAPOJIGEUZA USINGIZINI USIKU

DUA UNAPOJIGEUZA USINGIZINI USIKU [ لا إله إلا الله الواحد القهار، ربُّ السموات والأرض وما بينهما العزيز الغفار ] [Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu  Mmoja  Alieshinda, Mola wa mbingu na ardhi na vilivyo kati yake, Aliyetukuka Mwingi wa Msamaha]        [Imepokewa na Haakim na Al-Nnasaai]

NYIRADI ZA KULALA

NYIRADI ZA KULALA Alikuwa Mtume ﷺ akienda kulala usiku anakusanya viganja vyake kisha akivipuliza na akivisomea Suratul-Ikhlaasw, na Suratul-Falaq, na Suratun-Naas, kisha akipangusa kwa hivyo viganja vyake kiasi anachoweza katika mwili wake, akianza kichwani na usoni na mbele. akifanya hivyo mara tatu.     [Imepokewa na Bukhari na Muslim.] Mtume ﷺ amesema : [Ukienda kulala soma Ayatul-Kursiy mpaka uimalize kwani Allaah ataendelea kukuhifadhi wala hakukaribii Shaytwaan mpaka asubuhi] […..اللّهُ لا إلهَ إلاّ هُـوَ الـحَيُّ القَيّـومُ لا تَأْخُـذُهُ سِنَـةٌ وَلا نَـوْمٌ ] [Imepokewa na Bukhari.] Amesema Mtume ﷺ [Anayesoma aya mbili za mwisho wa Suratul-Baqarah usiku zinamtosheleza] آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ كُلٌّ آمَنَ بِاللّهِ وَمَلآئِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لاَ نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ وَقَالُواْ سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ) ( لاَ يُكَلِّفُ اللّهُ نَفْسًا إِلاَّ وُسْعَهَا ...

NYIRADI ZA ASUBUHI NA JIONI

NYIRADI ZA ASUBUHI NA JIONI Imepokelewa kutoka kwa  Anas  Radhi za Allah ziwe juu yake amesema:  Amesema Mtume ﷺ [Kukaa pamoja na watu wanaomtaja Mwenyezi Mungu  Aliyetukuka  kuanzia Swalah ya Al-Fajiri  mpaka kuchomoza jua kunapendeza zaidi kwangu mimi kuliko kuacha huru watu wanne miongoni mwa wana wa Ismail na kukaa na watu wanaomtaja  Mwenyezi Mungu  Aliyetukuka  kuanzia baada ya Swalah ya Al-Asiri mpaka kuchwa jua kunapendeza zaidi kwangu mimi kuliko kuwaacha huru watu wanne.]      [Imepokewa na Abuu Daud]. اللّهُ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ لاَ تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلاَ نَوْمٌ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الأَرْضِ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِنْدَهُ إِلاَّ بِإِذْنِهِ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلاَ يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلاَّ بِمَا شَاء وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ وَلاَ يَؤُودُهُ حِفْظُهُمَا وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ Mwenye kusoma (Ayatul-Kursiy...

DUA YA SWALATUL-ISTIKHARA (SWALA YA KUTAKA USHAURI)

DUA YA SWALATUL-ISTIKHARA (SWALA YA KUTAKA USHAURI) Amesema Jaabir Bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akitufundisha Swala ya Istikhara kama vile anavyotufunza sura ya Qur’an. Anasema ﷺ  ‘Akikusudia mmoja wenu kufanya jambo, aswali rakaa mbili zisizo za faradhi, kisha aseme:  اللهم إني أستخيرك بعلمك ، وأستقدرك بقدرتك ، وأسألك من فضلك العظيم فإنك تقدِرُ ولا أقدِرُ ، وتعلم ولا أعلم ، وأنت علام الغيوب ، اللهم إن كنت تعلم أن هذا الأمر -يسمي حاجته – خير لي في ديني ومعاشي وعاقبة أمري – أو قال : عاجلة وآجله – فاقدره لي ويسره لي ، ثم بارك لي فيه ، وإن كنت تعلم أن هذا الأمر شر لي في ديني ومعاشي وعاقبة أمري – أو قال : عاجله وآجله – فاصرفه عني واصرفني عنه ، واقدر لي الخير حيث كان ، ثم ارضني به [Ewe Mwenyezi Mungu  hakika mimi nakutaka ushauri (muelekezo) kwa ujuzi Wako, na nakuomba uniwezeshe kwa uwezo Wako, na nakuomba fadhila Zako kubwa, hakika Wewe unaweza, nami siwezi, nawe unajua nami sijui, nawe nimjuzi wa yale yaliyofichikana.  ...

