KISA CHA NABII MUSSA
KISA CHA NABII MUSSA
Jina lake kamili ni Musa bin Umraan bin Wahib bin Laawy bin Yaakub bin Ishaaq bin Ibrahim (AS). Pia inasemekana kuwa ni Musa bin Umraan bin Yashar bin Faahib bin Laawy bin---. Mama yake jina lake Yuhab (pia inasemeka jina lake ni Afahiyah) ambae vile vile ni mama yake Harun (AS).
Bani Israiyl waliishi huko Misri kutokea wakati wa Yusuf (AS). Na hawa Bani Israiyl wanatokana na Yaakub (AS), ambae akijulikana kwa jina la Israiyl. Kama tulivyoona katika hadithi ya Yusuf (AS), aliwachukuwa wazee wake pamoja na ndugu zake kutoka Falastini wakahamia Misri na kaishi huko. Wanasema waandikaji historia kuwa walipoingia Misri walikuwa watu thamanini na sita, wakazaliana na alipokuja Musa (AS) kutoka nao Misri walikuwa idadi yao laki sita. Firauni (Mfalme) aliyehukumu wakati wa Yusuf (AS) alikuwa jina lake Rayyan bin Alwalid, na Firauni huyu alimuachilia Yusuf (AS) mambo mengi ya kuendesha nchi kwa vile Yusuf (AS) alivyoiokowa nchi katika njaa kubwa. Wakaiishi Bani Israiyl maisha ya raha kabisa wakati huo, nao wakitukuzwa sana. Baada ya kufa Rayyan, alihukumu Firauni Qaboos bin Musaab. Huyu alikuwa mtu dhalimu na kafiri mkubwa, nae akawa anawaadhibu sana Bani Israiyl baada ya kufa Yusuf (AS).
Baada ya Firauni huyu alikuja ndugu yake, Alwalid bin Musaab bin Muawia bin Abi Namir, nae ni wa nne katika ma Firauni wa Misri. Mkewe jina lake Bibi Asiya bint Muzaahem (RAAH), na huyu bibi alikuwa mtu muumin. Akataka Firauni amchukuwe kutoka kwa baba yake kwa nguvu, lakini baba yake akamwambia ikiwa anamtaka atowe mahari yake. Na baba yake alipokuja kumwambia Bibi Asiya habari hii, alikataa kwanza kwa kusema hataki kuolewa na kafiri. Baba yake akamwambia kuwa akikataa basi yeye na watu wake wote wataadhibiwa, akakubali kuolewa. Akaishi nae lakini hakuwa katika raha.
Firauni huyu alifikia ujabaruti wake kupindukia kiasi akajiita kuwa yeye ni mungu. Anasema Mwenyenzi Mungu: Na Firauni akasema: ‘Enyi wakuu ! Simjui kwa ajili yenu mungu asiyekuwa mimi. .
Pia amesema Akasema : ‘Mimi ndiye mola wenu mkuu. (Huyo Mola wake Musa ni mdogo.)’
Kuzaliwa na Kulelewa Kwake
Musa (AS) alizaliwa huko Misri katika zama za Firauni Alwalid bin Musaab. Firauni huyu aliwagawa watu katika tabaka mbali mbali, na wale aliowaweke katika tabaka ya chini kabisa ni hawa Bani Israiyl. Akawa anawatesa hao Bani Israiyl na kuwafanya watu wa chini kabisa, kwani akisema asili zao ni wachunga wanyama na ni watu waliokuwa wakishi katika majangwa. Aliwafanya kama watumwa na kuwatumia katika kazi ngumu, pia akiwatumilia wanawake zao anavyotaka.
Hawa Bani Israiyl walikuwa wana utabiri kuwa atakuja kijana kutoka nyumbani kwa Firauni na kuwaokowa katika adhabu hiyo waliyokuwa nayo. Pia inasemekana kuwa Firauni aliota ndoto usingizini, kaona moto mkubwa unatokea upande wa Baitil-Maqdis na kuingia Misri, ukaunguza kila mtu isipokuwa walisalimika Bani Israiyl. Wakaja Makuhani wakamwambia kuwa atazaliwa mtoto mwanamume katika watu wa Bani Israiyl ambae atampindua katika ufalme wake.
