HISTORIA YA NABII DHUL-KIFL

HISTORIA YA NABII DHUL-KIFL




1. MAELEZO YA IMAM IBN JARIR:

Wakati nabii Ilyaas alipoozeeka, alihitaji kupata mrithi wa kiti chake cha ufalme ambae angeweza kuwaongoza wanaisrael, hivyo alihitaji mtu mchaMungu, Mwenye hekima, busara na maarifa. Nabii Ilyaas, aliitisha mkutano wa wa viongozi mbalimbali pamoja na watu aliokuwa akiwaongoza kisha akawaambia dhumuni la mkutano huo ambao lilikuwa kumtafuta kiongozi (Naibu) ambae atamsadia kuongoza.
Ili kuhakikisha mtu anaepatikana na kuwa kiongozi  anakuwa na sifa alizohitaji, Ilyaas aliweka masharti matatu kwa yoyote anayoitaka nafasi hiyo aweze kuyatimiza.

Masharti hayo yalikuwa:

1. Kufunga mwaka mzima mchana ya bila kupoteza swaumu yoyote
2. Asali na amkumbuke Allah mchana kutwa
3. Asiwe mwenye kukasirika kamwe, na awe na hekima / busara ya maamuzi yake

Masharti hayo yalikuwa magumu mno kwa kila mtu aliekuwepo pale na hivyo kukaa kimya ingawa kila mtu aliahidi kujaribu. Bila kutarajia alijitokeza mtu mmoja mzee wa hadhi ya chini na kumwambia Alyaas kuwa angeweza kujitolea kushika nafasi hiyo na kukamalisha masharti hayo yaliyowekwa.
Watu walimdharau, ingawa hiyo haikumfanya Ilyaas kuacha kumpa nafasi hiyo. Ilyaas alimuuliza ikiwa angeweza kutimiza masharti hayo na akathibitisha ndio angeweza. 
Baada ya wiki kadhaa Ilyaas aliwaita tena watu wote na kuwauliza ikiwa kuna yeyote alieweza kukamilisha masharti yale japo kwa kipindi kile kifupi. Kila mtu alibaki kimya kuashiria kuwa hawakuweza kuyakamalisha isipokuwa mtu yule pekee ambae aliinika na kumwambia Mfalme kuwa ameyakamilisha masharti hayo.

Hapo Ilyaas hakuamini hivyo akumuomba aende aendelee na masharti hayo. Nyuma Ilyaas aliandaa kikundi cha watu kwenda kwa mzee yule kumjaribu kwa kila namna ili ashindwe kutimiza masharti yale matatu. 
Watu waliotumwa, walitumia mbinu tofautitofauti za kumfanya mzee yule ashindwe kufunga, kufanya ibada na aweze kukasirika lakini mbinu hizo ziligonga mwamba.
Watu wale walirudi kwa Ilyaas na kumwambia kuhusu khabari zile, Ilyaas aliamini lakini kabla ya kukabidhiwa nafasi ile Shaitwani ( Ibilis) aliona atumie fursa ile kumuharibia mzee yule ili ashindwe mtihani.

Katika kipindi chote hicho, mtu yule alikuwa amekwisha jiimarisha katika sala pamoja na funga huku akitumia muda mchache kulala ili kuupa mwili wake nguvu.
Siku moja Ibilis alimfata mtu huyo nyumbani kwake muda ambao alihitaji kujipumzisha baada ya ibada mbalimbali na majukumu mbalimbali. Ibilisi alifika mlangoni kwa yule mzee kisha kubisha hodi huku akisema " Nahitaji msaada, mimi ni mzee mwenye matatizo makubwa".
Ibilisi alikaribishwa ndani na akaanza kutoa malalamiko yake kuhusu ukatili, uonevu na mambo machafu anayofanyiwa . Alitoa malalamiko yake kwa muda mrefu kiasi kwamba alichukua muda wote ambao mzee yule angeutumia kujipumzisha.  Mwishoe alimtaka Ibilisi afike katika nyumba yake ya usuluhishi akiwa na watu wale wanaomfanyia ukatili.
Siku inayofuata mtu huyo alikaa katika eneo lake la usuluhishi huku akimsubiri Ibilisi lakini wala hakutokea. 

Siku iliyofuata asubuhi, mtu yule aliendeea kumsubiri  Ibilisi lakini bado hakufika. Hatiamae muda wa mchana aliamua kwenda  kwake ili kujipumzisha.
Mtu huyo alipofika kwake kabla ya kulala,  Ibilisi alifika tena nyumbani kwa mzee yule na kuanza kupiga hodi kwa vurugu.  Bila taharuki wala kuchukizwa na kitendo kile cha Ibilisi, mtu yule alimfungulia mlango na kumkaribisha huku akimuuliza " Kwanini hakuja katika nyumba ya usuluhishi ilihali alimtaka aende ila haki ipatikane?"
Ibilisi bila aibu alijibu, " Maadui zangu ni watu wabaya sana", walipoona tunakuja katika nyumba ya usuluhishi waliona tuyamalize wenyewe lakini mara ulipoondoka walifuta ahadi yao.
Kama ilivyo ada ya Ibilisi, alikaa pale huku akimuongelesha mzee yule hadi muda wake wa kulala ukawa umepotea na mwishoe akamtaka Ibilisi siku inayofuata aende tena katika Nyumba yake ya usuluhishi. Safari hii pia, Ibilisi hakufika licha ya uvumilivu wa kusubiri wa mtu ( mzee ) yule.