NYIRADI BAADA YA KUTOA SALAM

NYIRADI BAADA YA KUTOA SALAM  [ أستغفر الله ” ثلاثاً ..” اللهم أنت السلام ، ومنك السلام ، تباركت يا ذا الجلال والإكرام]  مسلم1/ 414 [Naomba msamaha Mwenyezi Mungu” (mara tatu)  Ewe Mwenyezi Mungu  Wewe ndie Amani, na Kwako ndiko kutokako amani, Umetukuka Ewe Mwenye Utukufu na Ukarimu]   [Imepokewa na Muslim]   لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ اللَّهُمَّ لَا مَانِعَ لِمَا أَعْطَيْتَ وَلَا مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ وَلَا يَنْفَعُ ذَا الْجَدِّ مِنْكَ الْجَدُّ    البخاري 1 /255 ومسلم 1 / 414 [Hapana apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu  hali ya kuwa peke yake hana mshirika, niwake Ufalme, na ni Zake sifa njema, na Yeye ni muweza wa kila kitu.  Ewe Mwenyezi Mungu  hapana anaeweza kukizuia ulichokitoa, na wala kutoa ulichokizuia, na wala haumnufaishi mwenye utajiri kwani kwako wewe ndio utajiri.]       [Imepokewa na Bukhar...

DUA BAADA YA TASHAHHUD (ATTAHIYATU)

DUA BAADA YA TASHAHHUD (ATTAHIYATU)  اللهم إني أعوذ بك من عذاب القبر،ومن عذاب جهنم،ومن فتنة المحيا والممات ،ومن شر فتنة المسيح الدجال البخاري 2/ 102 ومسلم 1/ 412 واللفظ لمسلم [Ewe Mwenyezi Mungu mimi nakutaka unihifadhi na adhabu za kaburi, na adhabu ya (moto wa) jahannam, na fitna ya uhai, na ya kufa, na shari ya fitna ya Masihi-dajjaal.]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim] اللهم إني أعوذ بك من عذاب القبر،وأعوذ بك من فتنة المسيح الدجال،وأعوذ بك من فتنة المحيا والممات، اللهم إني أعوذ بك من المأثم والمغرم البخاري 1/ 202 ومسلم 1/ 412 [Ewe Mwenyezi Mungu  hakika mimi najilinda Kwako kutokana na adhabu ya kaburi, na najilinda Kwako kutokana  na fitna ya Masihi-dajjaal, na najilinda Kwako kutokana na fitna ya uhai na ya mauti, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda Kwako kutokana na dhambi na deni.]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim]  اللهم إني ظلمت نفسي ظلماً كثيراً ، ولا يغفر الذنوب إلا أنت ، فاغفر لي مغفرة من عندك وارحمني إنك أنت الغف...

KUMSWALIA MTUME ﷺ BAADA YA TASHAHHUD

KUMSWALIA MTUME ﷺ BAADA YA TASHAHHUD  اللهم صل على محمد وعلى آل محمد ، كما صليت على  إبراهيم ، وعلى آل إبراهيم ، إنك حميد مجيد ، اللهم بارك على محمد وعلى آل محمد كما باركت على إبراهيم ، وعلى آل إبراهيم إنك حميد مجيد       البخاري مع الفتح 6/ 408 [Ewe Mwenyezi Mungu mrehemu Muhammad na jamaa zake Muhammad kama uliyomrehemu Ibrahim, na jamaa zake Ibrahim, hakika Wewe ni Mwenye kusifika Mtukufu. Ewe Mwenyezi Mungu mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammad, kama ulivyo mbariki Ibrahim na jamaa zake Ibrahim, hakika Wewe ni Mwenye kusifika Mtukufu.]        [Imepokewa na Bukhari.] اللهم صل على محمد وعلى أزواجه وذريته،كما صليت على آل إبراهيم، وبارك على محمد وعلى أزواجه وذريته كما باركت على آل إبراهيم إنك حميد مجيد   البخاري مع الفتح  6/ 407 ومسلم  1/ 306 واللفظ له [Ewe Mwenyezi Mungu mrehemu Muhammad, na wake zake, na kizazi chake, kama ulivyowarehemu jamaa wa Ibrahim.  Na mbariki Muhammad, na wake zake, na kizazi chake, kama u...