Basi akatoa amri ya kuwa akizaliwa mtoto wa kiume katika Bani Israiyl lazima auliwe. Ilipotoka amri hii Harun (AS) alikuwa ameshazaliwa, na mama yake alikuwa ana mimba ya Musa (AS) katika miezi yake ya mwanzo lakini aliificha mimba yake nae alikuwa hatoki nje. Alipokuja kuzaa hakuna mtu aliyejuwa isipokuwa wale watu wake wa nyumbani. Akazaliwa Musa (AS); mama yake hakuweza kumchukua mwanawe akauawe, akawa anamficha. Kwa Miujiza yake Mwenyenzi Mungu, akateremshiwa Wahyi (ufunzi) mama yake akaambiwa amnyonyeshe mtoto wake na atapomuogopea basi amtie katika sanduku kisha amtupe mtoni (mto wa Nile).
Kuzaliwa kwa Musa(a.s)
Musa(a.s) alizaliwa wakati bado msako unafanywa na askari wa Firauni kumwua kila mtoto wa kiume wa Kiisrail anayezaliwa. Kwa rehema zake Allah(s.w) mama yake Musa alijifungua bila kutambulika kwa askari wa Firauni. Na ili kumlinda zaidi Allah(s.w) alimteremshia Wahy mama yake Musa.
Ya kwamba mtie sandukuni, kisha litie mtoni, na mto utamtupa ufukoni ili amchukue adui yangu na adui yake (amlee kwa vizuri Naye ni Firaun). Na nimekutilia mapenzi yatokanayo kwangu (ili upendwe na watu wote), na ili ulelewe machoni mwangu.(20:39)
Baada ya kumtupa mtoni, mama yake akamtuma dada yake Musa kufuatilia: Akamwambia dada yake: “Mfuate”. Basi yeye akamwangalia kwa mbali bila wao kumjua (28:11)
Kitoto Musa kiliokotwa na kufikishwa kwa Firaun. Mkewe Firaun akamrai mumewe kuwa wasimuue bali wamfanye mtoto wao wa kulea. Na mkewe Firauni akasema (Kumwambia mumewe)
“Usimuuwe, atakuwa kiburudisho cha macho kwangu na kwako; na msimuuwe;huwenda atatunufaisha, au tumpange kuwa mtoto wetu,walisema haya hali ya kuwa hawatambui(kuwa atakuwa adui yao)”(28:9)
Watu wa Firauni walipomwokota Musa bila shaka walitambua kuwa ni mtoto wa Kiisrail na walimpeleka kwa Firauni ili auawe kama watoto wengine Wakiisrail.
Lakini mke wa Firauni alivutiwa na uzuri wa mtoto Musa. Ambaye kwa kweli Allah(s.w) alimfanya awe ni mwenye kupendeza machoni kwa watu.
Allah(s.w) Amruzuku Musa(a.s)
Elimu Ili kuweza kutekeleza jukumu la kutetea haki za binadamu na kuwaongoza watu katika njia iliyonyooka, Mwenyezi Mungu akamjaalia Musa elimu ya kutosha na akili yenye upeo mkubwa wa kupembua mambo.
Tunafahamishwa kuwa:
Na Musa alipofikia baleghe yake na kustawi, tulimpa akili na elimu, na hivi ndivyo tunavyowalipa watu wema (28:14)
Usiogope umekwisha kuokoka na watu madhalimu (28:25)
Akasema: Mimi nataka nikuoze mmoja wapo katika binti zangu hawa wawili kwa kunitumikia miaka minane na kama ukitimiza kumi hiari yako, lakini mimi sitaki kukutaabisha utanikuta Inshaa-Allah miongoni mwa watu wema .(28:27)
Musa(a.s) aliafiki suala hilo, na mmoja katika wale mabinti aliridhia kuolewa na Musa(a.s) kwa mahari ya kutoa nguvukazi:
“Akasema(Musa: “Mapatano) hayo yamekwisha kuwa baina yangu na baina yako; muda mmoja wapo nitakaoumaliza, basi nisidhulumumiwe; na Mwenyzi Mungu ni Mlinzi juu ya haya tunayoyasema.”(28:28)
Musa(a.s) Ahamia Madiani
Mchana wa siku moja Musa(a.s) alimuona mtu wa Firauni amemuelemea Muisrail akimtwanga makonde mazito.
Musa alichukizwa na kitendo kile, hivyo alipoombwa msaada alijikuta amemtwika Mmisri huyo ngumi nzito na kumuuwa palepale.
