KISA CHA NABII SWALIH
KISA CHA NABII SWALIH
Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) alikuwa ni Rasuli katika kabila maarufu linatokana na jina la Babu yao Thamuwd ambaye ni katika ukoo wa Nabiy Nuwh ('alayhis-salaam). Hivyo jina lake ni Swaalih ibn 'Ubayd ibn Maasiyh ibn 'Ubayd ibn Haajir ibn Thamuwd, ibn 'Aabir ibn Iram, ibn Saam, ibn Nuwh.
Naye Swaalih na watu wake wa Thamuwd ni Waarabu waliokuwa wakiishi Hijr ambayo iko baina ya Hijaaz na Tabuwk (Kaskazini Magharibi ya Madiynah) ambako siku moja Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipita wakati wanaelekea kwenda kwenya vita vya Tabuwk. (maelezo haya yatatajwa mwishoni mwa kisa hiki).
Watu wa Thamuwd walikuwa ni baada ya Nabiy Nuwh ('alayhis-salaam) waliokuwa wakiabudu masanamu na ambao waliangamizwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) baada ya kumkanusha Nabiy Nuwh ('alayhis-salaam) na da’wah yake ya kuwalingania katika Tawhiyd ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Baada ya miaka, watu wa Thamuwd wakaibuka na kuwa na nguvu na ufakhari. Nao pia walimshirikisha Allaah ('Azza wa Jalla) kwa kuabudu masanamu. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akawatumia Rasuli miongoni mwao ambaye ni Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam). Na kawaida ya risala ya Rasuli ni kuwalingania washirikiana katika Tawhiyd; kumpwekesha Allaah ('Azza wa Jalla) kwa kumuabudu Yeye Pekee bila ya kumshirikisha na yeyote au chochote. Juu ya hivyo, kuwanasihi waombe maghfirah na watubie kwa Allaah ('Azza wa Jalla). Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuhusu hayo kama ifuatavyo:
وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ هُوَ أَنشَأَكُم مِّنَ الْأَرْضِ وَاسْتَعْمَرَكُمْ فِيهَا فَاسْتَغْفِرُوهُ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ ۚ إِنَّ رَبِّي قَرِيبٌ مُّجِيبٌ﴿٦١﴾
61. Na kwa Thamuwd (Tulimpeleka) ndugu yao Swaalih. Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Yeye Ndiye Aliyekuanzisheni katika ardhi, na Akakufanyieni makazi humo; basi mwombeni maghfirah, kisha tubieni Kwake. Hakika Rabb wangu Yuko Karibu, Mwenye kuitikia. [Huwd: 61]
Kwa maana: Amekujaalieni kuwa makhalifa baada ya watu wengine (kina 'Aad na wa nyuma yao) ili mfikiri na mtambue uovu wao waliotenda, na nyinyi msiwe kama wao, na Akakujaalieni katika hii ardhi na kukuneemesheni neema mbali mbali kama za mashamba na matunda na majumba ya fakhari mkastarehe, basi Yeye Allaah ('Azza wa Jalla) Ndiye Pekee Anayestahiki kuabudiwa bila ya kumshirikisha. Vile vile mkabilini Rabb wenu kwa kumshukuru na kufanya amali njema wala msjije kumkhalifu amri Zake mkaja kutoka nje ya mipaka kwa kutokumtii, basi rudini kwake kwa kutubia na Yeye Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Yuko tayari kupokea tawbah zenu. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ قَدْ جَاءَتْكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ ۖ هَـٰذِهِ نَاقَةُ اللَّـهِ لَكُمْ آيَةً ۖ فَذَرُوهَا تَأْكُلْ فِي أَرْضِ اللَّـهِ ۖ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٣﴾
73. Na kwa Thamuwd (Tuliwapelekea) kaka yao Swaalih. Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Kwa yakini imekujieni hoja bayana kutoka kwa Rabb wenu. Huyu ngamia jike wa Allaah ni Aayah (ishara, dalili) kwenu. Basi muacheni ale katika ardhi ya Allaah, na wala msimguse kwa uovu isije ikakuchukueni adhabu iumizayo.
وَاذْكُرُوا إِذْ جَعَلَكُمْ خُلَفَاءَ مِن بَعْدِ عَادٍ وَبَوَّأَكُمْ فِي الْأَرْضِ تَتَّخِذُونَ مِن سُهُولِهَا قُصُورًا وَتَنْحِتُونَ الْجِبَالَ بُيُوتًا ۖ فَاذْكُرُوا آلَاءَ اللَّـهِ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ ﴿٧٤﴾
74. Na kumbukeni Alipokujaalieni warithi baada ya ‘Aad, Akakufanyieni makazi katika ardhi mnachukua katika nyanda zake tambarare majumba ya fakhari na mnachonga majumba kutokana na majabali. Basi kumbukeni neema nyingi za Allaah na wala msifanye vitendo vya hujuma katika ardhi mkifisidi. [Al-A’raaf: 73 - 74]
Lakini kama ilivyokuwa kawaida za umati za kale, kila walipotumiwa Rasuli kutoka kwa Rabb wao, wengi wao wao walikmanusha Rasuli na risala yake. Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ فَإِذَا هُمْ فَرِيقَانِ يَخْتَصِمُونَ ﴿٤٥﴾
45. Na kwa yakini Tuliwapelekea kina Thamuwd ndugu yao Swaalih kwamba: Mwabuduni Allaah. Tahamaki wakawa makundi mawili yanayokhasimiana. [An-Naml: 45]
Waliomkanusha walimtuhumu kuwa anawaletea shari, na kwamba labda akili yake haiko sawa kwani hawakumtegemea mtu kama wao ambaye ni Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) na ambaye alikuwa kwao ni mtu mwema kabisa, aje kuwakataza kuacha waliyokuja nayo mababu zao na kutaka wamfuate hayo anayotaka yeye. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
قَالُوا يَا صَالِحُ قَدْ كُنتَ فِينَا مَرْجُوًّا قَبْلَ هَـٰذَا ۖ أَتَنْهَانَا أَن نَّعْبُدَ مَا يَعْبُدُ آبَاؤُنَا وَإِنَّنَا لَفِي شَكٍّ مِّمَّا تَدْعُونَا إِلَيْهِ مُرِيبٍ﴿٦٢﴾
62. Wakasema: Ee Swaalih! Kwa yakini ulikuwa kwetu mwenye kutarajiwa (khayr) kabla ya haya. Je, unatukataza kuabudu wale wanaowaabudu baba zetu; na hakika sisi tumo katika shaka na wasiwasi katika unayotuitia. [Huwd: 62]
Walikuwa na shaka kubwa juu ya risala aliyowalingania nayo Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) na kuona kuwa jambo geni mno. Lakini Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) akawajibu na akawanaisihi na kuwapa dalili ya muujiza waliomtaka Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) awaletee mbele ya macho yao; nao ni ngamia jike mwenye mimba na ambaye Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Aliwatimizia ombi lao hilo:
قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَآتَانِي مِنْهُ رَحْمَةً فَمَن يَنصُرُنِي مِنَ اللَّـهِ إِنْ عَصَيْتُهُ ۖ فَمَا تَزِيدُونَنِي غَيْرَ تَخْسِيرٍ﴿٦٣﴾
63. (Swaalih) Akasema: Enyi kaumu yangu! Je, mnaonaje ikiwa niko katika hoja bayana kutoka kwa Rabb wangu, na Amenipa rahmah (Unabiy na risala) kutoka Kwake basi nani atakayeninusuru nikimuasi? Basi hamnizidishii ila khasara.
