HISTORIA YA NABII NUHU (A.S)
HISTORIA YA NABII NUHU (A.S)
Kabla ya Kuja kwa Nabii Nuhu A.S na Kuondoka kwa Wanazuoni Baada ya karne 10 kupita tokea kufa kwa Nabii Adam (A.S) Shetani akawa anaendelea kufanya kazi ya kukibadilisha kizazi kuelekea kumuasi Allah (S.W). Wanazuoni wengi kipindi hichowalikufa na watu zikajawa nyoyo zao na huzuni kubwa, na wakawa wanakaa na kuwakumbuka na kuzungumzia habari zao.
Siku moja Iblisi alipita na kuwaona wakizungumza mazuri yaliyofanywa na wanazuoni mpaka wakawa wanalia. Iblisi akawaza na kuona kuwa hii ndio njia ya kuyatimiza yale mabaya aliyoyaahidi kuyafanya mbele ya Allah (S.W), akawauliza sababu ya kulia kwao. Watu hao wakamjibu : ‘’Sisi tuliondokewa na wanazuoni wetu ambao walitupa chakula cha roho,walitutowa kwenye giza na kutupeleka kwenye nuru’’. Iblis akawaambia kuwa, ‘’Hilo ni jambo dogo sana, ina maana mnahuzunika kwa kuwa hawapo tu?
Mimi nitakupeni njia ya kuwatowa kwenye huzunizenu’’. Watu wakawa na hamu ya kutaka kujuwa. Akaendelea kusema Iblis,‘’Jengeni katika kila sehemu waliyokaa mashekhe wenu masanamu yao na kila siku mkiyaangalia na huzuni zenu zitaondoka’’. Watu wakaona njia hiyo ni sawa na wakawa wanatengeneza masanamu ya mashekhe wao waliopita waliohitaji kuwaona.
Hivyo njama zote hizo Iblisi alizifanya kwa makusudi ili umma huu unaojuwa mengi katika dini utaondoka naumma utakaokuja uwe ni rahisi kwake kuuingiza katika shirki.
Hivyo watu wakadumu katika hali hiyo mpaka kizazi chao kikaondoka nakuja kizazi cha watoto wao. Iblisi akawajia watoto wao hao, akawakusanya nakuwaambia, ‘’Mnajuwa baba zenu waliabudia kitu gani?
Wakauliza, ‘’Kwani nini?’’. Iblisi akawaambia, ‘’Mnawaona hawa? Hawa ni waungu wa baba zenu. Babazenu walikuwa na heshima sana kwa watu hawa. Sasa nyinyi mnataka kwenda kinyume na ibada walizozifanya baba zenu? Na atakaekwenda kinyume na hivyo basi atakuwani mkosevu’’. Moja kwa moja watoto hao wakaingia katika ibada ya kuabudia masanamu ambapo ibada hiyo ikawa ni ibada ya mwanzo na ibada yao kuu.
Kuja kwa Nabii Nuhu A.S , Kama Allah S.W alivyoahidi katika Quran kuwa hatowaadhibu watu ispokuwa mpaka awapelekee ubainifu (uongofu) kupitia mjumbe, akamleta Nuhu A.S , kwa qaumu hii ili awalinganie waache ibada hiyo ya masanamu. Allah SW anasema katika Quran, ‘’Na tulimpeleka Nuhu kwenda kwa watuwake, akawaambia hakika mimi kwenu ni muonyaji aliyewazi kwenu nyinyi kwambamsiabudu (yeyote) ispokuwa Allah na naogopa isije ikakupateni adhabu siku yakiama.
Wakasema ambao wamekufuru : Nuhu sisi hatukuoni (yeyote) ispokuwa weweni mtu kama sisi, na hao walikufuata tunawaona ni watu madhalili mno (watuwenye maisha duni). Kauli zao ni dhaifu na hatuoni ubora wowote mlionao kulikosisi. Na sisi tunakuoneni ni waongo tu.’’ Nuhu akasema, ‘’Hamuoni kama nipo katika ubainifu kutoka kwa molawangu? Mungu kanipa rehma zake akanichagua. Enyi watu wangu sihitajii chochote kutoka kwenu bali ujira wangu upo kwa Allah na hawa mnaowaona wadhalilifu, basimimi siwafukuzi.
Hakika wao watapewa mema na mola wao lakini nyinyi nakuonenini watu mnaoufanya ujinga kuwa ndo mfumo wenu.’’ Baadae Nuhu akarudi kwake Allah na kusema, ‘’Mola wangu hakika mimi nimewalingania watu wangu usiku na mchana na sikupata chochote ila waliponionawao walinikimbia.’’