Hapo Musa(a.s) akashituka na kuleta toba:
Mola wangu! Bila shaka nimedhulumu nafsi yangu, basi nisamehe; naye (Allah) akamsamehe. Kwa hakika yeye ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu. (28:16)
Akasema: Mola wangu! Kwa kuwa umenineemesha, basi sitakuwa kabisa msaidizi wa watu wabaya. (28:17)
Habari ile ya kuuliwa mtu na Musa(a.s) ilifika kwa Firaun na ikatoka shauri kuwa Musa(a.s) akamatwe na kuuliwa. Musa(a.s) alipopata habari za kuaminika kutoka kwa mtu mwema,kuhusu hukumu ile, aliamua kutorokea nchini Madian katika mji awa Al-Bid uliopo kilometa 480 hivi mashariki ya Misr.
Alipofika Madian hakuwa na pakwenda bali alijipumzisha kisimani ambapo aliwasaidia wasichana wawili kuwanywesha wanyama wao. Wasichana wale hawakuweza kupigana vikumbo na wanaume katika kunywesha wanyama wao, wakawa tu wanabakia pembeni wanaangalia.
Kitendo kile kilimfurahisha Mzee wa Madian na akaagiza Musa(a.s) aitwe ili apate ujira wa kazi ile. ........... Basi akamjia mmoja katika (wasichana) wale wawili, anakwenda na huku anaona haya, akasema:
“Baba yangu anakuita ili akulipe ujira wa kutunyweshea..........(28:25)
Musa alipofika kwa yule mzee alimsimulia hali halisi kuhusu dhulma, ukandamizaji na ukiukwaji wa haki za binadamu uliopo nchini Misri, pamoja na kisa kilichompelekea yeye kuhamia Madiani.
Musa(a.s)Kupewa Utume Rasmi
Musa alipotimiza muda, alifunga safari na ahali zake kurejea Misri. Njiani aliona moto upande wa mlimani akawaambia ahali zake:
Ngojeni hakika nimeona moto; labda nitakujieni na habari za huko au kijinga cha moto ili muote (28:29)
Basi alipofika, aliitwa: “Ewe Musa! Hakika Mimi ndiye Mola wako. Basi vua viatu vyako. Hakika wewe uko katika bonde takatifu la Tuwa. (20:11-12)
Nami nimekuchagua, (uwe Mtume). Basi yasikilize unayoelezwa kupitia wahy.
Kwa yakini Mimi ndiye Mwenyezi Mungu, hakuna aabudiwaye kwa haki ila Mimi, Basi niabudu na usimamishe swala kwa kunitaja (20:13-14)
Miujiza Kama Ushahidi wa Utume wa Nabii Musa(a.s)
Allah(s.w) alimjaalia Nabii Musa(a.s) miujiza ya kuthibitisha Utume wake. Miujiza si viinimacho kama ilivyo mazingaombwe. Muujiza ni jambo halisi lisilola kawaida ambalo hutokea kwa idhini ya Allah(s.w). Musa alipoulizwa na Allah(s.w) kuwa ameshika nini alisema:
..Akasema: “Hii ni fimbo yangu, ninaiegemea na ninaangushia majani kwa ajili ya wanyama wangu. Tena ninaitumia kwa mambo mengine.(20:18)
Inadhihirika hapa kuwa Nabii Musa alikuwa na fimbo ya kawaida kabisa, lakini Allah(as) anaigeuza kuwa muujiza.Allah(s.w) akasema:
Itupe, ewe Musa”. Akaitupa. Mara ikawa nyoka anayekwenda mbio. Allah akasema: “Ikamate wala usiogope, sasa hivi Tutairudisha hali yake ya kwanza.(20:19-21)
“Na uambatanishe mkono wako katika kwapa lako; utatoka ukiwa mweupe sana pasipo na ubaya wowote. Huu ni muujiza mwingine. Ili Tukuoneshe miujiza mingine mikubwa (20:22-23)
Inabainika wazi kuwa chanzo cha miujiza yote aliyokuwa nayo Musa na Mitume wengine, ni Allah(s.w). Hakuna Mtume au Nabii aliyefanya miujiza kwa uweza wake mwenyewe!