وَيَا قَوْمِ هَـٰذِهِ نَاقَةُ اللَّـهِ لَكُمْ آيَةً فَذَرُوهَا تَأْكُلْ فِي أَرْضِ اللَّـهِ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابٌ قَرِيبٌ﴿٦٤﴾
64. Enyi kaumu yangu! Huyu ni ngamia jike wa Allaah, ni Aayah (miujiza, ishara) kwenu, basi mwacheni ale katika ardhi ya Allaah, na wala msimguse kwa uovu ikakupateni adhabu iliyo karibu.
Lakini hawakuwa wenye kutakwa kuongoka. Bali walizidi kumtuhumu Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) wakimwambia kuwa amerogwa!
قَالُوا إِنَّمَا أَنتَ مِنَ الْمُسَحَّرِينَ ﴿١٥٣﴾
153. Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa waliorogwa. [Ashu’araa: 153]
Mujaahid kasema; Wamemaanisha kuwa kaathirika na uchawi.
Baadhi ya wafasiri wa Qur-aan wamesema wamekusudia kuwa Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) hakuwa anajua anachokisema kuwalingania katika ‘ibaada ya Mwabudiwa Mmoja (Laa ilaaha illa-Allaah) na badala yake kuacha waabudiwa wao waliokuwa wakiabudiwa na mababu zao.
Ilikuwa ni kawaida ya watu wa umati za nyuma kuwatilia shaka na kuwatuhumu Manabii kuwa ni wachawi au wamerogwa au waongo,. Hata Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alituhumiwa na makafiri wa ki-Quraysh. Na pia waliwatilia shaka kwa kuwa wao ni wana Aadam kama wao; walitegemea watumiwe Malaika badala yake. Basi Kauli ya Thamuwd nao wakamwambia Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam):
مَا أَنتَ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا فَأْتِ بِآيَةٍ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿١٥٤﴾
154. Wewe si chochote isipokuwa mtu kama sisi; basi lete Aayah (dalili, muujiza) ukiwa wewe ni miongoni mwa wakweli. [Ash-Shu’araa: 154]
Na pia Kauli za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِالنُّذُرِ ﴿٢٣﴾
23. Kina Thamuwd waliwakadhibisha Waonyaji.
فَقَالُوا أَبَشَرًا مِّنَّا وَاحِدًا نَّتَّبِعُهُ إِنَّا إِذًا لَّفِي ضَلَالٍ وَسُعُرٍ ﴿٢٤﴾
24. Wakasema: Ah! Tumfuate binaadamu miongoni mwetu? Hakika hapo sisi tutakuwa katika upotofu na wazimu.
أَأُلْقِيَ الذِّكْرُ عَلَيْهِ مِن بَيْنِنَا بَلْ هُوَ كَذَّابٌ أَشِرٌ ﴿٢٥﴾
25. Ah! Ameteremshiwa ukumbusho baina yetu? Bali yeye ni muongo mkubwa mfidhuli mwenye kutakabari mno.
سَيَعْلَمُونَ غَدًا مَّنِ الْكَذَّابُ الْأَشِرُ ﴿٢٦﴾
26. Watakuja kujua kesho nani muongo mkubwa mfidhuli mwenye kutakabari mno. [Al-Qamar: 23- 26]
Wakadai muujiza uwatokezee mbele ya macho yao, na hata walipotimiziwa ombi lao hawakumwamini Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam). Basi Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) akajitenga nao kwa kuwa alikata tamaa nao kuwa wataitikia risala ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
فَتَوَلَّىٰ عَنْهُمْ وَقَالَ يَا قَوْمِ لَقَدْ أَبْلَغْتُكُمْ رِسَالَةَ رَبِّي وَنَصَحْتُ لَكُمْ وَلَـٰكِن لَّا تُحِبُّونَ النَّاصِحِينَ ﴿٧٩﴾
79. (Swaalih) akajitenga nao na akasema: Enyi kaumu yangu! Kwa yakini nilishakubalighishieni risala ya Rabb wangu na nilikunasihini, lakini nyinyi hamuwapendi wenye kunasihi. [Al-A’raaf: 79]
Muujiza Wa Ngamia:
Wafasiri wa Qur-aan wamesema kwamba siku moja watu wa Thamuwd walikusanyika katika baraza lao akaja Nabiy Swaalih (‘alayhis-salaam) kuwalingania katika Tawhiyd ya Allaah (Kumpwekesha Allaah), na akawapa mawaidha na kuwaonya. Wakadai dalili kuhusu ujumbe wake aliokuja nao kama kweli umetoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).
Wakamwambia: “Ewe Swaalih! Tutolee katika jabali lile (wakaashiria jabali lililokuwepo) ngamia wa kike, ambaye ana mimba ya miezi kumi.” (Na wakataja sifa nyingine kadha)
Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) akawauliza: "Je, mkiletewa hiyo miujiza mliyoomba na mliyotaka iwe vile vile, mtaniamini na kuamini ujumbe niliotumwa nao kwenu?" Wakajibu: "Ndio tutakuamini na kukusadiki yote utakayotuambia." Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) akachukua ahadi hiyo kwa watu wake kisha akamuelekea Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kumuomba awaletee miujiza hiyo waliyotaka. Kama tunavyojua na kuamini kuwa hakuna jambo lolote linalomshinda Allaah ('Azza wa Jalla) kulifanya kama Anavyosema Mwenyewe:
إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَن يَقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٨٢﴾
Hakika amri Yake Anapotaka chochote hukiambia: Kun! (Kuwa), nacho huwa. [Yaasiyn: 82]
Basi watu wa Nabiy Swaalihi ('alayhis-salaam) wakakusanyika mbele ya jabali hilo na kusubiri waone kama ombi lao litatimizwa. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Aliamrisha jabali lipasuke na akatoka ngamia mwenye sifa zile zile walizozitaka; ngamia mwanamke, mwenye mimba ya miezi kumi, mweupe. Akatokeza huyo ngamia kutoka kwenye hilo jabali akipita mbele yao wakimtazama.
Ulikuwa ni muujiza mkubwa wa kustaajabisha ambao ni dalili za dhahiri ya uwezo wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Lakini juu ya hivyo wengi katika watu hao wa Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) hawakuamini!
Hali ya watu wa Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) imetajwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika Aayah zifuatazo:
قَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا مِن قَوْمِهِ لِلَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا لِمَنْ آمَنَ مِنْهُمْ أَتَعْلَمُونَ أَنَّ صَالِحًا مُّرْسَلٌ مِّن رَّبِّهِ ۚ قَالُوا إِنَّا بِمَا أُرْسِلَ بِهِ مُؤْمِنُونَ ﴿٧٥﴾
Wakasema wakuu waliotakabari katika kaumu yake kuwaambia wale waliokandamizwa ambao walioamini miongoni mwao: Je, mnajua kwamba Swaalih ametumwa kutoka kwa Rabb wake? Wakasema: Hakika sisi kwa yale aliyotumwa nayo ni wenye kuyaamini.
قَالَ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا إِنَّا بِالَّذِي آمَنتُم بِهِ كَافِرُونَ ﴿٧٦﴾
Wakasema wale waliotakabari: Hakika sisi kwa yale mliyoyaamini tunayakanusha. [Al-A’raaf: 75-76]
Ngamia huyo wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) aliletwa na shuruti zake walizoombwa watu wa Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) wazitimize nazo ni: wamwache huru wala wasimdhuru, wala wasimuuwe kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ قَدْ جَاءَتْكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ ۖ هَـٰذِهِ نَاقَةُ اللَّـهِ لَكُمْ آيَةً ۖ فَذَرُوهَا تَأْكُلْ فِي أَرْضِ اللَّـهِ ۖ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٣﴾
Na kwa Thamuwd (Tuliwapelekea) kaka yao Swaalih. Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Kwa yakini imekujieni hoja bayana kutoka kwa Rabb wenu. Huyu ngamia jike wa Allaah ni Aayah (ishara, dalili) kwenu. Basi muacheni ale katika ardhi ya Allaah, na wala msimguse kwa uovu isije ikakuchukueni adhabu iumizayo. [Al-A’raaf: 73]
Na wakapewa mtihani mwengine ambao ulikuwa ni sharti la kufanya zamu ya kunywa maji baina yao na baina ya ngamia huyo. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
إِنَّا مُرْسِلُو النَّاقَةِ فِتْنَةً لَّهُمْ فَارْتَقِبْهُمْ وَاصْطَبِرْ ﴿٢٧﴾
Hakika Sisi Tutawapelekea ngamia jike awe jaribio kwao, basi (ee Nabiy Swaalih عليه السلام) watazame na vuta subira.
