KISA CHA NABII AYYUWB
KISA CHA NABII AYYUWB
Kwa mujibu wa Muhammad ibn Is'haq ibn Yasar ﺭﺣﻤﻪ ﺍﻟﻠﻪ_ ambaye ni mwanahistoria wa Kiislamu aliyeishi Madina (704 - 770 AD), Nabii Ayyub عليه سلام alikuwa mtu wa Rumi. Jina lake kamili ni _Ayyub ibn Mose ibn Razih ibn Esau ibn Is'haq ibn Ibrahim ﻋﻠﻴﻬﻢ ﺍﻟﺴﻼﻡ. Ni mjukuu wa Nabii Ibrahim عليه سلام kupitia kwa Is'haq عليه سلام. Yako mapokezi mengi, ila mapokezi haya ndiyo yenye nguvu zaidi.
Mama yake alikuwa binti wa Nabii Lutwi عليه سلام, na mkewe alikuwa kizazi cha Nabii Yusuf عليه سلام.
Nabii Ayyub عليه سلام alikuwa mchamungu sana, mwenye subira na mvumilivu sana, ndio akatajwa na Allah ﻋﺰﻭﺟﻞ katika Qur'an:
"Bila shaka tulimkuta ni mwenye subira, mja mwema, kwa hakika alikuwa mnyenyekevu sana." (Q 38:44).
Kundi la malaika lilikuwa likiwajadili binadamu, na mmoja wao akasema: "Kiumbe bora katika ardhi leo ni Ayyub عليه سلام. Ana mwenendo uliotukuka, mwenye subira sana na anayemtaja Allah ﻋﺰﻭﺟﻞ wakati wote. Ni kielelezo bora cha wanaomuabudu Allah ﻋﺰﻭﺟﻞ. Malipo yake, Mola wake amemjaalia umri mrefu na watumishi wengi pamoja na fungu la masikini na wenye shida katika mali yake. Anawalisha na kuwavisha masikini na hununua watumwa ili kuwaacha huru. Alivyo mpole na muungwana huwafanya wanaopokea msaada wake wajihisi kama vile wanamfanyia hisani (kwa ile kupokea msaada anaowapa)."
HUSDA YA IBILISI JUU YA AYYUB عليه سلام:
Ibilisi aliudhika kusikia yote haya. Alianza kumshawishi Ayyub عليه سلام akiwa ndani ya swala kwa kumnong'oneza mambo mbali mbali, lakini Ayyub عليه سلام hakuyumba.
IBILISI AANGAMIZA MALI YA AYYUB عليه سلام:
Ibilisi akalalamika kwa Allah ﻋﺰﻭﺟﻞ kwamba Ayyub عليه سلام hakuwa anamuabudu kwa ukweli, ila alifanya hivyo ili kumridhisha yeye Allah ﻋﺰﻭﺟﻞ ili asimnyang'anye mali yake. Ili (Allah ﻋﺰﻭﺟﻞ) kumuonesha Ibilisi ukweli na subira ya Ayyub عليه سلام, akamruhusu yeye na wasaidizi wake wafanye chochote wanachotaka juu ya mali ya Ayyub عليه سلام.
Ibilisi alifurahi sana, wakajikusanya, wakaanza kuangamiza mifugo, watumishi na mashamba ya Ayyub عليه سلام hadi mali yote ikaisha. Kisha Ibilisi huku akifuta mikono yake kwa furaha akajitokeza mbele ya Ayyub عليه سلام katika sura ya mwanamume mzee mwenye busara, akamwambia: "Mali yako yote imepotea; baadhi ya watu wanasema ni kwa sababu unatoa mno sadaka na kwamba unapoteza muda kumuabudu Allah ﻋﺰﻭﺟﻞ. Wengine wanasema Allah ﻋﺰﻭﺟﻞ amekuletea hili (janga) ili kuwafurahisha maadui zako. Kama Allah ﻋﺰﻭﺟﻞ angekuwa na uwezo wa kuzuia dhara basi angelinda mali yako."
