Yanayobatilisha na yasiyo batilisha swaum

Yanayobatilisha na yasiyo batilisha swaum



1-At-Tahaamiyl: (Suppository) Dawa Za Kuteremsha Homa Zinazowekwa Kwa Njia Ya Utupu Wa Nyuma

Hukmu Yake: Haibatilishi.

[Imaam ibn ‘Uthaymiyn]

2-Dawa Ya Macho Ya Maji (Eye Drops)

 Hukmu Yake: Haibatilishi. Lakini atakapohisi ladha ya hiyo dawa kwenye koo lake, basi kiakiba akilipa hiyo siku ni bora. [Imaam Ibn ‘Uthaymiyn]

 3-Wanja Wa Macho

Hukmu Yake: Haibatilishi na lakini ni bora atumie usiku baada ya kufuturu.  [Ibn ‘Uthaymiyn, Ibn Baaz]

 4-Dawa Ya Kudondoshea Masikioni

Hukmu Yake: Haibatilishi. [Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]

 5-Kipulizo Cha Pumu.

Hukmu Yake:  Haibatilishi. [Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn, Al-Lajnah Ad-Daaimah]

6-Kipulizo; Mashine Ya Kuvuta Hewa (Oxygen)

Hukmu Yake: Haibatilishi kwa kuhitajika kwa dharura.
[Ibn ‘Uthaymiyn]

 7-Sindano Ya Penicillin
Hukmu Yake: Haibatilishi. [Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
 
8-Sindano Ya Insoline Kwa Mgonjwa Wa Kisukari

Hukmu Yake:  Haibatilishi.  [Ibn ‘Uthaymiyn, Ibn Baaz]

9-Sindano Ya Ganzi Kwa Ajili Ya Kung’olewa Jino Na Kuweka Mjazo Wa Meno Na Kusafishwa Meno.
Hukmu Yake: Haibatilishi. Lakini atahadhari kumeza chochote katika dawa na damu (kwa maana akimeza atabatilisha Swawm). [Ibn Baaz]

10-Kutumia Manukato Mazuri Na Kuyanusa

 Hukmu Yake: Haibatilishi. [Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]

 11-Kunusa Harufu Ya Udi Uliofukizwa

 Hukmu Yake: Haibatilishi.  [Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]

12-Dawa Ya Kulainisha Mdomo (Lip Balm)

Hukmu Yake: Haibatilishi, kwa sharti kwamba asimeze kitu. [Ibn ‘Uthaymiyn]

13-Vipodozi (Make Up)

Hukmu Yake: Haibatilishi. [Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]

Tanbihi: Mwanamke hapaswi kujipamba kudhihirisha mapambo yake kwa wanaume ajnabiy wasio mahaarim wake.

 14- Kuvuja Damu Pua Na Kun’goa Jino Huku Damu Ikitoka

Hukmu Yake: Haibatilishi. [Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
 
15-Kutolewa Damu Kwa Ajili Ya Kipimo

Hukmu Yake: Haibatilishi. [Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
 
16-Kuota Kitendo Cha Ndoa Na Kutokwa Manii

 Hukmu Yake: Haibatilishi [Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]

 17-Kutokwa Na Madhii. (Madhii Ni Maji Mepesi Mno Yenye Kunatanata Yanayotoka Wakati Wa Matamanio Ya Kimwili)

Hukmu Yake: Haibatilishi [Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]

18-Kuogelea Na Kupiga Mbizi

Hukmu Yake: Haibatilishi. [Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
 
19-Dawa Ya Kusukutua

Hukmu Yake: Haibatilishi kwa sharti kuwa asimeze kitu.  [Ibn ‘Uthaymiyn]

 20-Kutumia Mswaki

Hukmu Yake: Haibatilishi. [Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn] Lakini ni mswaki wa kawaida na si ambao una ladha.