وَنَبِّئْهُمْ أَنَّ الْمَاءَ قِسْمَةٌ بَيْنَهُمْ ۖ كُلُّ شِرْبٍ مُّحْتَضَرٌ ﴿٢٨﴾
Na wajulishe kwamba maji ni mgawanyo baina yao (ngamia na wao), kila sehemu ya maji itahudhuriwa (kwa zamu). [Al-Qamar: 27]
Alikuwa ni ngamia mwenye baraka nyingi, maziwa yake yaliyokamuliwa siku moja yaliwatosheleza watu wa mji mzima! Alikuwa akilala mahali ambapo wanyama wengine walikuwa hawapakaribii pahali hapo. Kwa hiyo walijua kuwa huyo hakuwa ngamia wa kawaida, bali alikuwa ni ishara kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Wakatakiwa wamwache atembee anapotaka katika mji huo, ale anavyotaka, na zamu ya kunywa maji iwe siku moja anywe ngamia na siku ya pili wanywe wao. Na siku ya zamu ya watu wa Thamuwd, walijichotea maji ya kutosha na kuyaweka ili kuyatumia kwa haja zao ya siku ya pili. Na ile siku ya zamu ya ngamia, watu wa Thamwud walikuwa wakinywa maziwa yake huyo ngamia. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
قَالَ هَـٰذِهِ نَاقَةٌ لَّهَا شِرْبٌ وَلَكُمْ شِرْبُ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ ﴿١٥٥﴾
Akasema: Huyu hapa ngamia jike ana zamu ya kinywaji, nanyi mna zamu ya kinywaji siku maalumu. [Ash- Shu’araa: 155] Tena wakaonywa kuwa wasimdhuru wasije kupata adhabu.
وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابُ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿١٥٦﴾
Na wala msimguse kwa uovu, ikaja kukuchukueni adhabu ya Siku adhimu. [Ash-Shua’raa: 156]
Na pia katika Suwrah nyengine.
وَيَا قَوْمِ هَـٰذِهِ نَاقَةُ اللَّـهِ لَكُمْ آيَةً فَذَرُوهَا تَأْكُلْ فِي أَرْضِ اللَّـهِ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابٌ قَرِيبٌ﴿٦٤﴾
Enyi kaumu yangu! Huyu ni ngamia jike wa Allaah, ni Aayah (miujiza, ishara) kwenu, basi mwacheni ale katika ardhi ya Allaah, na wala msimguse kwa uovu ikakupateni adhabu iliyo karibu. [Huwd: 64] Lakini hawakutaka kutii amri ya mwanzo ya kuacha kuabudu masanamu wala hawakutaka kutii amri ya kumtunza huyo ngamia, bali walimuua na wakakusudia kumua pia Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam). Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَمَا مَنَعَنَا أَن نُّرْسِلَ بِالْآيَاتِ إِلَّا أَن كَذَّبَ بِهَا الْأَوَّلُونَ ۚ وَآتَيْنَا ثَمُودَ النَّاقَةَ مُبْصِرَةً فَظَلَمُوا بِهَا ۚ وَمَا نُرْسِلُ بِالْآيَاتِ إِلَّا تَخْوِيفًا ﴿٥٩﴾
Na hakuna kinachotuzuia kuleta Aayaat (muujiza) isipokuwa ni kuwa watu wa awali waliikadhibisha. Na Tuliwapa kina Thamuwd ngamia jike kuwa dalili dhahiri lakini wakamdhulumu. Na Hatupeleki Aayaat (miujiza, maonyo) isipokuwa kwa ajili ya kukhofisha. [Al-Israa: 59]
Kwa maana: walikanusha na wakamdhuru.
Basi haukupita muda, na hawakuweza kustahmili hali hiyo ya ngamia na masharti waliyopewa. Na chuki zao juu ya Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) wakazigeuza kumchukia ngamia. Wakuu katika watu wa Thamwud wakakutana kupanga njama ya kumuua ngamia ili wapate uhuru wa maji yao. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
فَعَقَرُوا النَّاقَةَ وَعَتَوْا عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ وَقَالُوا يَا صَالِحُ ائْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِن كُنتَ مِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٧٧﴾
Wakamuua yule ngamia jike na wakaasi amri ya Rabb wao; na wakasema: Ee Swaalih, tuletee hayo unayotutishia ukiwa ni miongoni mwa Rusuli. [Al-A’raaf: 77]
Kisha wakamhimiza Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) awaletee adhabu aliyowaonya nayo. Maasi yao yakwa ni kuhalifu amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake kwa kumuua ngamia huyo. Na pia kufanya istihizai na kuhimiza adhabu ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) iwateremkie.
Njama Za Kumuua Ngamia:
Walipopanga njama za kumuua ngami wa Allaah, walitafuta usaidizi kutoka kwa mwanamke Swaduwq bin Mahya aliyekuwa tajiri na ambaye alitokana na kabila la heshima kabisa. Akajitolea kujiuza kwa kijana aliyeitwa Masra'i ibn Mahraj kwa sharti amkate miguu ngamia. Mwanamke mwengine mtu mzima aliyeitwa ‘Aniza, alijitolea kumuuza mtoto wake wa kike kwa kijana aliyeitwa Qudaar ibn Saluf kwa sharti amuue ngamia. Vijana hao wawili walipata tamaa kwa hayo waliyoahidiwa wakatoka kutafuta watu wengine saba kuwasaidia kufanya kazi hiyo. Vijana hao wawili wakaungana na wengine saba wakawa jumla ni watu tisa.
Wakawa wanamfuatilia ngamia na kumvizia, wakitazama nyendo zake zote. Alipokuja ngamia kunywa maji katika kisima, Masra'i akamdunga katika mguu wake kwa mshale. Ngamia aljaribu kukimbia lakini alishindwa kwani mshale ulishamwingia katika mguu na kumjeruhi. Qudaar akamfuata ngamia na kumdunga mshale katika mguu mwengine. Ngamia akaanguka chini, na kisha akamchoma na upanga.
Kauli za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَكَانَ فِي الْمَدِينَةِ تِسْعَةُ رَهْطٍ يُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ وَلَا يُصْلِحُونَ ﴿٤٨﴾
Na kulikuweko katika mji ule watu tisa wakifanya ufisadi katika ardhi na wala hawatengenei.
قَالُوا تَقَاسَمُوا بِاللَّـهِ لَنُبَيِّتَنَّهُ وَأَهْلَهُ ثُمَّ لَنَقُولَنَّ لِوَلِيِّهِ مَا شَهِدْنَا مَهْلِكَ أَهْلِهِ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ ﴿٤٩﴾
Wakasema: Apishaneni kwa Jina la Allaah kwamba tutamhujumu (Swaalih) kwa siri usiku na ahli yake, kisha tutasema kwa jamaa yake wa karibu: Hatukushuhudia maangamizi ya ahli yake; nasi hakika ni wa kweli.
وَمَكَرُوا مَكْرًا وَمَكَرْنَا مَكْرًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٥٠﴾
Wakapanga njama Nasi Tukapanga mipango ya kuvurumisha njama nao huku hawatambui. [An-Naml: 48-50} Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
فَنَادَوْا صَاحِبَهُمْ فَتَعَاطَىٰ فَعَقَرَ ﴿٢٩﴾
Wakamwita swahibu wao, akakamata (upanga) akaua (ngamia). [Al-Qamar: 29] Na Hadiyth ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu mtu muovu kabisa:
عن عمار بن ياسر، قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم لعلي: "ألا أحدثك بأشقى الناس"؟ قال: بلى، قال: "رجلان: أحدهما أحيمر ثمود الذي عقر الناقة، والذي يضربك يا علي على هذا ـ يعني قرنه ـ حتى تبتل منه هذه ـ يعني لحيته رواه ابن أبي حاتم
Kutoka kwa 'Ammaar bin Yaasir ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema (kumwambia 'Aliy) ((Je, nikujulishe ni yupi mtu muovu kabisa?)) Akasema ndio: Akasema: ((Watu wawili; mmoja ni mpiga chuku wa Thamuwd aliyemuua ngamia na mwengine ni yule atakayekupiga ee 'Aliy hapa juu (yaani kichwani kwake) mpaka hizi (ndevu) zirowe damu)) [Imesimuliwa na ibn Haatim]
Maelezo zaidi yamo katika Kauli za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwenye Suwrah mbali mbali kuhusu kisa cha Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam):
كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِطَغْوَاهَا ﴿١١﴾
Kina Thamuwd walikadhibisha (Rasuli wao) kwa upindukaji mipaka ya kuasi kwao.
إِذِ انبَعَثَ أَشْقَاهَا ﴿١٢﴾
Pale alipochomoka haraka muovu wao mkuu.
فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللَّـهِ نَاقَةَ اللَّـهِ وَسُقْيَاهَا ﴿١٣﴾
Rasuli wa Allaah (Swaalih عليه السلام) aliwaambia: (Msimdhuru) Ngamia jike wa Allaah, na kinywaji chake.
فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمْدَمَ عَلَيْهِمْ رَبُّهُم بِذَنبِهِمْ فَسَوَّاهَا ﴿١٤﴾
Lakini walimkadhibisha na wakamuua; basi Rabb wao Akawaangamiza kwa sababu ya dhambi zao, na Akayafanya mateketezi yao sawasawa kwa wote.
وَلَا يَخَافُ عُقْبَاهَا ﴿١٥﴾
Na wala (Allaah) Hakhofu hatima yake. [Ash-Shams: 11-15]
Na pia:
وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ قَدْ جَاءَتْكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ ۖ هَـٰذِهِ نَاقَةُ اللَّـهِ لَكُمْ آيَةً ۖ فَذَرُوهَا تَأْكُلْ فِي أَرْضِ اللَّـهِ ۖ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٣﴾
Na kwa Thamuwd (Tuliwapelekea) kaka yao Swaalih. Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Kwa yakini imekujieni hoja bayana kutoka kwa Rabb wenu. Huyu ngamia jike wa Allaah ni Aayah (ishara, dalili) kwenu. Basi muacheni ale katika ardhi ya Allaah, na wala msimguse kwa uovu isije ikakuchukueni adhabu iumizayo.
وَاذْكُرُوا إِذْ جَعَلَكُمْ خُلَفَاءَ مِن بَعْدِ عَادٍ وَبَوَّأَكُمْ فِي الْأَرْضِ تَتَّخِذُونَ مِن سُهُولِهَا قُصُورًا وَتَنْحِتُونَ الْجِبَالَ بُيُوتًا ۖ فَاذْكُرُوا آلَاءَ اللَّـهِ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ ﴿٧٤﴾
Na kumbukeni Alipokujaalieni warithi baada ya ‘Aad, Akakufanyieni makazi katika ardhi mnachukua katika nyanda zake tambarare majumba ya fakhari na mnachonga majumba kutokana na majabali. Basi kumbukeni neema nyingi za Allaah na wala msifanye vitendo vya hujuma katika ardhi mkifisidi.
قَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا مِن قَوْمِهِ لِلَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا لِمَنْ آمَنَ مِنْهُمْ أَتَعْلَمُونَ أَنَّ صَالِحًا مُّرْسَلٌ مِّن رَّبِّهِ ۚ قَالُوا إِنَّا بِمَا أُرْسِلَ بِهِ مُؤْمِنُونَ ﴿٧٥﴾
Wakasema wakuu waliotakabari katika kaumu yake kuwaambia wale waliokandamizwa ambao walioamini miongoni mwao: Je, mnajua kwamba Swaalih ametumwa kutoka kwa Rabb wake? Wakasema: Hakika sisi kwa yale aliyotumwa nayo ni wenye kuyaamini.
قَالَ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا إِنَّا بِالَّذِي آمَنتُم بِهِ كَافِرُونَ ﴿٧٦﴾
Wakasema wale waliotakabari: Hakika sisi kwa yale mliyoyaamini tunayakanusha.
فَعَقَرُوا النَّاقَةَ وَعَتَوْا عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ وَقَالُوا يَا صَالِحُ ائْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِن كُنتَ مِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٧٧﴾
Wakamuua yule ngamia jike na wakaasi amri ya Rabb wao; na wakasema: Ee Swaalih, tuletee hayo unayotutishia ukiwa ni miongoni mwa Rusuli
فَأَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دَارِهِمْ جَاثِمِينَ ﴿٧٨﴾
Basi ikawachukua tetemeko la ardhi wakawa majumbani mwao wenye kuanguka kifudifudi (wamekufa).
فَتَوَلَّىٰ عَنْهُمْ وَقَالَ يَا قَوْمِ لَقَدْ أَبْلَغْتُكُمْ رِسَالَةَ رَبِّي وَنَصَحْتُ لَكُمْ وَلَـٰكِن لَّا تُحِبُّونَ النَّاصِحِينَ ﴿٧٩﴾
(Swaalih) akajitenga nao na akasema: Enyi kaumu yangu! Kwa yakini nilishakubalighishieni risala ya Rabb wangu na nilikunasihini, lakini nyinyi hamuwapendi wenye kunasihi. [Al-A’raaf: 73-79] Wauaji hao wakapongezwa kwa uhodari wao wa kumuua ngamia, wakashangiliwa kwa nyimbo na mashairi ya kuwasifu uhodari wao, na wakamkejeli Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) lakini akawatahadharisha adhabu ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na hali ikawa kama ifuatavyo:
فَعَقَرُوهَا فَقَالَ تَمَتَّعُوا فِي دَارِكُمْ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ ۖ ذَٰلِكَ وَعْدٌ غَيْرُ مَكْذُوبٍ﴿٦٥﴾
Basi wakamuua; (Swaalih) akasema: Stareheni majumbani mwenu siku tatu. Hiyo ni ahadi isiyo ya uongo.
فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا صَالِحًا وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَمِنْ خِزْيِ يَوْمِئِذٍ ۗ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ الْقَوِيُّ الْعَزِيزُ﴿٦٦﴾
Basi ilipokuja amri Yetu, Tulimuokoa Swaalih na wale walioamini pamoja naye kwa rahmah kutoka Kwetu, na kutokana na hizaya ya Siku hiyo. Hakika Rabb wako Yeye Ndiye Mwenye nguvu, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika.
وَأَخَذَ الَّذِينَ ظَلَمُوا الصَّيْحَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دِيَارِهِمْ جَاثِمِينَ﴿٦٧﴾
Na wale waliodhulumu uliwachukuwa ukelele angamizi, wakapambazukiwa wameanguka kifudifudi majumbani mwao (wamekufa).
كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا فِيهَا ۗ أَلَا إِنَّ ثَمُودَ كَفَرُوا رَبَّهُمْ ۗ أَلَا بُعْدًا لِّثَمُودَ﴿٦٨﴾
Kama kwamba hawakuishi wakineemeka humo. Tanabahi! Hakika kina Thamuwd walimkufuru Rabb wao. Tanabahi! Wameangamiziliwa mbali kina Thamuwd. [Huwd: 65-68]
Maelezo zaidi ya kisa hiki katika kauli za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) zifuatazo:
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ فَإِذَا هُمْ فَرِيقَانِ يَخْتَصِمُونَ ﴿٤٥﴾
Na kwa yakini Tuliwapelekea kina Thamuwd ndugu yao Swaalih kwamba: Mwabuduni Allaah. Tahamaki wakawa makundi mawili yanayokhasimiana.
قَالَ يَا قَوْمِ لِمَ تَسْتَعْجِلُونَ بِالسَّيِّئَةِ قَبْلَ الْحَسَنَةِ ۖ لَوْلَا تَسْتَغْفِرُونَ اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٤٦﴾
(Swaalih) Akasema: Enyi kaumu yangu! Kwa nini mnahimiza uovu kabla ya mema; kwa nini msimwombe Allaah maghfirah ili huenda mkarehemewa?
قَالُوا اطَّيَّرْنَا بِكَ وَبِمَن مَّعَكَ ۚ قَالَ طَائِرُكُمْ عِندَ اللَّـهِ ۖ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ تُفْتَنُونَ ﴿٤٧﴾
Wakasema: Tumepata nuksi kwa sababu yako na kwa wale walio pamoja nawe. (Swaalih) Akasema: Nuksi yenu iko kwa Allaah. Bali nyinyi ni watu mliojaribiwa.
وَكَانَ فِي الْمَدِينَةِ تِسْعَةُ رَهْطٍ يُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ وَلَا يُصْلِحُونَ ﴿٤٨﴾
Na kulikuweko katika mji ule watu tisa wakifanya ufisadi katika ardhi na wala hawatengenei.
قَالُوا تَقَاسَمُوا بِاللَّـهِ لَنُبَيِّتَنَّهُ وَأَهْلَهُ ثُمَّ لَنَقُولَنَّ لِوَلِيِّهِ مَا شَهِدْنَا مَهْلِكَ أَهْلِهِ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ ﴿٤٩﴾
Wakasema: Apishaneni kwa Jina la Allaah kwamba tutamhujumu (Swaalih) kwa siri usiku na ahli yake, kisha tutasema kwa jamaa yake wa karibu: Hatukushuhudia maangamizi ya ahli yake; nasi hakika ni wa kweli.
وَمَكَرُوا مَكْرًا وَمَكَرْنَا مَكْرًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٥٠﴾
Wakapanga njama Nasi Tukapanga mipango ya kuvurumisha njama nao huku hawatambui.
فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ مَكْرِهِمْ أَنَّا دَمَّرْنَاهُمْ وَقَوْمَهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٥١﴾
Basi tazama vipi ilikuwa hatima ya njama zao, kwamba Tuliwadamirisha na watu wao wote.
فَتِلْكَ بُيُوتُهُمْ خَاوِيَةً بِمَا ظَلَمُوا ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٥٢﴾
Basi hizo ni nyumba ni magofu kwa sababu ya yale waliyodhulumu. Hakika katika hayo kuna Aayah (ishara, zingatio, funzo n.k.) kwa watu wanaojua. [an-Naml: 45-52]
Njama Za Kumuua Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam):
Baada ya kumuua ngamia, na kuendelea kumkanusha Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) na kukanusha risala aliyotumwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), wakapanga njama kumuua Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam). Njama zao zimetajwa katika Aayah zifuatazo:
Maelezo zaidi ya kisa hiki katika kauli za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) zifuatazo:
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ فَإِذَا هُمْ فَرِيقَانِ يَخْتَصِمُونَ ﴿٤٥﴾
Na kwa yakini Tuliwapelekea kina Thamuwd ndugu yao Swaalih kwamba: Mwabuduni Allaah. Tahamaki wakawa makundi mawili yanayokhasimiana.
قَالَ يَا قَوْمِ لِمَ تَسْتَعْجِلُونَ بِالسَّيِّئَةِ قَبْلَ الْحَسَنَةِ ۖ لَوْلَا تَسْتَغْفِرُونَ اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٤٦﴾
(Swaalih) Akasema: Enyi kaumu yangu! Kwa nini mnahimiza uovu kabla ya mema; kwa nini msimwombe Allaah maghfirah ili huenda mkarehemewa?
قَالُوا اطَّيَّرْنَا بِكَ وَبِمَن مَّعَكَ ۚ قَالَ طَائِرُكُمْ عِندَ اللَّـهِ ۖ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ تُفْتَنُونَ ﴿٤٧﴾
Wakasema: Tumepata nuksi kwa sababu yako na kwa wale walio pamoja nawe. (Swaalih) Akasema: Nuksi yenu iko kwa Allaah. Bali nyinyi ni watu mliojaribiwa.
وَكَانَ فِي الْمَدِينَةِ تِسْعَةُ رَهْطٍ يُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ وَلَا يُصْلِحُونَ ﴿٤٨﴾
Na kulikuweko katika mji ule watu tisa wakifanya ufisadi katika ardhi na wala hawatengenei.
قَالُوا تَقَاسَمُوا بِاللَّـهِ لَنُبَيِّتَنَّهُ وَأَهْلَهُ ثُمَّ لَنَقُولَنَّ لِوَلِيِّهِ مَا شَهِدْنَا مَهْلِكَ أَهْلِهِ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ ﴿٤٩﴾
Wakasema: Apishaneni kwa Jina la Allaah kwamba tutamhujumu (Swaalih) kwa siri usiku na ahli yake, kisha tutasema kwa jamaa yake wa karibu: Hatukushuhudia maangamizi ya ahli yake; nasi hakika ni wa kweli.
وَمَكَرُوا مَكْرًا وَمَكَرْنَا مَكْرًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٥٠﴾
Wakapanga njama Nasi Tukapanga mipango ya kuvurumisha njama nao huku hawatambui.
فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ مَكْرِهِمْ أَنَّا دَمَّرْنَاهُمْ وَقَوْمَهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٥١﴾
Basi tazama vipi ilikuwa hatima ya njama zao, kwamba Tuliwadamirisha na watu wao wote.
فَتِلْكَ بُيُوتُهُمْ خَاوِيَةً بِمَا ظَلَمُوا ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٥٢﴾
Basi hizo ni nyumba ni magofu kwa sababu ya yale waliyodhulumu. Hakika katika hayo kuna Aayah (ishara, zingatio, funzo n.k.) kwa watu wanaojua. [an-Naml: 45-52
Kuhusu Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَكَانَ فِي الْمَدِينَةِ تِسْعَةُ رَهْطٍ يُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ وَلَا يُصْلِحُونَ ﴿٤٨﴾
Na kulikuweko katika mji ule watu tisa wakifanya ufisadi katika ardhi na wala hawatengenei. Ina maana walikuwa wakilazimishia watu wa Thamuwd wakubaliane na rai zao pamoja na njama zao kwa sababu wao walikuwa ni viongozi na vigogo wao.