Harun(a.s), Achaguliwa Kuwa Msaidizi Musa(a.s)
Nabii Musa(a.s)alimuomba Allah(s.w) amsaidie(amuwezeshe) kulimudu jukumu zito alilompa na pia alimuomba amfanye Harun(a.s) awe msaidizi wake. Harun alikuwa ndugu yake Musa(a.s)Akasema:
Ewe Mola wangu! Nipanulie kifua changu(nipe subira). Na unifanyie wepesi katika kazi yangu. Na ufungue fundo lililo katika ulimi wangu. Wapate kufahamu maneno yangu. Na unifanyie waziri katika jamaa zangu. Ndugu yangu Harun. Nitie nguvu kwa huyu. Na umshirikishe katika kazi yangu hii. Ili tukutukuze sana. Na tukutaje kwa wingi. Hakika Wewe unatuona (20:25-35)
Allah(s.w) alilikubali ombi la Nabii Musa (a.s), akamfanya Harun(a.s) kuwa Nabii pamoja naye. Allah(s.w) akasema kumwambia Musa: Hakika umekubaliwa maombi yako, Ewe Musa (20:36)
Lakini Musa(a.s) hakutishika kabisa kwa hizo kauli za Firauni. Badala yake akataka kumdhihirishia kuwa Allah(s.w) ana nguvu na uweza wa kufanya mambo makubwa ya kutisha zaidi kuliko hayo magereza yake. Basi(Musa) akatupa fimbo yake, mara ikawa nyoka aliye dhahiri. Na akatoa mkono wake, na mara ukawa mweupe (kweli kweli) kwa watazamao(26:32-33)
Hapo Firaun akatishika na alidhani kuwa ile miujiza aliyokuja nayo Nabii Musa(a.s) ni sawa na mazingaombwe au viinimacho wanavyofanya wachawi.
Akasema, kuwaambia wakuu waliomzunguka: Hakika huyu ni mchawi ajuae sana. Anataka kukutoeni katika nchi yenu kwa uchawi wake; basi mnasemaje? (26:34-35)
Musa na Harun(a.s) Kumkabili Firaun
Jukumu kubwa la kwanza walilokabidhiwa Musa(a.s) na Harun(a.s) lilikuwa kumwambia Firauni amwamini Allah(s.w) na awache kukiuka haki za binadamu kwa kuwapa Waisraili uhuru wao. Basi wakamkabili Firaun wakamwambia:
....Kwa hakika sisi ni Mitume wa Mola wako. Basi waachie wana wa Israili watoke pamoja nasi, wala usiwaadhibu. Hakika tumekuletea ishara zitokazo kwa Mola wako. Na amani itakuwa kwa wale wanaofuata uongofu (20:47)
Firauni kwa jinsi alivyokuwa amezama katika siasa za kidhalimu na unyonyaji hakupenda kabisa kuona Wana Israil wanarejeshewa haki zao za kibinadamu za kuwa huru. Akasema Firauni kwa kibri na jeuri kubwa kuwa: Enyi wakuu! Simjui kwa ajili yenu, mungu asiyekuwa mimi...(28:38) Akasema: Mimi ndiye mola wenu mkuu. (79:24)
Nabii Musa(a.s.) alijitahidi kumuelimisha Firauni na watu wake juu ya Mungu mmoja anayekataza dhulma, ukandamizaji na ukiukaji wa haki za binadamu. Lakini Firauni kwasababu ya kupenda sana dhulma, akazusha uongo akiwatangazia watu kwa kuwaambia:
Bila shaka Mtume wenu aliyetumwa kwenu ni mwendawazimu(26:27)
Pamoja na kujibiwa kwa dharau na kukashifiwa, Musa aliendelea kufafanua zaidi juu ya Mwenyezi Mungu anayemiliki ulimwengu mzima. ..(Allah ndiye) Mola wa Mashariki na Magharibi na vilivyomo baina yake ikiwa (mna akili) mfahamu (26:28)
Aliposhindwa kujibu hoja hiyo, Firauni akapandwa na hasira na kuanza kumtishia Musa(a.s): Firauni akasema: Kama ukishikilia (kuwa kuna) Mungu mwingine badala yangu, kwa hakika nitakufanya miongoni mwa wenye kufungwa gerezani(26:29)
Kuangamizwa Firauni na Majeshi Yake
