MANABII NA MITUME WA ALLAH

MANABII NA MITUME WA ALLAH

Assalam Alykum Warahmatullah Wabarakat.

Pamoja na kwamba inasemwa kuwa idadi ya Manabii wanafika hadi 124,000 kutokana na baadhi ya mapokezi, lakini Hadiyth hizo zimedhoofishwa na hivyo hatuwezi kuzitegemea, ila kuna Hadiyth ambayo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) iliyosimuliwa na Abu Dhar ambayo alimuuliza Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) idadi ya Manabii (‘Alayhim wa sallam) na akamjibu kuwa ni mia tatu na makumi kadhaa. Hadiyth hiyo imeelezwa usahihi wake na Imaam Al-Albaaniy kama ilivyo hapa chini:

عن أبي ذر ، قال : قلت : يا رسول الله ! أي الأنبياء كان أول ؟ ! قال : آدم ، قلت : يا رسول الله ! ونبي كان ؟ ! قال : نعم نبي مكلم ، قلت : يا رسول الله : كم المرسلون ؟ ! قال : ثلاث مئة وبضعة عشر ؛ جما غفيرا .

الراوي: أبو ذر الغفاري  -  خلاصة الدرجة: صحيح  -  المحدث: الألباني  -  المصدر: مشكاة المصابيح  -  الصفحة أو الرقم: 566

Kutoka kwa Abu Dhar ambaye amesema: Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah, Nabiy yupi wa mwanzo? Akasema: ((Aadam)). Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah, alikuwa ni Nabiy? Akasema: ((Ndio Nabiy aliyesemeshwa)) Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah. Wapo Manabii wangapi? Akasema: ((Mia tatu na makumi kidogo)) [Mishkaat Al-Maswaabiyh ikiwa na daraja ya Swahiyh]

Hata hivyo idadi iliyotajwa katika Qur-aan ni Rusuli 25 pekee na dalili ni kauli ya (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

  وَرُسُلاً قَدْ قَصَصْنَاهُمْ عَلَيْكَ مِن قَبْلُ وَرُسُلاً لَّمْ نَقْصُصْهُمْ عَلَيْك 

Na Rusuli Tuliokwishakusimulia kabla; na Rusuli (wengine) Hatukukusimulia.[An-Nisaa: 164] 

Rusuli 18 wametajwa kwa pamoja katika Aayah 4 zifuatazo zinazofuatana:

وَتِلْكَ حُجَّتُنَا آتَيْنَاهَا إِبْرَاهِيمَ عَلَىٰ قَوْمِهِ ۚ نَرْفَعُ دَرَجَاتٍ مَّن نَّشَاءُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ﴿٨٣﴾ وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۚ كُلًّا هَدَيْنَا ۚ وَنُوحًا هَدَيْنَا مِن قَبْلُ ۖ وَمِن ذُرِّيَّتِهِ دَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَىٰ وَهَارُونَ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿٨٤﴾  وَزَكَرِيَّا وَيَحْيَىٰ وَعِيسَىٰ وَإِلْيَاسَ ۖ كُلٌّ مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿٨٥﴾ وَإِسْمَاعِيلَ وَالْيَسَعَ وَيُونُسَ وَلُوطًا ۚ وَكُلًّا فَضَّلْنَا عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٨٦﴾

Na hiyo ndio hoja Yetu Tuliyompa Ibraahiym juu ya watu wake.  Tunampandisha cheo Tumtakaye. Hakika Rabb wako ni Mwenye hikmah wa yote, Mjuzi wa yote. Na Tukamtunukia Is-haaq, na Ya’quwb. Wote Tukawahidi. Na Nuwh Tulimhidi kabla. Na katika dhuria wake Daawuwd, na Sulaymaan, na Ayyuwb, na Yuwsuf, na Muwsaa, na Haaruwn. Na hivyo ndivyo Tulipavyo wafanyao ihsaan.  Na Zakariyyaa, na Yahyaa, na ‘Iysaa, na Ilyaas. Wote ni miongoni mwa Swalihina. Na Ismaa’iyl, na Al-Yasa’a na Yuwnus, na Luutw. Na wote Tuliwafadhilisha juu ya walimwengu. [Al-An’aam:  83-86]

Manabii na Rusuli waliotajwa katika Qur-aan kwa mpangio wa ujio ni kama ifutavyo:

  1.  Aadam
  2. Idriys
  3.  Nuwh
  4. Huwd
  5. Swaalih
  6. Ibraahiym
  7.  Luutw
  8. Ismaa'iyl bin Ibraahiym
  9. Is-haaq bin Ibraahiym
  10. Ya'quwb bin Is-haaq bin Ibraahiym
  11. Yuwsuf bin Ya'quwb bin Is-haaq bin Ibraahiym
  12.  Shu'ayb
  13. Ayyuwb
  14.  Dhul Kifl
  15. Muwsaa
  16. Haaruwn nduguye Muwsaa
  17.  Daawuwd
  18. Sulaymaan bin Daawuwd
  19.  Ilyaas
  20.  Alyasaa'
  21. Yuwnus
  22. Zakariyyaa
  23. Yahyaa bin Zakariyyaa
  24. 'Iysaa bin Maryam
  25. Muhammad

(Swalla Allaahu 'alayhim wa sallam)

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA NABII SULEIMAAN

The Story of the Prophet Idris (AS)

The Story of Prophet Dhul Kifl