SIRA YA NABII ISSA (A.S)
SIRA YA NABII ISSA (A.S)
Disemba 25 ni siku inayosadifiana na kumbukumbuu ya kuzaliwa Nabii Issa Masiya mwana wa Maryamu (Alayhas salaam) kwa mujibu wa imani ya Wakristo wengi.
Mtume huyo mwema alikuwa mtoa bishara njema na mlinganiaji wa kweli na upendo na itikadi na Mungu Mmoja. Isa Masiih alizungumza kwa amri ya Allaah akiwa katika susu na kuwaambia watu waliokuwa katika mghafala wa zama hizo kama inavyotwambia aya ya 30 hadi 33 za Surat Maryam kwamba:
قَالَ إِنِّي عَبْدُ اللَّهِ آتَانِيَ الْكِتَابَ وَجَعَلَنِي نَبِيًّا
وَجَعَلَنِي مُبَارَكًا أَيْنَ مَا كُنتُ وَأَوْصَانِي بِالصَّلاةِ وَالزَّكَاةِ مَا دُمْتُ حَيًّا
وَبَرًّا بِوَالِدَتِي وَلَمْ يَجْعَلْنِي جَبَّارًا شَقِيًّا
وَالسَّلامُ عَلَيَّ يَوْمَ وُلِدتُّ وَيَوْمَ أَمُوتُ وَيَوْمَ أُبْعَثُ حَيًّا
“Na akasema: Hakika mimi ni mja wa Allaah, amenipa kitabu na kunifanya Nabii. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo na ameniusia Swala na Zaka maadamu ni hai. Na kumtendea wema mama yangu. Wala hakunifanya jeuri, muovu. Na amani iwe juu yangu siku niliyozaliwa, na siku nitakayokufa, na siku nitakayofufuliwa."*_ [Maryam aya ya 30 hadi 33]
Kuzaliwa kwake
Nabii Issa AS alizaliwa katika zama ambazo makundi mbalimbali ya Kiyahudi yalikuwa yamezama katika hitilafu na migawanyiko mikubwa. Makundi mawili makuu ya Wasadukayo (Sadducees) na Mafarisayo (Pharisees) yalikuwa yakidhibiti na kutawala itikadi za watu wa zama hizo. Wasadukayo (Sadducees) lilikuwa kundi la mabwanyenye na aghalabu yao walikuwa makuhani na wanazuoni wa kidini ambao walikuwa wakishirikiana na utawala wa kifalme wa Roma kwa ajili ya kulinda mafundisho na ada za kidini na hawakukabiliana kwa njia yoyote ile ya utamaduni wa Kigiriki. Hii ni kwa sababu walikuwa wakiamini kwamba, Mwenyezi Mungu pia ameeneza maadili ya Kitabu Kitakatifu kati ya wasio Wayahudi. Mkabala wake, Mafarisayo (Pharisees) lilikuwa kundi lisilo la makuhani lakini lenye ushawishi mkubwa zaidi kuliko Wasadukayo (Sadducees). Kundi hili liliamini kuwa, kaumu ya Mayahudi inapaswa kuwa kaumu tofauti na iliyojitenga na kaumu nyinginezo na haipasi kufuata kaumu hizo au kuchanganyika nazo. Kundi la Mafarisayo (Pharisees) lilikuwepo katika maeneo yote ya Palestina na lilidhibiti masinagogi na maabadi zote za nje ya Beitul Muqaddas (Jerusalem) ambako Mayahudi walikuwa wakikusanyika kwa ajili ya ibada au kusoma.
Mbali na makundi hayo mawili makuu, kulikuwepo makundi mengine kama Samaritans (Wasamaria) na kundi na Wayahudi wenye misimamo mikali lililokuwa maarufu kama Zealots. Wasamaritani katika mtazamo wa makundi mengine, walitambuliwa kuwa makafiri, na Zealots lilikuwa kundi la Mayahudi wenye misimamo ya kuchupa mipaka la kisiasa lililokuwa likiwachochea Mayahudi kuwafukuza kwa mabavu na kwa njia za mauaji ya kigaidi Warumi na utawala wao katika ardhi ya Palestina. Kundi hili halikushambulia Warumi pekee, bali hata Wayahudi wenzao ambao kwa madai yao, hawakuwa na ghera ya kutosha ya udini na utaifa.
“Utabiri uliopuuzwa na Mayahudi”
Nabii Issa Masih alizaliwa katika mazingira kama haya. Wakuu wa kaumu ya Mayahudi katika kila kundi walijua vyema sifa na alama zake kutokana na utabiri wa hapo kabla na habari walizosoma na kukusanya katika vitabu vya kale. Hata hivyo walipuuza utabiri na alama hizo tangu hapo mwanzoni na kukabiliana na Nabii huyo mkubwa wa Allaah. Hatua ya kwanza kabisa ya Mayahudi hao ilikuwa kumtuhumu mama yake Masih, Bibi Maryam (Alayhas salaam) kuwa ni fasiki ili wapate kumrujumu mbele ya kadamnasi. Hata hivyo njama hiyo ilifeli, na Issa na mama yake, Bibi Maryam wakaokoka kifo na vitimbi vya Mayahudi baada ya Masih kuzungumza akiwa kwenye susu na kusema:
إِنِّي عَبْدُ اللَّهِ آتَانِيَ الْكِتَابَ وَجَعَلَنِي نَبِيًّا
_"Hakika mimi ni mja wa Allaah, amenipa kitabu na akanijaalia kuwa Nabi..". [Maryam aya ya 30]
Nabii Issa (Alayhis salaam) alibaathiwa na kuamrishwa kutangaza ujumbe wa Mwenyezi Mungu baina ya Banii Israel akiwa na umri wa karibu miaka 30. Alifanya jitihada kubwa za kuwaongoza katika ukweli na haki na kuwaondoa katika upotovu. Aliwabainishia halali na haramu na kuwahalalishia mengi waliyokuwa wamekatazwa. Kwa mujibu wa Injili ya Mathayo 4/17 ni kwamba Issa alianza kuhubiri kwa kusema: "Tubuni, kwa sababu Ufalme wa mbinguni umekaribia.
HISTORIA HII NI NDEFU HIVYO INAPATIKANA KATIKA APP YA HISTORIA YA NABII ISSA iliyopo Google Playstore

Comments
Post a Comment