DUA BAADA YA TASHAHHUD (ATTAHIYATU)

DUA BAADA YA TASHAHHUD (ATTAHIYATU)  اللهم إني أعوذ بك من عذاب القبر،ومن عذاب جهنم،ومن فتنة المحيا والممات ،ومن شر فتنة المسيح الدجال البخاري 2/ 102 ومسلم 1/ 412 واللفظ لمسلم [Ewe Mwenyezi Mungu mimi nakutaka unihifadhi na adhabu za kaburi, na adhabu ya (moto wa) jahannam, na fitna ya uhai, na ya kufa, na shari ya fitna ya Masihi-dajjaal.]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim] اللهم إني أعوذ بك من عذاب القبر،وأعوذ بك من فتنة المسيح الدجال،وأعوذ بك من فتنة المحيا والممات، اللهم إني أعوذ بك من المأثم والمغرم البخاري 1/ 202 ومسلم 1/ 412 [Ewe Mwenyezi Mungu  hakika mimi najilinda Kwako kutokana na adhabu ya kaburi, na najilinda Kwako kutokana  na fitna ya Masihi-dajjaal, na najilinda Kwako kutokana na fitna ya uhai na ya mauti, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda Kwako kutokana na dhambi na deni.]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim]  اللهم إني ظلمت نفسي ظلماً كثيراً ، ولا يغفر الذنوب إلا أنت ، فاغفر لي مغفرة من عندك وارحمني إنك أنت الغف...

KUMSWALIA MTUME ﷺ BAADA YA TASHAHHUD

KUMSWALIA MTUME ﷺ BAADA YA TASHAHHUD  اللهم صل على محمد وعلى آل محمد ، كما صليت على  إبراهيم ، وعلى آل إبراهيم ، إنك حميد مجيد ، اللهم بارك على محمد وعلى آل محمد كما باركت على إبراهيم ، وعلى آل إبراهيم إنك حميد مجيد   -    البخاري مع الفتح 6/ 408 [Ewe Mwenyezi Mungu mrehemu Muhammad na jamaa zake Muhammad kama uliyomrehemu Ibrahim, na jamaa zake Ibrahim, hakika Wewe ni Mwenye kusifika Mtukufu. Ewe Mwenyezi Mungu mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammad, kama ulivyo mbariki Ibrahim na jamaa zake Ibrahim, hakika Wewe ni Mwenye kusifika Mtukufu.]        [Imepokewa na Bukhari.] اللهم صل على محمد وعلى أزواجه وذريته،كما صليت على آل إبراهيم، وبارك عل ى م حمد وعلى أزواجه وذريته كما باركت على آل إبراهيم إنك حميد مجيد   البخاري مع الفتح  6/ 407 ومسلم  1/ 306 واللفظ له [Ewe Mwenyezi Mungu mrehemu Muhammad, na wake zake, na kizazi chake, kama ulivyowarehemu jamaa wa Ibrahim.  Na mbariki Muhammad, na wake zake, na kizazi chake, kam...

DUA YA TASHAHHUD (ATTAHIYATU)

DUA YA TASHAHHUD (ATTAHIYATU)  التحيات لله ، والصلوات ، والطيبات ، السلام عليك أيها النبي ورحمة الله وبركاته ، السلام علينا وعلى عباد الله الصالحين ،أشهد أن لا إله إلا الله ، وأشهد أن محمداً عبده ورسوله        البخاري مع الفتح 1/13 ومسلم 1/ 301 [Maamkuzi mema, na rehema na mazuri yote, ni kwa Mwenyezi Mungu, amani zishuke juu yako Ewe Mtume na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake, amani ishuke juu yetu, na juu ya waja wa Mwenyezi Mungu  walio wema, nakiri kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki ila ni Mwenyezi Mungu  na ninakiri kwamba Muhammad ni mja wake na ni Mtume wake.]    [Imepokewa na Bukhari.]

