UTANGULIZI

UTANGULIZI

App hii ni muongozo mfupi wa kuufahamu Uislamu. Nayo ina Sura tatu. Sura ya kwanza, ‘‘Baadhi ya vithibitisho juu ya ukweli wa Uislam,’’ Sura hiyo inajibu baadhi ya maswali muhimu ambayo watu wanayauliza:

  • Je ni kweli kwamba Qur’an ni maneno halisi ya Mungu, yaliyofunuliwa toka kwake ?
  • Je ni kweli kuwa Muhammad S.A.W ni Mtume alietumwa na Mungu?
  •  Je ni kweli kuwa Uislamu ni Dini ya Mungu ?

Katika sura hii, zimetajwa aina sita za ushahidi:

  1.  Miujiza ya kisayansi ndani ya Qur’an tukufu: Sehemu hii inazungumzia (kwa picha) baadhi ya hakika (facts) za uvumbuzi wa kisasa wa kisayansi zilizotajwa katika Qur’an tukufu, ambayo ilikwishafunuliwa karne kumi na nne zilizopita.
  2. Changamoto Kuu ya Kuunda Sura Moja kama Sura za Qur’an Tukufu: Katika Qur’an, Mungu amewapa changamoto watu wote watunge sura moja iliyo kama sura za Qur’an. Tangu kufunuliwa kwa Qur’an, karne kumi na nne zilizopita, mpaka leo, hakuna mtu aliyeweza kuifikia changamoto hii, ingawa sura ndogo sana ya Qur’an ni (sura ya 108) yenye jumla ya maneno kumi tu.
  3. Utabiri wa Biblia kuhusu kuja kwa Muhammad S.A.W, Mtume wa Uislamu: Katika sehemu hii, kumejadiliwa baadhi ya utabiri wa Biblia kuhusu kuja kwa Mtume Muhammad S.A.W
  4. Aya za Qur’an ambazo zimeeleza kutokea matukio katika siku za mbele na kisha yakatokea: Qur’an ilielezea kutokea kwa Matukio siku za mbele na ambayo baadae yakatokea, kwa mfano ushindi wa Warumi dhidi ya Wafursi (Wairani).
  5.  Miujiza iliyofanywa na Mtume Mohammad S.A.W Miujiza mingi ilifanywa na Mtume Muhammad S.A.W Miujiza hiyo  ilishuhudiwa na watu wengi.
  6. Maisha ya Hali ya Chini ya Muhammad S.A.W. Hii inaonyesha wazi kuwa Muhammad S.A.W hakuwa mtume wa uongo aliedai utume ili apate kuchuma mali, ukubwa au madaraka.

Kutokana na aina hizi sita za ushahidi, tunahitimisha kuwa:

  •  Qur'an lazima itakuwa ni maneno hilisi ya Mungu, yaliyofunuliwa naye.
  •  Muhammad S.A.W ni Mtume wa kweli alietumwa na Mungu.
  • Uislamu ni Dini ya kweli ya Mungu.

Ikiwa tunataka kufahamu kama dini ni ya kweli au ya uwongo, hututakiwi kutegemea miono yetu, mawazo, au tamaduni. Heri, tutegemee hoja na akili. Mungu alipowatuma mitume, aliwapa nguvu kwa miujiza na ushahidi ambao ulithibitisha kuwa wao ni mitume wa kweli waliotumwa na Mungu na kwa hiyo dini waliokuja nayo ni ya kweli. 

Sura ya pili,‘‘Baadhi ya Faida za Uislamu,’’ inataja baadhi ya faida ambazo zinatolewa na Uislamu kwa kila mtu, kwa mfano:

  1. Mlango wa Kuingia Peponi
  2. Wokovu wa Kuepukana na Moto
  3. Furaha ya Kweli na Amani Moyoni
  4. Msamaha wa Dhambi Zote Zilizotangulia.

Sura ya tatu, ‘‘Maelezo ya Ujumla kuhusu Uislamu,’’ inatoa maelezo ya ujumla kuhusu Uislamu, inasahihisha ufahamu potofu kuhusu Uislamu, na inajibu baadhi ya maswali yanayoulizwa mara mara, kama vile:

  • Uislamu unasemaje kuhusu Ugaidi?
  • Mwanamke ana nafasi gani katika Uislamu?


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA NABII SULEIMAAN

Full story of theProphet Al-Yasa

Umuhimu Wa Dua Katika Uislamu Na Njia Ya Kuomba