Kuendelea kwa Maasi ya Watu wa Nuhu A,S Nuhu aliishi kwa muda wa miaka mingi sana na kupelekea kulingania dinikwa muda wa miaka 900, kiasi ambacho vizazi vingi vilipita katika uhai wake. Hivyo ikawa kila baba alipoona anakufa basi alikuwa anamchukuwa mwanawe hadi kwa Nuhu na kumwambia mwanawe, ‘’Ewe mwanangu karibuni mimi nitakufa.
Pindi nitakapokufa wasia wangu wa kwanza mwanangu huyu usimuamini kwani huyu ni mwendawazimu.’’ Allah anaendelea kusema katika Quran, ‘’Walimkadhibisha mja wetu Nuhu na wakasema ni mwenda wazimu lakini Nuhu hakukata tamaa akawa anakwendakulingania usiku na mchana. Lakini vilevile alikimbiwa tena aliudhiwa sana Nabii Nuhu katika da’wa lakini hakuvunjika moyo.’’
Nuhu akasema kumshtakia Allah, ‘’kila nikiwaita waja wako wapate kukutambua basi wanatia vidole vyao katika masikio yao. Na wanajifunika maguoyao na kuleta kiburi pia. Na wakajilazimisha kutoacha ibada yao ya masanamu.Kisha nikaanza kuwalingania dhahir (wazi wazi), kisha nikawalingania kwa siri. Hivyo ikawa ni vigumu Nuhu kumpata mtu katika imani kwa vile wasia uliendelezwa kutoka kwa baba kwenda kwa watoto katika kila kizazi.
Nuhu akawa anamshtakia Allah na kuwatia hofu watu wake juu ya adhabu kali kutoka kwaAllah. Watu wake wakasema, ‘’Ewe Nuhu umetujadili sisi na ukazidisha mijadalayako. Sasa tujie na kile ulichoahidiwa ikiwa wewe ni mkweli’’. Nuhu akasema kuwajibu watu hao, ‘’Mungu ndie atakaeleta atakapopenda,na nyinyi hamna ubavu wa kuzuia adhabu hiyo na wala nasaha zangu hazitokufaenikwa chochote’’. Nuhu akainuwa mikono na kusema. ‘’Mola wangu nimeshindwa mimi sasaniokoe’’.
Jahazi la Nabii Nuhu A, S
Hapo Nuhu akaamrishwa kupanda mti na kujenga jahazi huku akimuambia kuwa hao walioamini nia hao hao tu, sasa atafute njia ya kuwaokoa waende sehemu nyengine’’. Nuhu akapanda mti mpaka ulipokuwa mkubwa, akaukata na kuanza kazi yakuchonga jahazi akisaidiwa na watu waliomuamini tu.
Makundi ya watu waliokuwa wakipita njiani hapo yalimshangaa sana na kumfanyia maskhara mengi sana nakumwambia, ‘’Ewe Nuhu sasa umekuwa fundi seremala baada ya kuwa Mtume?’’. Nuhu akawajibu, ‘’Ikiwa mnatufanyia maskhara sisi, hakika sisitutakufanyieni maskhara kama mnavyotufanyia’’. Watu hao kilichowashangaza ni kwamba inakuwaje Nuhu anajenga jahazi wakati maji ya bahari yapo mbali sana na walipo. Hivyo jahazi hilo litapelekwa vipi baharini na watu wachache? Nuhu alipomaliza akawa anaendelea kumshtakia Allah, basi Allah anasema katika Qurani tukufu: ‘’Na tukaifungua mifereji yenye kububujika maji mengi mno kutokambinguni.
Na ardhi tuakichana ikawa ni mto. Basi maji yote yakakutana kwa amri(yake Allah). Sasa Nuhu endelea kusubiri itakujia amri yetu. Wabebe na wachukuwe kila katika viumbe wawili wawili (kike na kiume). Na chukuwa watu wako walioamini wote ila niachie hao makafiri’’.
Hivyo Nuhu baada ya kushindwa na watu wake alipeleka ripoti kwa Allah baada ya kukata tama na kazi yake, Nuhu alimwambia Allah S.W : ‘’Ewe mola Wangu hakika wao wameniasi mimi na wakafuata ambavyo haviwaongezei chochote duniani wala akhera ispokuwa hasara tu. Na wananifanyiavitimbi vikubwa na wakasema : Msiwaache miungu yenu, na wala msimuache Wadda, wala Suwara, wala Yaghuutah, wala Naswra (Yote ni majina ya wanazuoni waliopita).
Na wamewapoteza wengi sana,wala usizidishe kwa makafiri ispokuwa ni upotevu, kwa sababu ya makosa yao wenyewe. Yamewagharikisha na yamewaingiza motoni. Na hawakupata yeyote mwenye kuwanusuru na adhabu hiyo. Na vile vile Nuhu akasema : Ewe mola usiache chochote juu ya mgongo wa ardhi miongoni mwa makafiri’’. Allah S.W alimpelekea wahyi Nuhu kwa kumwabia , ‘’Ewe Nuhu hakuna atakae kuamini tena miongoni mwa watu hao sasa usijali kitakachokuja baadae’’.
