DUA YA KUPATWA NA JANGA AU BALAA

DUA YA KUPATWA NA JANGA AU BALAA 

[لا إلَهَ إلاَّ اللَّهُ الْعَظـيمُ الْحَلِـيمْ، لا إلَهَ إلاَّ اللَّهُ   رَبُّ العَـرْشِ العَظِيـمِ، لا إلَهَ إلاَّ اللَّهُ  رَبُّ السَّمَـوّاتِ ورّبُّ الأَرْضِ ورَبُّ العَرْشِ الكَـريم]

البخاري 7/154ومسلم 4/ 2092

[Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu  aliye Mtukufu Mpole, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu  Mola wa Arshi  tukufu, hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki ila ni  Mwenyezi Mungu  Mola wa mbingu na Mola wa ardhi na Mola wa arshi tukufu.]          [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

[.اللّهُـمَّ رَحْمَتَـكَ أَرْجـوفَلا تَكِلـني إِلى نَفْـسي طَـرْفَةَ عَـيْن، وَأَصْلِـحْ لي شَأْنـي كُلَّـه لَا إِلَهَ إِلَّا أنْـت ]

أبو داود 4/324 وأحمد 5/42 وحسنه الألباني في صحيح أبو داود 3/ 959

[Ewe Mwenyezi Mungu  rehema zako nataraji, usinitegemeze  kwenye nafsi yangu japo kwa muda wa upepesa jicho, naunitengenezee mambo yangu yote, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe]       [Imepokewa na Abuu Daud na Ahmad.]

[ لاَ إِلَهَ إِلَّا أنْـت سُـبْحانَكَ إِنِّي كُنْـتُ مِنَ الظّـالِميـن ]

الترمذي 5/529 والحاكم وصححه ووفقه الذهبي 1/505

[Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, kutakasika ni Kwako.  Hakika mimi ni miongoni mwa waliodhumu nafsi zao.]       [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy na Al-Haakim.]

[ الله الله ربي لا أشرك به شيئاً ]

أخرجه أبو داود 2/87

[Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu , Mola wangu simshirikishi na kitu chochote kile.]     [Imepokewa na Abuu Daud.]

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA NABII SULEIMAAN

Full story of theProphet Al-Yasa

Umuhimu Wa Dua Katika Uislamu Na Njia Ya Kuomba