Je, Mtu Akifunga Siku Tatu Au Tano Kwa Ajili Ya Sitta Shawwaal Atapata Thawabu?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Naam, atapata thawabu lakini hatopata thawabu ambazo ameziainisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika kauli yake:
“Atakayefunga Ramadhwaan kisha akafuatiliza na Sitta Shawwaal itakuwa kama ni Swiyaam ya mwaka” [Muslim]." [Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb, Kanda (75)]
Comments
Post a Comment