DUA ZA SIJDA YA KISOMO

DUA ZA SIJDA YA KISOMO  [سجد وجهي للذي خلقه ، وشق سمعه وبصره بحوله وقوته  {فتبارك الله أحسن الخالقين] الترمذي 2/474 وأحمد 6/30 والحاكم وصححه ووافقه الذهبي 1/ 220 والزيادة له [Umesujudu uso wangu kumsujudia  yule ambae ameuumba  na akapasuwa masikio yake, na macho yake, kwa uwezo wake na nguvu zake, (Ametukuka Mwenyezi Mungu  mbora wa waumbaji)]        [Imepokewa na Al-Tirmidhiy na Ahmad na Hakim na kuisahihisha] [اللهم أكتب لي بها عندك أجراً ، وضع عني بها وزراً ، واجعلها لي عندك ذخراً ، وتقبلها مني كما تقبلتها من عبدك داود] الترمذي 2/473 والحاكم وصححه ووافقه الذهبي 1/ 219 [Ewe Mwenyezi Mungu  niandikie kwako kwa sijda hii malipo, na nifutie kwayo madhambi, na ijaalie kwangu mbele yako ni akiba, na nikubalie kama ulivyomkubalia mja wako Dawud]       [Imepokewa na Al-Tirmidhi na Hakim na akasahihisha na kuafikiwa na Al-Dhahabiy]

DUA ZA KIKAO KATI YA SIJDA MBILI

DUA ZA KIKAO KATI YA SIJDA MBILI   [ رب اغفر لي ، رب اغفر لي ] أبو داود 1/ 231 وانظر  صحيح ابن ماجة 1/ 148 [Mola nisamehe, Mola nisamehe]       [Imepokewa na Abuu Daud] [ اللهم اغفر لي ، وارحمني ، واهدني ، واجبرني، وعافني، وارزقني ، وارفعني] أخرجه أصحاب السنن إلا النسائي وانظر صحيح الترمذي 1/90 وصحيح ابن ماجه 1/ 148 [Ewe Mwenyezi Mungu  nisamehe, na unirehemu, na uniongoze, na uniungie, na unipe afya, na uniruzuku na uniinue.]        [Imepoewa na Abuu Daud na Al-Tirmidhiy na Ibnu Maajah.]

DUA YA WAKATI WA KUSUJUDU

DUA YA WAKATI WA KUSUJUDU   [سبحان ربي الأعلى ] ، ثلاث مرات  أخرجه أهل السنن وأحمد وانظر صحيح الترمذي 1/83 [Ametakasika Mola wangu aliyejuu]   (Atasema hivi mara tatu)        [Imepokewa na Abuu Daud na Al-tirmidhiy na Al-Nasai na Ahmad.  [ سبحانك اللهم ربنا وبحمدك ، اللهم اغفر لي ] البخاري ومسلم [Kutakasika ni Kwako, Ewe Mwenyezi Mungu , Mola wetu, na sifa njema zote ni Zako, Ewe Mwenyezi Mungu  nisamehe.]       [Imepokewa na Bukhari na Muslim] [ سبوح قدوس رب الملائكة والروح ] مسلم 1/ 533 [Mwingi wa kutakaswa Mtakatifu, Mola wa malaika na Jibriil.]  [Imepokewa na Muslim] [ اللهم لك سجدت وبك آمنت ولك أسلمت،سجد وجهي للذي خلقه وصوره وشق سمعه وبصره تبارك الله أحسن الخالقين ]    مسلم 1/ 534 [Ewe Mwenyezi Mungu  Kwako nimesujudu, na Wewe nimekuamini, na Kwako nimesilimu, umesujudu uso wangu kumsujudia  aliyeuumba na akautia sura na akaupasua usikizi wake na uwoni wake, Ametukuka Mwenyezi Mungu ...

