Je, Mwenye Deni La Ramadhwaan Atapata Thawabu Akifunga Sitta Shawwaal Kabla Kulipa Deni Lake?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
"Ni waajib kukimbilia kulipa deni hata kama Sitta Shawwaal zitampita kutokana na Hadiyth iliyotajwa na kwa sababu fardhi inatangulizwa kabla ya naafil (Sunnah)."
[Al-Fataawaa (15/393)]
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Hawezi mtu kupata thawabu za Swiyaam za Sitta Shawwaal isipokuwa ikiwa amemaliza Swiyaam za mwezi wa Ramadhwaan.
[Al-Fataawaa (18/20)]
Comments
Post a Comment