Maulamaa hapa wanatofautiana katika kubainisha idadi ya waliosilimu, baadhi yao wanasema ni watu 80 na wengine husema ni watu 70 ambao ndio waliosilimu katika miaka yote hiyo. Sayyidina Nuhu akatengeneza jahazi naye Allah S.W akamwambia‘’Waingize kila katika viumbe wawili wawili, mke na mume’’. Hadithi Iliyopokelewana Ibnu Abbas Ibnu Abas anasema kuwa : Siku moja Nabii Issa alitembelea na wanafunziwake Banii Israiil.
Wanafunzi wake wakamuuliza Nabii Issa kuhusu jahazi laNabii Nuhu. Nabii Issa akawachukuwa mpaka kwenye kaburi moja la zamani mno,hapo akawaambia wakae chini. Akawauliza wanafunzi wake hao, ‘’Je! Mnakijuwa hicho mbele yenu na ni kitu gani?’’. Wanafunzi wale wakasema kuwa hawajui. Nabii Issa akawaambia, ‘’Huu ni unyayo wa Haam Ibni Nuuh’’. Watoto maarufu wa nabii Nuhu ni watatu (3), nao ni : Saam, Haam na Yaafi na mwengine alikuwa anaitwa Yaafi.
Nabii Issa akaendelea kusema, ‘’Sasa tunataka kumtowa kwenye kaburi hili kwa kuwa alikuwemo kwenye jahazi, ili atupe habari kuhusu jahazi lile’’. Nabii Issa akachukuwa mchanga kutoka kaburini na akasema : Simama (Ewe Haam)kwa amri ya Allah’’. Kwa uwezo wake Allah Haam akafufuka kutoka kaburini, akasimama hali yakuwa akijikung'uta mchanga na akionekanwa kuwa ni mtu mzima sana.
Akaulizwa ‘’Hivi ndivyo ulivyokufa?’’ Haam akajibu, ‘’Hapana, lakini nilipopata uhai tena nilihisi kuwa sasani kiama na nimepata utu uzima kwa sababu ya kuhisi kuwa ni siku hiyo, sikuambayo ni nzito’’. Issa na wafuasi wake wakawa wanamuuliza, ‘’Tupe habari kuhusu jahazi la Nuuh’’. Haam akajibu, '’ Jahazi lilikuwa na khorofa tatu (3) :
Ya kwanza waliingia watu, ya pili wakaingia wanyama na ya tatu na yajuu waliingiandege’’.
Wakauliza, ‘’Na lilikuwa na urefu gani?’’ Haam akajibu : ‘’Jahazi lilikuwa na urefu wa dhiraa 1200 na upana nidhiraa 600’’.
Baada ya kumaliza kujibu maswali yao Nabii Issa akamuamrisha Haam arudi sehemu yake na akarudi. Wale wanafunzi walitaka wamchukuwe mitaani lakini Nabii Issah akawaambia, ‘’Huyu riziki zake zimeshamalizika hivyo hatoweza tena kuendelea kuishi’’.
KUINGIA KWA MARADHI YA NGOZI (MABALANGA) KWA WATU WA NABII NUHU A.S
Wakati jahazi likiwa katika hatua za mwisho za matengenezo, watuwaliomuasi Nuhu wakawa wanamfanyia vitimbi katika jahazi lake. Ndani ya jahazi mlikuwa mna hodhi kubwa ambalo walikuwa wakifanya haja kubwa na kupelekea haliya uchafu kukithiri na kuwa ni kero kwa Nuhu na waumini waliosalia. Allah akawapa mtihani watu wa Nuhu kwa maradh ya mabalanga kwenye ngozi zao. Wakajawa na upele na mwasho mkali mwilini mwao.
Siku moja alikuja bwana mmoja kujisaidi akwenye hilo hodhi ndani ya jahazi, wakati anamalizia haja zake ghafla alijikwaa na kuteleza ndani ya hilo shimo. Alipotoka akagundua kuwa yale maradhi yake yangozi yamepona ghafla. Alifurahia mno na alipofika kwa wenzake akahadithia huomkasa.
Habari zikaenea kuwa kinyesi kilichomo ndani ya jahazi la Nuhu ndiyo dawa ya maradhi yao, hivyo watu wakawa wanaingia humo kwenye hodhi na wakitoka basi wamepowa kabisa mpaka Allah akajaalia jahazi likawa ni safi kama mwanzo. Allah Anashusha Adhabu kwa Watu wa Nabii Nuhu.