DUA YA KUINUKA KUTOKA KWENYE RUKUU

 DUA YA KUINUKA KUTOKA KWENYE RUKUU [ سمع الله لمن حمده] البخاري مع الفتح 2/ 282 [Mwenyezi Mungu Amemsikia mwenye kumsifu.]      [Imepokewa na Bukhari.] [ ربنا ولك الحمد ، حمداً كثيراً طيباً مباركاً فيه ] البخاري مع الفتح 2/ 282 [Ee Bwana wetu ni zako sifa njema sifa nyingi, nzuri, zenye baraka.]      [Imepokewa na Bukhari.] ملء السموات وملء الأرض وما بينهما ، وملء ما شئت من شئ بعد .أهل الثناء والمجد،أحق ما قال العبد، وكلنا لك عبد ، اللهم لا مانع لما أعطيت ولا معطي لما منعت ولا ينفع ذا الجد منك الجد         مسلم 1/ 346 [Zimejaa mbingu na zimejaa ardhi na vilivyomo ndani yake sifa Zako, na zimejaa (sifa Zako)  kwa ulichokitaka baada yake, Wewe ni mstahiki wa sifa na utukufu, ni kweli aliyoyasema mja Wako, na sote ni waja wako, Ee Allaah hapana  anaeweza kukizuia ulichokitoa, na wala kutoa ulichokizuia, na wala haumnufaishi mwenye utajiri, kwani kwao Wewe ndio utajiri.]        [Imepokewa na Muslim.]...

DUA ZA KUFUNGULIA SWALA

DUA ZA KUFUNGULIA SWALA  اللهم باعد بيني وبين خطاياي كما باعدت بين المشرق والمغرب ، اللهم نقني من خطاياي كما ينقى الثوب الأبيض من الدنس اللهم اغسلني من خطاياي بالماء والثلج والبرد.     البخاري 1/ 181 ومسلم 1/ 419 [Ewe Mwenyezi Mungu  niweke mbali na madhambi yangu kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi, Ewe Mwenyezi Mungu  nitakase na madhambi yangu kama vile inavyoitakaswa nguo nyeupe na uchafu, Ewe Mwenyezi Mungu  nisafishe na madhambi yangu kwa theluji na kwa maji na kwa barafu.]         [Imepokewa na Bukhari na Muslim.] [ سبحانك اللهم وبحمد ك وتبارك اسمك وتعالى جدك، ولا أ له غيرك]  أخرجه أصحاب السنن الأربعة وانظر صحيح الترمذي 1/77 وصحيح ابن ماجه 1135 [Kutakasika ni Kwako ewe Mwenyezi Mungu , na sifa njema zote ni zako, na limetukuka jina lako, na utukufu niwako, na hapana apasae kuabudiwa kwahaki, asie kuwa wewe.]     [Imepokewa na Abuu Daud na Al-Tirmidhiy na Al-Nasai na Ibnu Maajah.] وجه...

DUA ZA WAKATI WA KURUKUU

DUA ZA WAKATI WA KURUKUU سبحان ربي العظيم ] ثلاث مرات ] أخرجه أهل السنن وأحمد وانظر صحيح الترمذي   [Ametakasika Mola wangu aliye Mtukufu.] (Utasema mara tatu) [Imepokewa na Abuu Daud na al-Tirmdhi na Ibnu Maajah na Ahmad ]   [ سبحانك اللهم ربنا وبحمدك ، اللهم اغفر لي ] البخاري 1/199 ومسلم 1/ 350   [Kutakasika ni Kwako, Ewe Mwenyezi Mungu mola wetu na sifa njema zote ni Zako ewe Mwenyezi Mungu , nisamehe.] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]  [ سبوح قدوس رب الملائكة والروح ] مسلم 1/ 353 وأبو داود 1/230   [Mwingi wa kutakaswa, Mtakatifu, mola wa malaika na Jibiriil.]   [Imepokewa na Muslim na Ibnu Majah.]  [ اللهم لك ركعت وبك آمنت ،ولك أسلمت خشع لك سمعي وبصري ودمي ولحمي وعظمي وعصبي،وما استقل به قدمي] مسلم 1/534 والأربعة إلا ابن ماجه   [Ewe Mwenyezi Mungu Kwako nimerukuu, na Wewe nimekuamini, na Kwako nimejisalimisha, umenyenyekea Kwako usikizi wangu, na uwoni wangu, na ubongo wangu, na mfupa wangu, na hisi...