HISTORIA YA NABII SULEIMAAN
HISTORIA YA NABII SULEIMAAN
Nabii Suleyman (AS) ni mtoto wa Nabii Daud (AS) Manabii hawa walijaaliwa na Mwenyeezi Mungu ilimu kubwa na Hikma. Walikuwa katika waja wema, wingi wa kushukuru kwa wanachoneemeshwa,wanyenyekevu na wepesi kurudi kwa mola wanapokosea,walijaaliwa ufalme ambao haukuwahi kuonekana toka dunia ianze hadi dunia itaisha.Ufalme wao ni ruzuku itokanao kwa muumba mbingu na Ardhi na ziliomo ndani.Na katika Manabii walojaaliwa kuzaa mtoto kwa kupewa Daraja ya Unabii ni Suleyman (AS)Na wengine walobahatika na hili ni Yahya (AS) babake ni Zakariya (AS).Na Ismael na nduguye Ishaq walizaliwa na Ebrahim (AS)Baba wa waumini wote.
Mwenyeezi mungu anasema katika Surat Nnaml Aya 15. .Na hakika tuliwapa Daudi na Sulaiman ilimu, na wakasema: Alhamdu Lillahi, Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu aliye tufadhilisha kuliko wengi katika waja wake Waumini.
Nabii Suleiman (AS) Qur’an imelitaja jina lake katika aya zipatazo 16. Suleiman (AS) alirithishwa kiti cha ufalme na baba yake Nabii Daud AS na urithi hu haukuwa ni urithi wa mali,sababu mitume na manabii hawarithi mali bali wanachokiacha huwa ni sadaka kwa maskini na mafukara.
Urithi alourithi Nabii suleyman (AS) ni Utume na Ufalme.kama alivosema Allah Subhaanahu Wataala katika Surat Nnaml Aya 16.
وَوَرِثَ سُلَيْمَانُ دَاوُودَ ۖ
وَقَالَ يَا أَيُّهَاالنَّاسُ عُلِّمْنَا مَنطِقَ الطَّيْرِ وَأُوتِينَا مِن كُلِّ شَيْءٍ ۖ إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ الْفَضْلُ الْمُبِينُ )
16.Na Sulaiman alimrithi Daudi, na akasema: Enyi watu! Tumefunzwa usemi wa ndege, na tumepewa kila kitu. Hakika hiini fadhila iliyo dhaahiri. Suleiman (AS) alineemeshwa na Mwenyezi Mungu tangia enzi za babaake Daud (AS).
Daud amani ya Mungu iwe juu yake, alipata daraja ya juu katika kusifiwa na Allah kwa ucha mungu na ufalme mkubwa.Alijaaliwa kizazi chema na watoto watiifu (wacha Mungu) na miongoni mwa watoto ni Suleyman AS aliyejaaliwa unabii ufalme hikma na elimu ya Lugha za wanyama. Utawala wa Nabii Suleyman (AS) ulikuwa muadilifu, utawala wa hukumu na sheria ya kitabu kitakatifu cha zaburi.
Utawala wa Daudi na mwanawe, (A.S):
Sisi tuliwapa ilimu nyingi za sharia na mazoezi ya kuhukumu. Wakasimamisha uadilifu, na wakamhimidi Mwenyezi Mungu aliye wapa fadhila kushinda wengi katika waja wake wenye kusadiki, na kuifuata. Ufalme na hukumu ukatoka kwa Daudi ukenda kwa mwanawe, Sulaiman; naye akasema:
Enyi watu! Sisi tumefunzwa lugha ya ndege, na tumepewa mengi tunayo yahitajia katika utawala wetu. Hakika neema hizi ni fadhila iliyo wazi aliyo tukhusisha sisi toka kwa Mwenyezi Mungu.
Sulaiman (A.S) Aliishi Kabla ya Kuzaliwa Nabii Isa). Mwenyezi Mungu alimjaalia kumjuvya kufahamu maneno ya ndege. Uchunguzi wakisasa umeonyesha kwamba kila namna ya ndege wana njia zao za kufahamiana wao kwa wao. Katika njia hizo ni kwa kugusa, na sauti, na ishara.
Nabii Suleyman AS alihukumu taifa lake kwa hukmu ile ile alokuwa akiwahumu nayo Daud (AS). Wafuasi wake walikuwa ni watu wa karimu na wepesi kufuata wanayoamrishwa. Siku moja Alipokuwa katika matembezi yake aliona ndege mume akimzunguka ndege mke.Nabii Suleyman AS akawauliza alokuwa amefuata nao,mwajuwa,
KISA HIKI NI KIREFU HIVYO KATIKA APP IITWAYO KISA CHA NABII SULEYMAN iliopo Google Playstore
Comments
Post a Comment