Maji yalipasua ardhini na kufika hadi vileleni mwa milima. Nabii Nuhu akaamrishwa awaache waliokufuru. Allah anasema, ‘’Ardhi ilibadilika ikawaimejaa maji, maji ya aina mbili yakakutana kwa amri iliyopitishwa’’. Nuhu akausiwa kuhusu kumtegemea Allah katika safari yake mwanzo hadi mwisho.
Allah anasema katika qurani tukufu : ‘’Pandeni humo kwa bismilahi ambayo ndiyo chombo cha kuliendeshea jahazi hilo na kulitia nanga jahazihilo…’’ Hivyo watu wote walioamini na viumbe vyengine wakaingia jahazini ispokuwa mtoto wa Nabii Nuhu aliyeitwa Yaam kwa vile alikataa kuingia jahazini. Allah anasema katika Suratul – Huud, ‘’Akamwita Nuhu mwanawe(akimlingania) alikuwa sehemu mbali kidogo na jahazi.
Ewe mwanangu panda pamojana sisi na usiwe miongoni mwa waliokufuru. Mtoto akajibu : Usiwe na wasiwasi nitapanda kwenye lile jabali (kubwa) litaniokoa na maji haya. Nuhu akasema :Leo hakuna kuokoka na adhabu hii ya Mungu ispokuwa wale aliowarehemu’’. Mtoto akashikilia hivyo na Allah akawaweka mbali baba na mtoto kwamawimbi ili baba asimuone mwanawe anavyoteketea kwa mawimbi makubwa, na Yaam akazama akawa ni miongoni mwa waliokula hasara. Nuhu akanadi kwa mola wake,‘’Ewe mola umesema niwachukuwe watu wangu sasa na mwanangu ni miongoni mwa watuwangu, nawe uliniahidi kuwa watu wangu utawaokoa ijapokuwa wewe ni hakimu wamahakimu’’.
Allah anasema katika Qurani kumjibu Nuhu : ‘’Ewe Nuhu hakika yeye simiongoni mwa watu wako. Hakika yeye kafanya vitendo vibaya. Tena Nuhuusiniulize tena mambo usiyokuwa na elimu nayo, mimi nataka unasihike nausiingie katika ujinga’’.
Nuhu akaomba radhi kwa mola wake nayeye Allah akamsamehe. Jahazi ikawa inatembea usiku na mchana kwa muda wa siku 150 mpaka Allah alipoamrisha ardhi na mbingu zizuie maji. Nabii Nuhu akamtuma kunguru iliakaangalie kama ardhi imeshakauka. Kunguru kwa bahati baada ya kwenda alikutamzoga njiani na akawa anakula na kushindwa kurejea.
Nabii Nuhu alimlaani kunguru na ndiyo maanampaka hii leo kunguru hawezi kukaa na binaadamu. Akamtuma tena njiwa, njiwa akaruka na baadae akarudi jahazini kwanamna ambayo ilimpa ishara Nabii Nuhu kuwa ardhi imeshakauka. Akashusha nanga kwa bismillahi kama alivyoamrishwa na akawa kwenye ulimw engu mpya pamoja nawaliomuamini, ndege na wanyama. Sehemu waliyoshuka ilikuwa ni katika kushoto ya mji wa Sham : NiKaskazini mwa Siria na Kusini mwa Uturuki.
Sasa baada ya kuangamizwa kizazi kilichokufuru, kizazi chote kilichobakia kilikuwa ni kizazi cha waumini tu.Wakaendelea na ibada ya kumuabudu Allah bila ya kumshirikisha na chochote. Nabii Nuhu akaondoka duniani hivyo baadae Iblis aliwajia na kuwashawishi waingie katika ibada ya masanamu nao wakafuata. Hivyo kizazi hichi kikawa nikizazi cha pili kuabudia masanamu. Nabii nuhu ndie binaadamu alieishi miaka mingi zaidi duniani, aliishi miaka 950 na kunabaadhi ya wanahistori wanatuambia ilifika mpaka 1000,
MWISHO. KISA HIKI KINAPATIKA KWENYE QURANI KWENYE AYA ZIFUATAZO : -
NUUH : 23,2-4,5-10,13-20
AL-ZUMAR : 2-3
AN-NISAA'I : 163
AL-AN'AAM : 83-84,165,162-163
AL-AARAAF : 69,74,59,62,60-61,143
AL-BAQARAH : 213,37,131-133
AL-MARIAM : 56
AL-FAATIHAH : 1
AL-JAATHIYAH : 16
YUNUS : 72
HUUD : 27-32,36-37,40,42-44
AS-SHU'ARAAI : 116,119-122
AL-QAMAR : 11-12,114-116
AL-ANBIYAAI : 89-90,83-84
AL-MUUMINUUN : 27

Comments
Post a Comment