MANABII NA MITUME WA ALLAH
MANABII NA MITUME WA ALLAH Assalam Alykum Warahmatullah Wabarakat. Pamoja na kwamba inasemwa kuwa idadi ya Manabii wanafika hadi 124,000 kutokana na baadhi ya mapokezi, lakini Hadiyth hizo zimedhoofishwa na hivyo hatuwezi kuzitegemea, ila kuna Hadiyth ambayo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) iliyosimuliwa na Abu Dhar ambayo alimuuliza Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) idadi ya Manabii (‘Alayhim wa sallam) na akamjibu kuwa ni mia tatu na makumi kadhaa. Hadiyth hiyo imeelezwa usahihi wake na Imaam Al-Albaaniy kama ilivyo hapa chini: عن أبي ذر ، قال : قلت : يا رسول الله ! أي الأنبياء كان أول ؟ ! قال : آدم ، قلت : يا رسول الله ! ونبي كان ؟ ! قال : نعم نبي مكلم ، قلت : يا رسول الله : كم المرسلون ؟ ! قال : ثلاث مئة وبضعة عشر ؛ جما غفيرا . الراوي: أبو ذر الغفاري - خلاصة الدرجة: صحيح - المحدث: الألباني - المصدر: مشكاة المصابيح - الصفحة أو الرقم: 566 Kutoka kwa Abu Dhar ambaye amesema: Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah...