HISTORIA YA NABII SULEIMAAN
HISTORIA YA NABII SULEIMAAN Nabii Suleyman (AS) ni mtoto wa Nabii Daud (AS) Manabii hawa walijaaliwa na Mwenyeezi Mungu ilimu kubwa na Hikma. Walikuwa katika waja wema, wingi wa kushukuru kwa wanachoneemeshwa,wanyenyekevu na wepesi kurudi kwa mola wanapokosea,walijaaliwa ufalme ambao haukuwahi kuonekana toka dunia ianze hadi dunia itaisha.Ufalme wao ni ruzuku itokanao kwa muumba mbingu na Ardhi na ziliomo ndani.Na katika Manabii walojaaliwa kuzaa mtoto kwa kupewa Daraja ya Unabii ni Suleyman (AS)Na wengine walobahatika na hili ni Yahya (AS) babake ni Zakariya (AS).Na Ismael na nduguye Ishaq walizaliwa na Ebrahim (AS)Baba wa waumini wote. Mwenyeezi mungu anasema katika Surat Nnaml Aya 15. .Na hakika tuliwapa Daudi na Sulaiman ilimu, na wakasema: Alhamdu Lillahi, Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu aliye tufadhilisha kuliko wengi katika waja wake Waumini. Nabii Suleiman (AS) Qur’an imelitaja jina lake katika aya zipatazo 16. Suleiman (AS) alirithishwa kiti cha uf...
Comments
Post a Comment