Baada ya ushindi alioupata Musa(a.s) dhidi ya wachawi, umati wa watu waliokuwa wamekusanyika kushuhudia mapambano baina ya haki na batili, waliona ukweli kuwa Musa(a.s) ndiye kiongozi halali anayepaswa kutiiwa, na haifai kabisa kutiiwa Firauni dhalimu. Kuanzia hapo waliomuamini Musa wakapata adha na mateso zaidi kutoka kwa Firauni. Ndipo Allah(s.w) alipomuamuru Musa(a.s): “Nenda na waja wangu wakati wa usiku(mtoke nchini Misri), bila shaka mtafuatwa (26:52)
Na yalipokutana majeshi mawili. Watu wa Musa walisema. Hakika tutakamatwa. Musa akasema: La, kwa yakini Mola wangu Yu pamoja nami bila shaka ataniongoza.(26:61-62)
Wana Israil walikuwa wamekwama kuendeleana safari kutokana na kuzuiwa na bahari hali ya kuwa Firauni na majeshi yake yamekwisha wakaribia. Kwa huruma na rehema zake, Allah(s.w) akamuongoza Musa kwa kumwambia: Piga bahari kwa fimbo yako; basi ikatengana, na kila sehemu ikawa kama mlima mkubwa. (26:63)
Bahari iligawanyika sehemu mbili na kuwacha njia ambayo Nabii Musa alipita na watu wake kwa salama. Lakini majeshi ya Firaun yalipofika katikati,maji ya bahari yalirudi katika nafasi yake na kuangamizwa yote. Firaun akawa anatapatapa, akijitupa huku na kule na akaona kuwa hapana nusra ila kutoka kwa Allah(s.w) ndipo akatoa shahada kuwa: .
.Naamini ya kwamba hakuna Mola aabudiwaye kwa haki ila Yule wanayemuamini wana wa Israeli, na mimi ni miongoni mwa wanaotii (10:90)
(Malaika wakamwambia)” Sasa (ndio unaamini)! hali uliasi kabla ya hapo na ukawa miongoni mwa waharibifu. Basi leo tutakuokoa kwa kuuweka mwili wako ili uwe dalili kwa ajili ya wa nyuma yako. Na watu wengi wameghafilika na ishara zetu.(10:91-92)
Huo ukawa ndio mwisho wa utawala wa kifirauni.
Kusilimu kwa Wachawi wa Firaun
Mawaziri waliokuwa washauri wakuu wa Firauni wakataka wakusanywe magwiji waliobobea katika uchawi nchi nzima, kisha wapambanishwe na Nabii Musa(as).
Basi walipofika wachawi, wakamwambia Firauni: Je, tutapata ujira tukiwa sisi ndio tutakaoshinda. Akasema: Naam, na pia mtakuwa miongoni mwa wale wanaowekwa mbele katika (Serikali) (26:41-42)
Basi wakatupa kamba zao na fimbo zao, na wakasema: Kwa nguvu za Firauni sisi tutakuwa ndio wenye kushinda (26:44)
Kisha Musa akatupa fimbo yake, nayo mara ikavimeza(vyote) walivyozusha wachawi (26:45)
Wachawi walipoona vitu vyao vya kichawi(viini macho) walivyovitupa uwanjani vimemezwa vyote na nyoka(wa muujiza), walisalimu amri na kutoa shahada:
Hapo wachawi walipinduka wakasujudu. Wakasema: Tumemuamini Mola wa walimwengu wote. Mola wa Musa na Harun (26:46-48)
Firaun aliwatishia wachawi kuwapa adhabu kubwa kwa kusilimu kwao pasina idhini yake (Qur’an 26:49).
Inabainika hapa kuwa uchawi si sawa na muujiza,na ndio maana wachawi walishindwa. Hakika uliwadhihirikia ukweli kwamba Musa(a.s) ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Ndio maana Firauni alipotangaza kuwa atawasulubu kwa kuwakata miguu na mikono yao kwa sababu wamesilimu pasina ridhaa yake; hawakuyumba katika imani yao. Wakasema:
Haidhuru, hakika sisi sote tutarejea kwa Mola wetu. Kwa yakini sisi tunatumai ya kwamba Mola wetu atatusamehe makosa yetu, maana sisi tumekuwa wa kwanza wa wenye kusilimu hapa (26:50-51)
(xiv)Hapana yeyote wa kumchelea katika kutekeleza amri ya Allah(s.w) ya kusimamisha Uislamu katika jamii. Musa na Harun(a.s) walimkabili Firaun na wakuu wake wa Dola waliozungukwa na majeshi na kuwafikishia ujumbe wa Allah(s.w).