Al-Awfi kasema kwamba Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: “Hawa ni watu waliomuuwa ngamia." [At-Twabariy 19:477] Wakapanga njama kumuua Nabiy Swaalih (‘alayhis-salaam) pindi atakapolala usiku akiwa pamoja na aila yake, wamuue kisha wawaambie jamaa zake Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) kuwa wao hawajui lolote kuhusu yaliyotokea usiku huo na kwamba wao wanasema kweli kwa sababu hakuna wala mmoja wao aliyeshuhudia jambo. Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
قَالُوا تَقَاسَمُوا بِاللَّـهِ لَنُبَيِّتَنَّهُ وَأَهْلَهُ ثُمَّ لَنَقُولَنَّ لِوَلِيِّهِ مَا شَهِدْنَا مَهْلِكَ أَهْلِهِ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ ﴿٤٩﴾
Wakasema: Apishaneni kwa Jina la Allaah kwamba tutamhujumu (Swaalih) kwa siri usiku na ahli yake, kisha tutasema kwa jamaa yake wa karibu: Hatukushuhudia maangamizi ya ahli yake; nasi hakika ni wa kweli. Akaapa kila mmoja kati yao na kuchukua ahadi kwamba usiku ule, yeyote atakayeonana na Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) amuue.
Lakini Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Alimuokoa Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) pamoja na kuikoa aila yake na wale walioamini kwa kuwaondosha usiku ule kwenda sehemu nyingine. Hivyo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akapanga mipango Yake adhimu ya kupindua njama zao na kuzifanya njama zao ziwarudie wenyewe.
Mujaahid kasema: "Wameapa kiapo na kuchukua ahadi ya kumuua lakini kabla ya hawajamfikia, wao na watu wao wakaangamizwa."
Maangamizi Ya Watu Wa Thamuwd:
Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) alikuwa ana sehemu maalumu ya kutekeleza ‘ibaada zake nayo ni katika bonde lenye mawe. Wakasema waovu hao: “Akija Swaalih kuswali tutamuua kisha tutarudi, na tukishammaliza tutakwenda kwa aila yake na kuwamaliza nao pia.”
Lakini Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akawateremshia jiwe kubwa kutoka mlimani, wakakhofia kuwa jiwe lile litawaangukia na kuwasaga, hivyo wakakimbia katika pango lakini lile jiwe likaziba upenyo wa pango hilo hali ya kuwa wamo ndani. Watu wao hawakua na khabari hiyo ya yaliyowafika! Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَمَكَرُوا مَكْرًا وَمَكَرْنَا مَكْرًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٥٠﴾
Wakapanga njama Nasi Tukapanga mipango ya kuvurumisha njama nao huku hawatambui.
Ikawa hiyo ni moja katika adhabu za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa watu wa Thamuwd, na wengineo Akawaadhibu kwa maangamizi mengineyo kama Alivyotaja Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَأَخَذَ الَّذِينَ ظَلَمُوا الصَّيْحَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دِيَارِهِمْ جَاثِمِينَ﴿٦٧﴾
Na wale waliodhulumu uliwachukuwa ukelele angamizi, wakapambazukiwa wameanguka kifudifudi majumbani mwao (wamekufa). [Huwd: 67] Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akamuokoa Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) pamoja na wale walioamini kama Anavyosema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا صَالِحًا وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَمِنْ خِزْيِ يَوْمِئِذٍ ۗ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ الْقَوِيُّ الْعَزِيزُ﴿٦٦﴾
Basi ilipokuja amri Yetu, Tulimuokoa Swaalih na wale walioamini pamoja naye kwa rahmah kutoka Kwetu, na kutokana na hizaya ya Siku hiyo. Hakika Rabb wako Yeye Ndiye Mwenye nguvu, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika
وَأَخَذَ الَّذِينَ ظَلَمُوا الصَّيْحَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دِيَارِهِمْ جَاثِمِينَ﴿٦٧﴾
Na wale waliodhulumu uliwachukuwa ukelele angamizi, wakapambazukiwa wameanguka kifudifudi majumbani mwao (wamekufa).
كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا فِيهَا ۗ أَلَا إِنَّ ثَمُودَ كَفَرُوا رَبَّهُمْ ۗ أَلَا بُعْدًا لِّثَمُودَ﴿٦٨﴾
Kama kwamba hawakuishi wakineemeka humo. Tanabahi! Hakika kina Thamuwd walimkufuru Rabb wao. Tanabahi! Wameangamiziliwa mbali kina Thamuwd. [Huwd: 66-68]
Maangamizi yao yalikuwa baada ya siku tatu kama ilivyotajwa:
فَعَقَرُوهَا فَقَالَ تَمَتَّعُوا فِي دَارِكُمْ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ ۖ ذَٰلِكَ وَعْدٌ غَيْرُ مَكْذُوبٍ﴿٦٥﴾
Basi wakamuua; (Swaalih) akasema: Stareheni majumbani mwenu siku tatu. Hiyo ni ahadi isiyo ya uongo. [Huwd: 65] Maangamizi yalianza kuwadhihirikia kama walivyoonywa na Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam). Nayo yalianza siku ya Alkhamys, nyuso zao zikaanza kubadilika rangi kuwa manjano. Kisha siku ya Ijumaa zikawa nyekundu. Kisha siku ya Jumamosi nyuso zao zikageuka kuwa nyeusi kabisa. Baada ya kuchomoza jua siku ya Jumapili wakawa wanangojea wakitaja kujua ni adhabu gani hiyo itawafika ambayo Nabiy Swaalih ('alayhis-salaam) aliwaonya:
Ikaanza kumiminika mvua ya nguvu ya umeme na radi kisha ikafuatia mtetemeko wa ardhi mkali ambao uliharibu mji mzima na kuwaangamiza watu wake. Mji ulitingishwa na viumbe vyote vilivyokuwemo humo vilikufilia mbali. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
فَأَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دَارِهِمْ جَاثِمِينَ ﴿٧٨﴾
Basi ikawachukua tetemeko la ardhi wakawa majumbani mwao wenye kuanguka kifudifudi (wamekufa). [Al-A’raaf: 78] Athari za adhabu za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kaumu mbali mbali waliokanusha Rusuli wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) zipo bado duniani sehemu mbali mbali kwa mfano: Adhabu ya watu kaumu ya Nabiy Luutw ('alayhis-salaam) ilikuwa ni bahari iliyokufa inayojulikana kwa ‘the dead sea’. Ndio maana Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema katika Aayah kadhaa:
قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ ثُمَّ انظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ ﴿١١﴾
Sema: Nendeni katika ardhi, kisha mtazame vipi ilikuwa hatima ya wenye kukadhibisha. [Al-An’aam: 11] Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ دَمَّرَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ ۖ وَلِلْكَافِرِينَ أَمْثَالُهَا﴿١٠﴾
Je, hawakutembea katika ardhi wakatazama vipi imekuwa hatima ya ambao wa kabla yao? Allaah Amewadamirisha mbali, na kwa makafiri (itakuwa) mfano wa hayo. [Muhammad: 10] Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) maangamizi ya kaumu ya Thamuwd
فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ مَكْرِهِمْ أَنَّا دَمَّرْنَاهُمْ وَقَوْمَهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٥١﴾
Basi tazama vipi ilikuwa hatima ya njama zao, kwamba Tuliwadamirisha na watu wao wote.
فَتِلْكَ بُيُوتُهُمْ خَاوِيَةً بِمَا ظَلَمُوا ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٥٢﴾
Basi hizo ni nyumba ni magofu kwa sababu ya yale waliyodhulumu. Hakika katika hayo kuna Aayah (ishara, zingatio, funzo n.k.) kwa watu wanaojua. [An-Naml: 51-52]
Vile vile Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Kataja adhabu yao nyingine ya ukelele mkali ambao kabla ya kumalizika kwake ukelele huo, makafiri wote wa Thamuwd walikufa pamoja wote kwa wakati mmoja. Hakuna chochote kilichoweza kuwahifadhi, wala majumba yao ya mawe na ya kifakhari ya hayakuweza kuwalinda na adhabu hizo: Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَأَخَذَ الَّذِينَ ظَلَمُوا الصَّيْحَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دِيَارِهِمْ جَاثِمِينَ﴿٦٧﴾
Na wale waliodhulumu uliwachukuwa ukelele angamizi, wakapambazukiwa wameanguka kifudifudi majumbani mwao (wamekufa).
كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا فِيهَا ۗ أَلَا إِنَّ ثَمُودَ كَفَرُوا رَبَّهُمْ ۗ أَلَا بُعْدًا لِّثَمُودَ﴿٦٨﴾
Kama kwamba hawakuishi wakineemeka humo. Tanabahi! Hakika kina Thamuwd walimkufuru Rabb wao. Tanabahi! Wameangamiziliwa mbali kina Thamuwd. [Huwd: 67-68]
Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuhusu adhabu za kaumu ya Thamuwd:
وَأَمَّا ثَمُودُ فَهَدَيْنَاهُمْ فَاسْتَحَبُّوا الْعَمَىٰ عَلَى الْهُدَىٰ فَأَخَذَتْهُمْ صَاعِقَةُ الْعَذَابِ الْهُونِ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿١٧﴾
Na ama kina Thamuwd, Tuliwaongoza, lakini walistahabu upofu kuliko Uongofu basi ikawachukuwa radi na umeme angamizi wa adhabu idhalilishayo kwa yale waliyokuwa wakichuma.
وَنَجَّيْنَا الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ﴿١٨﴾
Na Tukawaokoa wale walioamini na walikuwa wenye taqwa. [Fusw-Swilat: 17-18]
Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
كَذَّبَتْ ثَمُودُ وَعَادٌ بِالْقَارِعَةِ﴿٤﴾
Kina Thamuwd na ‘Aad walikadhibisha tukio lenye kugongagonga na kutia kiwewe nyoyo.
فَأَمَّا ثَمُودُ فَأُهْلِكُوا بِالطَّاغِيَةِ﴿٥﴾
Ama kina Thamuwd, waliangamizwa kwa ukelele mkali uliovuka mipaka. [Al-Haaqah: 4-5]
Maelezo zaidi kuhusu adhabu za kaumu ya Thamuwd:
فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ ﴿٣٠﴾
Basi vipi ilikuwa adhabu Yangu na maonyo Yangu?
إِنَّا أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ صَيْحَةً وَاحِدَةً فَكَانُوا كَهَشِيمِ الْمُحْتَظِرِ ﴿٣١﴾
Hakika Sisi Tumewapelekea ukelele angamizi mmoja tu, basi wakawa kama mabuwa yaliyokatika-katika ya mtengenezaji zizi. [Al-Qamar: 30-31] As-Sudi kasema: “Walikuwa kama nyasi kavu za kichaka katika jangwa, zinapoungua na kupeperushwa na upepo.” Ibn Zayd kasema "Waarabu walikuwa wakisimamisha 'Hizar' (kutokana na neno 'almuhtazir') ambayo ni kichaka kikavu, (walichowazungushia) wakiwawekea ngamia na ngo'mbe. Ndipo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Aliposema:
فَكَانُوا كَهَشِيمِ الْمُحْتَظِرِ ﴿٣١﴾
Basi wakawa kama mabuwa yaliyokatika-katika ya mtengenezaji zizi. [Al-Qamar: 31] Na pia kauli za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuhusu kaumu ya Thamuwd:
كَذَّبَتْ ثَمُودُ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٤١﴾
Kina Thamuwd walimkadhibisha Rusuli.
إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ صَالِحٌ أَلَا تَتَّقُونَ ﴿١٤٢﴾
Alipowaambia ndugu yao Swaalih: Je, hamtokuwa na taqwa?
إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ ﴿١٤٣﴾
Hakika mimi kwenu ni Rasuli mwaminifu.
فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿١٤٤﴾
Basi mcheni Allaah na nitiini.
وَمَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٤٥﴾
Na wala sikuombeni ujira wowote juu yake. Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Rabb wa walimwengu.
أَتُتْرَكُونَ فِي مَا هَاهُنَا آمِنِينَ ﴿١٤٦﴾
Je, mtaachwa mkiwa katika amani kwenye haya hapa mliyonayo?
فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ ﴿١٤٧﴾
Katika mabustani na chemchemu
وَزُرُوعٍ وَنَخْلٍ طَلْعُهَا هَضِيمٌ ﴿١٤٨﴾
Na mimea na mitende makole yake laini, yamewiva.
وَتَنْحِتُونَ مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتًا فَارِهِينَ ﴿١٤٩﴾
Na mnachonga majabalini nyumba kwa uhodari kabisa.
فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿١٥٠﴾
Basi mcheni Allaah na nitiini.
وَلَا تُطِيعُوا أَمْرَ الْمُسْرِفِينَ ﴿١٥١﴾
Na wala msitii amri ya wenye kupindukia mipaka.
الَّذِينَ يُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ وَلَا يُصْلِحُونَ ﴿١٥٢﴾
Ambao wanafanya ufisadi katika ardhi na wala hawatengenezi.
قَالُوا إِنَّمَا أَنتَ مِنَ الْمُسَحَّرِينَ ﴿١٥٣﴾
Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa waliorogwa.
مَا أَنتَ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا فَأْتِ بِآيَةٍ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿١٥٤﴾
Wewe si chochote isipokuwa mtu kama sisi; basi lete Aayah (dalili, muujiza) ukiwa wewe ni miongoni mwa wakweli.
قَالَ هَـٰذِهِ نَاقَةٌ لَّهَا شِرْبٌ وَلَكُمْ شِرْبُ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ ﴿١٥٥﴾
Akasema: Huyu hapa ngamia jike ana zamu ya kinywaji, nanyi mna zamu ya kinywaji siku maalumu.
وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابُ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿١٥٦﴾
Na wala msimguse kwa uovu, ikaja kukuchukueni adhabu ya Siku adhimu.
فَعَقَرُوهَا فَأَصْبَحُوا نَادِمِينَ ﴿١٥٧﴾
Basi wakamuua wakapambazukiwa wenye kujuta.
فَأَخَذَهُمُ الْعَذَابُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٥٨﴾
Ikawachukuwa adhabu. Hakika katika hayo pana Aayah (ishara, zingatio n.k.), lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini. [Ash-Shu’araa: 141-158]
Maelezo zaidi ya kisa cha watu wa Thamuwd katika kauli za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِالنُّذُرِ ﴿٢٣﴾
Kina Thamuwd waliwakadhibisha Waonyaji.
فَقَالُوا أَبَشَرًا مِّنَّا وَاحِدًا نَّتَّبِعُهُ إِنَّا إِذًا لَّفِي ضَلَالٍ وَسُعُرٍ ﴿٢٤﴾
Wakasema: Ah! Tumfuate binaadamu miongoni mwetu? Hakika hapo sisi tutakuwa katika upotofu na wazimu.
أَأُلْقِيَ الذِّكْرُ عَلَيْهِ مِن بَيْنِنَا بَلْ هُوَ كَذَّابٌ أَشِرٌ ﴿٢٥﴾
Ah! Ameteremshiwa ukumbusho baina yetu? Bali yeye ni muongo mkubwa mfidhuli mwenye kutakabari mno.
سَيَعْلَمُونَ غَدًا مَّنِ الْكَذَّابُ الْأَشِرُ ﴿٢٦﴾
Watakuja kujua kesho nani muongo mkubwa mfidhuli mwenye kutakabari mno.
إِنَّا مُرْسِلُو النَّاقَةِ فِتْنَةً لَّهُمْ فَارْتَقِبْهُمْ وَاصْطَبِرْ ﴿٢٧﴾
Hakika Sisi Tutawapelekea ngamia jike awe jaribio kwao, basi (ee Nabiy Swaalih عليه السلام) watazame na vuta subira.