Akisimamia imani yake, Ayyub عليه سلام akamjibu: "Alichochukua Allah ﻋﺰﻭﺟﻞ kwangu ni mali yake. Nilikuwa mwangalizi wake (hiyo mali) kwa muda mchache. Humpa amtakaye na humnyima amtakaye." Na kwa kauli hii Ayyub عليه سلام akamsujudia Mola wake.
IBILISI AANGAMIZA WATOTO WA AYYUB عليه سلام:
Ibilisi alipoona hivi akachanganyikiwa, akamkabili tena Allah ﻋﺰﻭﺟﻞ, akamwambia: *_"Nimemuondoshea Ayyub mali yake yote, na bado anakushukuru. Hata hivyo anaficha kukata kwake tamaa tu, kwani anawatumainia watoto wake ambao ni wengi. Mtihani halisi kwa mzazi ni kupitia kwa watoto wake, utaona jinsi Ayyub atakavyokukana."
Allah ﻋﺰﻭﺟﻞ akampa mamlaka juu ya watoto wa Ayyub عليه سلام, lakini akamuonya kwamba haitapunguza imani wala subira ya Ayyub عليه سلام kwa Mola wake.
Ibilisi akakusanya wasaidizi wake, wakaporomosha nyumba waliyokuwa wakiishi watoto wa Ayyub عليه سلام, wakawaua wote. Kisha akajigeuza kama mtu anayekwenda kutoa pole, akamfuata Ayyub عليه سلام. Kwa sauti ya kuliwaza akamwambia: "Mazingira ya kifo cha watoto wako yanahuzunisha. Hakika Mola wako hakulipi sawa na swala zako zote (unazoswali)."_* Hapa akatarajia Ayyub عليه سلام kumkana Mola wake.
Ayyub عليه سلام akamvunja moyo tena, akamjibu: "Baadhi ya muda Allah hutoa, na baadhi ya muda huchukua. Baadhi ya muda huridhika na matendo yetu, na baadhi ya muda haridhiki. Iwe kitu kina manufaa au madhara kwangu, nitasimama thabiti katika imani yangu na kumshukuru Muumba." Kisha akamsujudia Mola wake. Kwa hili Ibilisi alizidi kuvurugikiwa.
Dua ya Ayyuub(a.s)
Nabii Ayyuub(a.s) aliendelea na maradhi yale mazito kwa kipindi kirefu (ina semekana miaka saba). Mwishowe akaona amuelekee Mola wake na kumuomba amuondolee maradhi yale kama tunavyojifunza katika ya zifuatazo:
Na (Mtaje) Ayyubu, alipomwita Mola wake (akasema) “Mimi imenipata dhara, nawe ndiwe Unayerehemu kuliko wote wanaorehemu.” (21:83)
Dua ya Ayyuub(a.s) ilikuwa makubuli kwa Mola wake kumuelekeza dawa ya matibabu yale:
(Mwenyezi Mungu akamwambia):- “Uharikishe mguu wako (patachimbuka chemchem chini yake, maji yake yatakuwa dawa yako). Basi haya maji baridi ya kuogea (koga), na (haya maji baridi) ya kunywa, (yanywe).” (38:42)
Baada ya kutumia dawa hii Nabii Ayyuub(a.s) alikuwa mzima wa afya kama alivyokuwa hapo awali kabla ya ugonjwa. Furaha zaidi kwake, pamoja kurudishiwa afya yake, pia alirudishiwa mali na watu wake kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:
Basi tukamkubalia (wito wake) na tukamuondolea dhara aliyokuwa nayo, na tukampa watu wake na mfano wao pamoja nao. Ni rehema inayotoka kwetu, na ukumbusho (mzuri kwa wafanyao Ibada. (21:84)
Na tukampa watu wake na wengine kama wao pamoja nao, kwa rehema itokayo kwetu, na (ipate kuwa) mauidha kwa watu wenye akili. (38:43)
INAENDELEA KATIKA APP YA KISA CHA NABII AYUBU INAYOPATIKANA GOOGLE PLAYSTORE

Comments
Post a Comment