ZAKARIA(A.S) NA YAHYA(A.S)

 ZAKARIA(A.S)  NA  YAHYA(A.S)


Nabii Zakaria(a.s) ni miongoni mwa mitume wa Bani Israil (Mayahud) na anatokana na kizazi cha Nabii Sulaiman(a.s). 

Alikuwa mwangalizi mkuu wa nyumba ya Ibada na alikuwa anapta riziki yake kwa kazi ya useremala. Zakaria(a.s)  Kumlea  Maryam  na  Kuomba  Mtoto Mwema Zakaria(a.s) alichaguliwa  na ukoo kumlea Maryamu, mama yake Nabii Issa(a.s).   Alimlea vyema  katika malezi ya kiislamu. Katika kumlea Marymu, Zakaria(a.s) siku moja alishangaa kumkuta Maryam binti Imraan na vyakula mezani ambavyo hakumpa yeye, ikabidi amuulize:

“...Ewe Maryam! unapta wapi hivi ?  Akasema: Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu” (3:37) 

Jibu hili la Maryamu lilimsisimua na kumuhamasisha Mzee Zakaria kiasi cha kumfanya naye amuelekee Mola wake na kumuomba mtoto mwema atakaye mrithi katika ucha-mungu na kusimamisha Dini ya  Allah(s.w) katika jamii.  Zakaria(a.s) alimuelekea Mola wake na kulalama. Akasema: 

Mola wagu. Bila shaka mifupa yangu imekuwa dhaifu na kichwa kinawaka (kinan’gara) kwa mvi,wala sikuwa mweye bahati mbaya (mwenye kukhasirika) Mola wangu, kwa kukuomba wewe. Na hakika mimi nawahofia jamaa zangu baada yangu(kuharibu Dini). Na mke wangu ni tasa. Basi nipe mrithi (anijie) kutoka kwako.  Atakaye nirithi na kuwa na kuwarithi(wazee wake wengine)kizazi cha Ya‘aquub. Na umfanye, Mola wangu mwenye kukuridhisha”(19:4-6)

 Yahya(a.s)  Jibu  la  Dua  ya  Mzee Zakaria(a.s)

Dua ya Zakaria(a.s) ilijibiwa kwa kubashiriwa kupata mtoto, Yahya (Akaambiwa): 

“Ewe Zakaria! Tunakupa habari njema ya (kuwa utazaa)mtoto, jina lake ni Yahya: Hatujafanya kabla yake aliye na jina namna hilo.” (19:7) 

Yahya(a.s)  Kupewa  Utume Alizaliwa mtoto  Yahya na kupewa utume akingali mtoto na akainukia kuwa mtu mwema kwa wazazi wake na kwa walimwengu wote kwa ujumla.  Alijitoa muhanga kwa ajili ya kulingania Dini ya  Allah(s.w). 

Ewe Yahya! kishike kitabu (hiki unachopewa) kwa hima kubwa.” Na tulimpa hikima angali mtoto. Na (tukamfanya ni) huruma kutoka kwetu, na utakaso na akawa mcha-Mungu. Na mwema kwa wazazi wake wala hakuwa jeuri ,asi. Na amani ilikuwa juu yake siku aliyozaliwa na siku aliyokufa na siku atakayofufuliwa hai.(19:12-15) . Nabii Zakaria na  Yahya(a.s) wote waliuliwa na Mayahud.

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Zakaria(a.s) na Yahya(a.s)

Kutokana na Historia ya Nabii Zakaria (a.s) na  Yahya (a.s) tunajifunza yafuatayo: 

  •  Tuwe makini katika kulea watoto wetu hasa mabinti , Binti akileleka vizuri atakuwa ni chimbuko la malezi bora katika jamii. 
  • Tusichoke kumuomba  Allah(s.w) jambo lolote la msingi tunalohitajia kwa ajili ya kusimamisha Uislamu na    kuendeleza wema katika jamii,  Hapana linaloshindikana kwa Allah(s.w). 
  • Waumini wanaharakati wa kusimamisha Uislamu katika jamii, waombe watoto wema watakaorithi harakati za Kiislamu na kuziendeleza kwa ari na hima zaidi. 
  • Ili watoto wetu waweze kuwa wanaharakati wazuri, hatunabudi sisi wenyewe kuwa mfano mwema wa kuigwa kama alivyokuwa mzee Zakaria(a.s) na kisha tuwafunze kwa kina elimu sahini ya Uislamu inayotokana na Qur-an na Sunnah na tuwape kwa upana elimu ya mazingira. 
  • Mtoto anayependeka mbele ya  Allah(s.w) ni yule  anayewafanyia wema wazazi wake kisha kuifanyia wema jamii. Mtu hawezi kuwa mwema kwa jamii yake endapo ameshindwa kuwatendea wema wazazi wake waliomzaa na kumlea kwa taabu. 
  • Kila mtoto anazaliwa katika amani, (katika Uislamu).   Atabakia kuwa katika amani mpaka kufa kwake na kufufuliwa kwake endapo tutamlea Kiislamu naye akaendelea kubakia kuwa Muislamu mtendaji mwenye kufanya jitihada za makusudi za kusimamisha Uislamu katika jamii baada ya baleghe yake mpaka kufa kwake.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA NABII SULEIMAAN

The Story of the Prophet Idris (AS)

The Story of Prophet Dhul Kifl