وَنَبِّئْهُمْ أَنَّ الْمَاءَ قِسْمَةٌ بَيْنَهُمْ ۖ كُلُّ شِرْبٍ مُّحْتَضَرٌ ﴿٢٨﴾
Na wajulishe kwamba maji ni mgawanyo baina yao (ngamia na wao), kila sehemu ya maji itahudhuriwa (kwa zamu).
فَنَادَوْا صَاحِبَهُمْ فَتَعَاطَىٰ فَعَقَرَ ﴿٢٩﴾
Wakamwita swahibu wao, akakamata (upanga) akaua (ngamia).
فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ ﴿٣٠﴾
Basi vipi ilikuwa adhabu Yangu na maonyo Yangu?
إِنَّا أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ صَيْحَةً وَاحِدَةً فَكَانُوا كَهَشِيمِ الْمُحْتَظِرِ ﴿٣١﴾
Hakika Sisi Tumewapelekea ukelele angamizi mmoja tu, basi wakawa kama mabuwa yaliyokatika-katika ya mtengenezaji zizi. [Al-Qamar: 23-31]
Na katika Suwrah Huwd:
وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ هُوَ أَنشَأَكُم مِّنَ الْأَرْضِ وَاسْتَعْمَرَكُمْ فِيهَا فَاسْتَغْفِرُوهُ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ ۚ إِنَّ رَبِّي قَرِيبٌ مُّجِيبٌ﴿٦١﴾
Na kwa Thamuwd (Tulimpeleka) ndugu yao Swaalih. Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Yeye Ndiye Aliyekuanzisheni katika ardhi, na Akakufanyieni makazi humo; basi mwombeni maghfirah, kisha tubieni Kwake. Hakika Rabb wangu Yuko Karibu kwa ujuzi Wake, Mwenye kuitikia.
قَالُوا يَا صَالِحُ قَدْ كُنتَ فِينَا مَرْجُوًّا قَبْلَ هَـٰذَا ۖ أَتَنْهَانَا أَن نَّعْبُدَ مَا يَعْبُدُ آبَاؤُنَا وَإِنَّنَا لَفِي شَكٍّ مِّمَّا تَدْعُونَا إِلَيْهِ مُرِيبٍ﴿٦٢﴾
Wakasema: Ee Swaalih! Kwa yakini ulikuwa kwetu mwenye kutarajiwa (khayr) kabla ya haya. Je, unatukataza kuabudu wale wanaowaabudu baba zetu; na hakika sisi tumo katika shaka na wasiwasi katika unayotuitia.
قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَآتَانِي مِنْهُ رَحْمَةً فَمَن يَنصُرُنِي مِنَ اللَّـهِ إِنْ عَصَيْتُهُ ۖ فَمَا تَزِيدُونَنِي غَيْرَ تَخْسِيرٍ﴿٦٣﴾
(Swaalih) Akasema: Enyi kaumu yangu! Je, mnaonaje ikiwa niko katika hoja bayana kutoka kwa Rabb wangu, na Amenipa rahmah (Unabiy na risala) kutoka Kwake basi nani atakayeninusuru nikimuasi? Basi hamnizidishii ila khasara.
وَيَا قَوْمِ هَـٰذِهِ نَاقَةُ اللَّـهِ لَكُمْ آيَةً فَذَرُوهَا تَأْكُلْ فِي أَرْضِ اللَّـهِ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابٌ قَرِيبٌ﴿٦٤﴾
Enyi kaumu yangu! Huyu ni ngamia jike wa Allaah, ni Aayah (miujiza, ishara) kwenu, basi mwacheni ale katika ardhi ya Allaah, na wala msimguse kwa uovu ikakupateni adhabu iliyo karibu.
فَعَقَرُوهَا فَقَالَ تَمَتَّعُوا فِي دَارِكُمْ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ ۖ ذَٰلِكَ وَعْدٌ غَيْرُ مَكْذُوبٍ﴿٦٥﴾
Basi wakamuua; (Swaalih) akasema: Stareheni majumbani mwenu siku tatu. Hiyo ni ahadi isiyo ya uongo.
فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا صَالِحًا وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَمِنْ خِزْيِ يَوْمِئِذٍ ۗ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ الْقَوِيُّ الْعَزِيزُ﴿٦٦﴾
Basi ilipokuja amri Yetu, Tulimuokoa Swaalih na wale walioamini pamoja naye kwa rahmah kutoka Kwetu, na kutokana na hizaya ya Siku hiyo. Hakika Rabb wako Yeye Ndiye Mwenye nguvu, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika.
وَأَخَذَ الَّذِينَ ظَلَمُوا الصَّيْحَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دِيَارِهِمْ جَاثِمِينَ﴿٦٧﴾
Na wale waliodhulumu uliwachukuwa ukelele angamizi, wakapambazukiwa wameanguka kifudifudi majumbani mwao (wamekufa).
كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا فِيهَا ۗ أَلَا إِنَّ ثَمُودَ كَفَرُوا رَبَّهُمْ ۗ أَلَا بُعْدًا لِّثَمُودَ﴿٦٨﴾
Kama kwamba hawakuishi wakineemeka humo. Tanabahi! Hakika kina Thamuwd walimkufuru Rabb wao. Tanabahi! Wameangamiziliwa mbali kina Thamuwd. [Huwd: 61-68]
Athari Za Maangamizi Ya Kaumu Ya Thamuwd Zingalipo Duniani:
Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesimulia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa akipita nyumba za kaumu ya Thamuwd wakati akielekea na jeshi lake la Maswahaba kwenda katika vita vya Tabuwk, alisimama hapo, kisha Maswahaba wakachota maji katika visima ambavyo watu wa Thamuwd walikuwa wakichota maji. Wakatumia maji kukandia unga wao wa kupikia mikate, na wakajaza maji ya kunywa katika mifuko yao ya ngozi (viriba). Lakini Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaamrisha wayamwage maji na unga waliokanda walishe ngamia wao. Kisha akaondoka nao mpaka wakafika katika kisima ambacho ngamia wa Thamuwd alikuwa akinywa maji, akawaonya wasiingie kwa watu walioangamizwa kwa kuwaambia: "Nakhofu msije kupatwa yale yaliyowapata wao, kwa hiyo msiingie kwao."
Riwaayah nyingine imesema:
عن عبد الله بن عمر قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم وهو بالحجر: ((لا تدخلوا على هؤلاء المعذبين، إلا أن تكونوا باكين، فإن لم تكونوا باكين فلا تدخلوا عليهم، أن يصيبكم مثل ما أصابهم)). أخرجاه في (الصحيحين) من غير وجه.
Abdullaah Bbin 'Amr amehadithia: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema pindi alipokuwa Hijr "Msiingie kwao hawa walioadhibiwa, isipokuwa muingie na huku mnalia, na kama hamlii basi msiingie kwao msije kufikwa na masaibu kama yaliyowafikia wao)) [Al-Bukhari na Muslim]
Na Allaah Anajua zaidi
لَقَدْ كَانَ فِي قَصَصِهِمْ عِبْرَةٌ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ۗ مَا كَانَ حَدِيثًا يُفْتَرَىٰ وَلَـٰكِن تَصْدِيقَ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَتَفْصِيلَ كُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿١١١﴾
Kwa yakini katika visa vyao kuna mafunzo kwa wenye akili. Haikuwa (Qur-aan) hadithi zinazotungwa, lakini ni sadikisho la (vitabu) vya kabla yake na tafsili ya waziwazi ya kila kitu, na ni mwongozo na rahmah kwa watu wanaoamini. [Yuwsuf: 111]

Comments
Post a Comment