HISTORIA YA NABII IS-HAQA NA YAAQOUB

HISTORIA YA NABII IS-HAQA NA YAAQOUB


 Is-haq(a.s)  ni mtoto wa pili wa Nabii Ibrahiim(a.s), mama yake akiwa Sarah. Habari njema ya kumzaa Is-haq ilimjia Nabii Ibrahim(a.s.) mara tu baada ya kufuzu mtihani wa kumchinja mwanae mkubwa, Isma il(a.s).  Alipongezwa kwa kubashiriwa kuzaliwa kwa Is-haq(a.s.):  Amani kwa Ibrahim. Hivi ndivyo tunavyowalipa watendao mema. Bila shaka yeye alikuwa miongoni mwa waja wetu walioamini (kweli kweli).Tena tukambashiria (kumzaa) Is-haq, Nabii miongoni mwa watu wema (kabisa).  (37:109-112). 

Maelezo ya kuzaliwa Is-haq na hatimaye  Ya‘aquub(a.s.) yanapatikana  katika kisa cha  Malaika waliompa Nabii Ibrahiimu habari za kuangamizwa  watu waovu wa Nabii Lut(a.s) na zile za yeye kupata mtoto katika uzee wake.

Mafunzo Yatokanayo na Historia Nabii Is-hhaqa  na Ya’aquub(a.s)

  1. Kutenda mema kunampatia muumini faida kubwa hapa duniani na huko akhera. 
  2. Tunatakiwa tuwachague kuwa viongozi wetu wa jamii wale waliotuzidi katika matendo mema. 
  3. Ni wajibu wa Waumini kumshukuru  Allah(s.w) baada ya kupata ushindi, kufaulu au kupata mafanikio yoyote yale katika  mchakato wa maisha.

Shukurani  za  Nabii  Ibrahiim(a.s)  kwa  Allah(s.w)

Kwa neema hii ya kuruzukiwa watoto wawili - Ismail na Ishaqa(a.s), Nabii Ibrahim(a.s.) alimshukuru  Allah(s.w) kwa maneno yafuatayo:

“Namshukuru Mwenyezi Mungu aliyenipa juu ya uzee (wangu watoto wawili hawa):- Ismail na Is-haqa. Hakika Mola wangu ni mwenye kusikia maombi (ya waja wake)”  (14:39).

 Is-haqa alipofikia utu uzima naye alipewa Utume na akaruzukiwa mtoto -  Ya‘aquub(a.s) naye pia akapewa Utume. ....... .............Tulimpa Is-haqa na Ya‘akub, na kila mmoja tukamfanya Nabii.Na tukawapa rehema zetu na tukawafanyia sifa za kweli tukufu(za kusifiwa na viumbe). (19:49-50). 

Na tukawajaalia kuwa maimamu wanaoongoza kwa amri yetu, na tukawapelekea wahyi wa kuzifanya kheri na kusimamisha Sala na kutoa Zaka. Na walikuwa kwetu ni  wenye kutunyenyekea. (21:73). 

Aya tulizozinukuu zaweka wazi kuwa Is-haqa na mwanawe Ya’aquub, walikuwa Mitume na viongozi wa kusimamia utekelezaji wa sheria za  Allah(s.w).

 Na mkewe (Ibrahim - bibi Sarah) alikuwa kasimama wima, akacheka. Basi tukampa habari njema ya (kuwa watazaa mtoto wamwite) Is-haq na baada ya I’shaq (watapata mjukuu wamwite) Yaaquub.(11:71) 

(Mkewe Ibrahim) akasema: “Ee mimi we! Nitazaa na hali mimi ni mkongwe, na huyu mume wangu ni mzee sana? Hakika hili ni jambo  la ajabu.”(11:72) 

Wakasema (wale Malaika): Je, unastaajabia amri ya Mwenyezi Mungu? Rehema ya Mwenyezi Mungu na Baraka zake ziko juu yenu, enyi watu wa nyumba hii! Hakika Yeye (Mwenyezi Mungu) ndiye anayestahiki kusifiwa na kutukuzwa.”

ndiye anayestahiki kusifiwa na kutukuzwa.” (11:73)

Shukurani  za  Nabii  Ibrahiim(a.s)  kwa  Allah(s.w)

Kwa neema hii ya kuruzukiwa watoto wawili - Ismail na Ishaqa(a.s), Nabii Ibrahim(a.s.) alimshukuru  Allah(s.w) kwa maneno yafuatayo: “Namshukuru Mwenyezi Mungu aliyenipa juu ya uzee (wangu watoto wawili hawa):- Ismail na Is-haqa. Hakika Mola wangu ni mwenye kusikia maombi (ya waja wake)”  (14:39).

 Is-haqa alipofikia utu uzima naye alipewa Utume na akaruzukiwa mtoto -  Ya‘aquub(a.s) naye pia akapewa Utume. ....... .............Tulimpa Is-haqa na Ya‘akub, na kila mmoja tukamfanya Nabii.Na tukawapa rehema zetu na tukawafanyia sifa za kweli tukufu(za kusifiwa na viumbe). (19:49-50).  Na tukawajaalia kuwa maimamu wanaoongoza kwa amri yetu, na tukawapelekea wahyi wa kuzifanya kheri na kusimamisha Sala na kutoa Zaka. Na walikuwa kwetu ni  wenye kutunyenyekea. (21:73). 

Aya tulizozinukuu zaweka wazi kuwa Is-haqa na mwanawe Ya’aquub, walikuwa Mitume na viongozi wa kusimamia utekelezaji wa sheria za  Allah(s.w).

Mafunzo Yatokanayo na Historia Nabii Is-hhaqa  na Ya’aquub(a.s)

  1. Kutenda mema kunampatia muumini faida kubwa hapa duniani na huko akhera. 
  2.  Tunatakiwa tuwachague kuwa viongozi wetu wa jamii wale waliotuzidi katika matendo mema. 
  3.  Ni wajibu wa Waumini kumshukuru  Allah(s.w) baada ya kupata ushindi, kufaulu au kupata mafanikio yoyote yale katika  mchakato wa maisha.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA NABII SULEIMAAN

The Story of Prophet Dhul Kifl

Full Story of the Prophet Ayyub