Aliporudi nyumbani siku ile alijihisi amechoka sana  kwa sababu ya kutokupata usingizi mzuri kutokana na majukumu yake na purukushani za Ibilisi.  Hivyo akawataka wanafamilia yake kutomrushu mtu yoyote kuingia hadi atakapoamka.
Ibilisi alirudi tena na kutaka kumjaribu mtu yule, alifika nyumbani kwake na kuanza kupiga hodi kwa fujo. Wanafamilia walimzuia na kutotaka kumfungulia mlango. Wakati huu Ibilisi alikuwa amedhamiria haswa, hivyo akatafuta mbinu nyingine ya kuingia ndani na hatimae akafanikiwa.

Baada ya Ibilisi kuingia ndani, mtu yule aliangalia mlango wake ambao  ulikuwa umefungwa pasina dalili ya kufunguliwa na hapo akagundua yule hakuwa mzee bali Ibilisi. Mzee yule akamuuliza Ibilisi " Je, wewe ni adui wa Mungu?"
Alithibitisha kuwa yeye ni Iblis na akasema, “Umezima mipango yangu yote na kuharibu jitihada zangu zote za kukushawishi katika mpango wangu. Nia yangu ilikuwa kufanya ukasirike kwa namna yoyote, ili moja ya madai yako mbele ya Ilyaas iweze kuthibitishwa kuwa si ya kweli.”
Kutokana na tukio hili, mtu huyo alipewa jina la Dhul-Kifl, jina lenye maana ya "mmiliki wa, au kutoa, malipo mara mbili au sehemu".

KUTOKANA NA QUR'AN

Yawezekana Waislamu wengi hawatatoa jibu la haraka ukiwauliza Dhul-Kifli ni nani, na alitumwa kwa watu wa nchi gani? Huyu ni Nabii miongoni mwa Manabii 25 waliotajwa ndani ya Qur’an.

Dhul-Kifl au Zul-Kifl (c.600 BCE) ni Nabii ambaye ametambuliwa kama Ezekiel katika Biblia. Yasadikika kuwa Nabii huyu aliishi miaka 75, na nchi aliyoifikishia Ujumbe wa dini ya Mwenyezi Mungu ni ile ambayo leo hii inaitwa Iraq.

Ni Nabii aliyepewa daraja kubwa katika maisha haya na anatajwa katika Qur’an kama mtu wa kundi la watu wema. Japo hakuna mengi yanayofahamika kuhusu Dhul-Kifli kutoka vyanzo vingine vya historia, maandiko yote kutoka kwa mufasirina mashuhuri kama Ibn Ishaq na Ibn Kathiir yanamzungumzia Dhul-Kifli kama nabii na mtu mwema ambaye alidumu katika Swala za kila siku na ibada nyingine.

Dhul-Kifl ndani ya Qur'an

Dhul-Kifl ametajwa mara mbili katika aya zifuatazo za Qur’an:

Na (mtaje) Ismail, na Idrisi, na Dhul-Kifli, wote walikuwa miongoni mwa wanaosubiri. Na Tukawaingiza katika rehema Yetu. Hakika wao walikuwa katika watu wema.” (21:85-86).

Na Mkumbuke Ismaili na Alyasa’a na Dhul-Kifli; na hao wote walikuwa ni miongoni mwa watu bora.” (38:48)

Katika Aya zote mbili, Dhul-Kifli anajumuishwa katika orodha ya Manabii.

Historia

Jina Dhul-Kifli, kiistilahi, lina maana ya “mzee wa mkupuo”, hii ni aina ya majina inayoanza na “Dhu” (mmiliki wa) ambayo hutangulia jina fulani. Majina ya aina hii yametumika katika Qur’an kutaja watu wengine mashuhuri.

Mathalani, Dhu’l-Nun, “mtu (mzee) wa samaki” yaani Nabii Yunus na wengineo. 

Mtume Dhul-kifl ananasibishwa na Ezekiel anayetajwa ndani ya Biblia. Ni miongoni mwa Mitume waliopata mateso sana mikononi mwa Bani Israil. Hata hivyo hakuacha kufundisha Ujumbe wa Allah.  Tunamsoma Dhul-kifl katika aya zifuatazo: 

Na (mtaje) Ismail na Idris na Dhul-kifl – wote walikuwa miongoni mwa wanaosubiri. Na tukawaingiza katika rehema yetu. Hakika wao walikuwa katika watu wema” (21:85-86). 

“Na mkumbuke Ismail na  Alyasaa na Dhul-kifl, na hao wote walikuwa miongoni mwa watu bora” (38:48). 

Mtume Dhul-kifl anatajwa kwa wema wake katika kuufuata mwongozo wa  Allah(s.w). Na Mwenyezi Mungu anaahidi kuwa marejeo ya watu wema ni mahali pazuri kabisa. 

Huu ni ukumbusho (wa watu wema). Na kwa yakini wamchao Mungu mahali pao pa kurudia patakuwa pazuri kabisa” (38:49).

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA NABII SULEIMAAN

The Story of Prophet Dhul Kifl

Full Story of the Prophet Ayyub