KINGA YA MUISLAM
بسم الله الرحمن الرحيم
KINGA YA MUISLAM
Ndugu katika imani hii ni bahati iliyoje katika huu ummat Muhammad (s.a.w)? Allah anatupenda sana hakutuacha ovyo! bali ametuelekeza na kutubainishia kupitia kwa Mtume wake Muhammad (s.a.w) kila lenye manufaa na sisi na namna ya kuliendea, na kila lenye shari na sisi ametubainishia jinsi ya kuliepuka!. Chakushangaza kuna baadhi ya watu wameacha kinga sahihi ya Allah (S.w) na kufuata mambo ya kishirikina wanakwenda kwa waganga wa kienyeji basi huko hupewa karatasi zenye maandishi ya rangi nyekundu kisha huzining'iniza katika milango wakiwa na imani kwamba ndio kinga kwao.
Na wengine hupewa mizigo (vitu vya ajabu) wakaambiwa wavichimbie na kuvifukia katika kona za nyumba zao kwa imani kua ni kinga kwa familia nzima, INNAA LILLAHI WA INNAA ILAYHI RAJIUN!!!!! Huu ni msiba wa hali ya juu na ni haram katika sheria ya kiislam. TAMBIIH (UZINDUO) Tunawausia wanaofanya shirki (ushirikina) kuyaacha mambo hayo na kufanya Toba haraka, kwani umauti unakuja ghafla, na mtu akifa hali ya kuwa ni mshirikina Allah (S.w) hamsamehe mtu kama huyo. ALLAH ANASEMA:- ((إن الله لا يغفر أن يشرك به و يغفر ما دون ذلك لمن يشاء و من يشرك بالله فقد افترى إثما عظيما)) سورة النساء: ٤٨ Hakika Allah hamsamehe mwenye kumshirikisha na anasamehe mengine yasikua hayo (ya shirki) kwa yule amtakae na anaemshirikisha Allah basi hakika amezua dhambi kubwa. Surat Nisaa aya ya 48. Tunamuomba Allah atuepushe na shirki na atujaalie mwisho mwema. Ameen!!!!
Comments
Post a Comment