(xv)Hapana yeyote mwenye uwezo wa kutweza au kutengua maamuzi ya nafsi ya mwanaadamu.Wachawi walipobainikiwa na Haki na wakasilimu, Firaun hakuweza kuwaritadisha pamoja na adhabu kali aliyoitoa dhidi yao Qir-an (26:49-51).
(xvi)Toba inayokubalika ni ile inayoletwa haraka kabla ya kufikwa na mauti – Qur-an (4:18).
(xvii)Kuishi nje ya shahada na kutarajia kufa ndani ya shahada ni muhali. Allah(s.w) ametuamrisha tuishi na shahada na tujitahidi kubakia nayo mpaka kufa kwetu– Qur-an (3:102).
(vii)Muumini wa kweli hanabudi kuchukia vitendo vya dhuluma na kuwa tayari kuwatetea wanaodhulumiwa haki zao kwa kadiri ya uwezo wake.
(viii)Ni muhimu kuwekeana mikataba ya kazi tunapoajiri au kuajiriwa. Nabii Musa(a.s) aliwekeana mkataba wa kazi na mzee wa Madian.
(ix) Nyenzo muhimu ya kutuwezesha kusimamisha Uislamu katika jamii baada ya Elimu ni kusimamisha Swala za Faradh na sunah,Qiyamullayl na kuleta dhikiri kwa wingi – Qur-an(20:14), (73:1-10), (74:1-7).
(x) Miujiza ni katika dalili za kuwepo Allah(s.w).
(xi) Katika harakati za kusimamisha Uislamu katika jamii tunatakiwa tusimvamie tu kila mtu na kumuingiza kwenye harakati, bali tuanze na ndugu, jamaa na rafiki wa karibu ambao tunajua fika tabia na mwenendo wao.
Nabii Musa (a.s) aliomba ndugu yake Harun awe msaidizi wake si kwa kuwa alikuwa ndugu yake tu, bali alimfahamu fika kwa ucha Mungu wake.
(xii)Muumini mwanaharakati hahongeki kwa fadhila atakazofanyiwa na madhalimu ili arudi nyuma katika kusimamisha uadilifu. Musa(a.s) alilelewa katika nyumba ya mfalme,lakini hakuacha kudhihirisha kwa matendo udhalimu wa Firaun na serikali yake ikawa ndio sababu ya kuhukumiwa kifo.
(xiii)Ni kawaida ya matwaghuti kufanya propaganda dhidi ya wanaharakati na kuwapachika majina mabaya. Firaun na serikali yake alimpakazia Nabii Musa(a.s) uwendawazimu na uchawi.
Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Musa(a.s) na Harun(a.s)
Kutokana na Historia ya Nabii Musa na Harun(a.s) tunajifunza yafuatayo:
(i) Tunajifunza kuwa ni muhimu kuweka mipango katika kuhuisha na kusimamisha Uislamu katika jamii. Allah(s.w) anauwezo wa kukiamrisha kitu “kiwe” na kikawa pale pale, lakini bado tunaona ameweka mpango wa muda mrefu wa kuwaokoa Bani Israil na makucha ya Firaun.
(ii) Vile vile mpango huu wa Allah(s.w) wa kuwakomboa Bani Israil,unatufunza kuwa kuibadilisha jamii ya kijahili kuwa ya Kiislamu ni jambo linalohitaji muda na subira.
(iii) Elimu na siha ni nyenzo muhimu za kumuwezesha mtu kuwa khalifa katika ardhi. Nabii Musa alipewa siha nzuri na kuruzukiwa akili na elimu.
(iv) Hakuna hila wala nguvu zinazoweza kuzuia jambo analotaka Allah(s.w) liwepo au lisiwepo katika jamii, yeye anazo namna nyinyi za kumlinda mja wake na vile vile anaweza kumuangamiza mbabe yeyote awaye.
(v) Tabia njema na kuwatendea watu wema ni nyenzo muhimu katika harakati za kusimamisha Uislamu katika jamii. Nabii Musa(a.s)kwa wema wake aliletewa taarifa ya mipango ya Firaun dhidi yake; pia kwa huruma yake alipata hifadhi kwa mzee wa Madian.
(vi) Hakuna binaadamu asiyeteleza na kumkosea Allah(s.w), lakini muumini anakuwa mwepesi wa kurejea kwa Allah (s.w).Musa(a.s) aliteleza kwa kuingilia ugomvi asioujua na kumuua mtu,alirejea kwa Mola wake haraka haraka–Qur-an (28:16).

Comments
Post a Comment