BAADHI YA VITHIBITISHO JUU YA UKWELI WA UISLAMU

 BAADHI YA VITHIBITISHO JUU YA UKWELI WA UISLAMU

Mwenyezi Mungu amempa nguvu Mtume wake wa mwisho Muhammad S.A.W kwa Miujiza mingi na Ushahidi mwingi ambao unathibithisha kuwa yeye ni mtume wa kweli alietumwa na Mungu.

Vile vile Mwenyezi Mungu amekipa nguvu Kitabu chake alichokishusha mwisho, ambacho ni Qur’an tukufu, kwa Miujiza mingi ambayo inathibitisha kuwa Qur’an hii ni Maneno halisi ya Mungu, aliyoyafunua, na kwa hiyo Qur’an haijatungwa na mtu yeyote. Sura hii inajadili baaadhi ya ushahidi huo.

(1) Miujiza ya Kisayansi ndani yaQur’an Tukufu 

Qur’an ni maneno halisi ya Mwenyezi Mungu, ambayo aliyashusha kwa Mtume wake Muhammad S.A.W kwa kupitia Malaika Jibril (Gabriel.). Qur’an ambayo ilihifadhiwa na Muhammad S.A.W naye akawasomea Qur’an hiyo wafuasi wake. Nao, kwa zamu, waliihifadhi, kuiandika, na kuipitia
pamoja na Mtume Muhammad S.A.W. 

Zaidi ya hayo Mtume Muhammad S.A.W aliipitia Qur’an pamoja na Malaika Jibril kila mwaka mara moja na katika mwaka wa mwisho wa uhai wake Mtume S.A.W waliipitia mara mbili. 
Tangu wakati iliposhushwa Qur’ani, mpaka leo hii, daima kumekuwepo na idadi kubwa nno ya Waislam ambao wamehifadhi Qur,an yote, neno kwa neno. Baadhi yao wameweza kuhifadhi nzima wakiwa na umri wa miaka kumi.

Hakuna hata herufi moja ya Qur’an iliyobadilishwa ingawa karne nyingi zimepita. Qur’an, iliyoshushwa karne kumi na nne zilizopita, imeelezeamambo ya hakika ambayo yamevumbuliwa au kuthibitishwa na wanasayansi hivi karibuni tu. Hii bila ya shaka inathibitisha kuwa Qur’an ni lazima itakuwa ni maneno halisi ya Mungu, yaliyofunuliwa naye kwenda kwa Mtume Muhammad S.A.W na kwa hiyo Qur’an haikutungwa na Muhammad S.A.W au na mtu yeyote. Hii pia inathibitisha kuwa Muhammad S.A.W ni mtume wa kweli alietumwa na Mungu. Haingii akilini kuwa mtu yeyote wa miaka elfu moja na mia nne iliyopita angelijua hakika hizi zilizogunduliwa au kuthibitishwa hivi karibuni tu kwa kutumia nyenzo na njia za kisayansi za kisasa.
Baadhi ya mifano inafuata. 

A) Qur’an na ukuaji wa mimba:

Katika Qur’an tukufu, Mwenyezi Mungu anaeleza kuhusu hatua za maendeleo ya ukuaji wa mimba ya binadamu:
{Na kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asli ya udongo* Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti* Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na
mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji . Qur’an Sura ya 23 aya 12 hadi 14.}

Asili, ya neno alaqah ni la kiarabu lina maana tatu:

  1. Ruba  
  2. kitu kilichotundikwa na 
  3. Pande la damu ilioganda.
Kwa kulinganisha kati ya Ruba na Kiinitete (mimba changa), katika hatua ya alaqah, tunapata kuwa kuna kufanana kati ya vituviwili hivyo,  kama tunavyoweza kuona katika umbo 1. Pia, kiinitete katika hatua hii kinapata virutubisho kutoka katika damu ya Mama, sawa sawa na ruba, ambaye anakula damu ya viumbe wengine.

Maana ya pili ya neno alaqah ni Kitu kilichotundikwa. Na hivi ndivyo tunavyoweza kuona katika Umbo namba 2 na 3, utundikwaji wa kiinitete (mimba changa), katika hatua ya alaqah kwenye mfuko
wa uzazi wa mama.

Na maana ya tatu ya neno alaqah ni pande la damu iliyoganda. Tunakuta kuwa umbo la upande wa nje wa kiinitete na mifuko yake, katika hatua ya alaqah, linafanana na pande la damu iliyoganda. Hii
ni kwa mujibu wa kuwepo kiasi kikubwa cha damu iliyo katika
kiinitete, katika hatua hii  (tazama umbo 4 ). Vilevile katika hatua hii, damu iliyo katika kiinitete haizunguki mpaka mwishoni mwa wiki ya tatu. Kwa hiyo kiinitete katika hatua hii kinafanana na pandela damu iliyoganda. 

Kwa hiyo maana tatu za neno alaqah zinaafikiana na sifa za kiinitete kikiwa katika hatua ya alaqah.
Hatua inayofuata ambayo imetajwa katika aya hii ni hatua ya Mudghah. Neno la kiarabu Mudghah maana yake ni “kitu kilichotafunwa”. Kama mtu akichukua bazoka na kuitafuna mdomoni mwake kisha ilinganishwe na kiinitete kilicho katika hatua ya Mudghah, tutahitimisha kuwa kiinitete katika hatua ya Mudghah kiumbo, kinafanana na bazoka iliyotafunwa. Hii ni kwa kuwa umbo
la uti wa mgongo wa mtoto akiwa katika hatua ya Mudghah linafanana kwa kiasi fulani na athari za meno katika bazoka iliyotafunwa.  ( tazama umbo 5 na 6)

Vipi Muhammad S.A.W angeweza kupata uwezo wa kufahamu mambo yote haya tangu karne kumi na nne zilizopita, wakati wanasayansi ni hivi karibuni tu ndio wamegundua yote hayo kwa kutumia vyombo vya hali ya juu na darubini zenye nguvu ambazo hazikuwepo wakati ule? Hamm na Leeuwenhoek walikuwa ni wanasayansi wa mwanzo kugundua viini vya mbegu za uzazi za Mwanadamu (Spermatozoa) kwa kutumia darubini zenye kiwango cha hali ya juu mwaka 1677 (zaidi ya miaka 1000 baada ya kufariki Muhammad (S.A.W.). Nao kwa bahati mbaya walidhani kuwa kiini cha mbegu za uzazi za binadamu kina kijimtu kidogo dogo ambacho hukua wakati kinapowekwa katika eneo la mfumo wa uzazi wa
mwanamke.





Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA NABII SULEIMAAN

Full story of theProphet Al-Yasa

Umuhimu Wa Dua Katika Uislamu Na Njia Ya Kuomba