SWALI: Je, inafaa kufunga siku sita za Shawwaal kabla ya kulipa deni la Ramadhwaan? Na inaruhusiwa kulipa kwa kufunga siku za Jumatatu na Alkhamiys katika mwezi wa Shawwaal kwa niyyah ya kulipa deni na niyyah ya kupata thawabu za Swiyaam za Sunnah ya Jumatatu na Alkhamiys? JIBU : Thawabu za kufunga Sittatu Ash-Shawwaal hazipatikani ila baada ya kukamilisha mwezi wa Ramadhwaan. Kwa hiyo kama mtu ana deni la Ramadhawan basi kwanza alipe deni kisha ndio afunge Siku Sita Za Shawwaal, kwani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: مَنْ صَامَ رَمَضَانَ ثُمَّ أَتْبَعَهُ سِتًّا مِنْ شَوَّالٍ كَانَ كَصِيَامِ الدَّهْرِ ((Atakayefunga Ramadhwaan, kisha akafuatia na Sitta za Shawwaal Swiyaam zake zitakuwa kama ni Swiyaam za mwaka)) [Muslim, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad, Ad-Daarimiy]. Kutokana na Hadiyth hiyo tunasema kwamba, yeyote mwenye deni la Swawm ya Ramadhwaan alipe kwanza kisha ndio afunge Siku Sita Za Shawwaal. Na ikiwa Siku Sita za Shaw...