21-Dawa Ya Kusafisha Meno

 Hukmu Yake: Haibatilishi ikiwa haitomezwa ikaingia tumboni. Na lililo salama zaidi ni kutokuitumia kwa sababu ina nguvu kali. [Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]

 22-Kumeza Makohozi

Hukmu Yake: Haibatilishi ikiwa haitofikia mdomoni. Ama ikifikia mdomoni akameza, basi inabatilisha Swawm. [Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]

 23-Kuonja Chakula

Hukmu Yake: Haibatilishi lakini bila ya kumeza na wala asifanye mtu isipokuwa kwa dharura.  [Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]

24-Vidonge Vinavyoweka Chini Ya Ulimi Kwa Kutibu Maradhi Ya Moyo

Hukmu Yake: Haibatilishi ikiwa havitoyeyuka na kumezwa mate yake ambayo yameyeyuka ndani ya mdomo. Hakika vinabatilisha Swawm. Lakini vikiwa haviyeyuki na havimezwi, basi havina madhara. [Ibn ‘Uthaymiyn]

 25-Dawa Ya Kudondoshea Puani

Hukmu Yake: Inabatilisha ikifikia tumboni [akimeza]. [Ibn ‘Uthaymiyn]

Dawa ya pua haifai kwa mwenye Swawm na atakayetia ikafikia kooni akasikia ladha yake, basi alipe Swawm yake.

26-Viraka Vya Nikotini (Vya Kubandika Mikononi Au Mabegani Kusaidia Wavutaji Sigara Waache Uvutaji)

 Hukmu Yake: Inabatilisha. [Al-Lajnah Ad-Daaimah]

27-Hijaamah (Kupigwa Chuku, Kuumikwa)

Hukmu Yake: Inabatilisha.

(Lakini Wanachuoni wengine wanaonelea ikiwa haitomdhoofisha anayefanyiwa Hijaamah, basi haibatilishi).  [Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]

28-Kuchangia Damu
Hukmu Yake: Inabatilisha ikiwa ni nyingi (na kumdhoofisha mtoaji damu) kama vile kiasi cha damu ya Hijaamah. [Ibn ‘Uthaymiyn]

29-Damu Inayotoka Katika Kidonda

Hukmu Yake: Inabatilisha ikiwa si kwa khiari yake kama vile kutolewa damu nyingi kwenye mishipa kwa ajili ya vipimo, lakini ikiwa ni kwa dharura bila ya khiari yake basi haibatilishi.

30-Kutapika Kwa Makusudi

 Hukmu Yake: Inabatilisha ikiwa kwa makusudi. Ikiwa si makusudi haibatilishi. [Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]

31-Sindano Ya Kuingiza Chakula Kupitia Maji Mwilini Kumtia Mtu Nguvu

Hukmu Yake: Inabatilisha. Ama sindano ya misuli au ya mishipa au ya ngozi haibatilishi. Na ni salama zaidi kufanya usiku baada ya kufuturu. [Ibn ‘Uthaymin, Ibn Baaz]

32-Kuvuta Harufu Ya Moshi Wa Udi

Hukmu Yake: Inabatilisha ikiwa anajua, ama ikiwa kunusa tu haibatilishi. [Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]

34-Kudungwa Sindano

Hukmu Yake: Haibatilishi. Ama ikiwa ni kwa ajili ya kuingiza chakula au nguvu ya chakula (kama glucose) inabatilisha. Na usalama zaidi kutumia usiku [baada ya kufuturu]. [Ibn Baaz]

35-Kupaka Hinna
Hukmu Yake: Haibatilishi. [Ibn ‘Uthaymiyn]

36-Kula Au Kunywa Kwa Kusahau

Hukmu Yake: Haibatilishi, lakini mtu anapokumbuka tu aachilie mbali hata kama kimo mdomoni akiteme. [Ibn ‘Uthayimyn].

37-Kuvuta Sigara

Hukmu Yake: Inabatilisha na ni haramu wakati wowote katika Ramadhwaan na nje ya Ramadhwaan. [‘Ibn ‘Uthaymiyn]

38-Kuoga
Hukmu Yake: Haibatilishi. [Ibn ‘Uthaymiyn]

 39-Kumeza Chakula Kilichokuja Kwa Kucheua

Hukmu Yake: Inabatilisha ikiwa chakula au maji aliyocheua yatafika mdomoni akameza, ama ikiwa yameishia kooni basi hana juu yake chochote [Ibn ‘Uthaymiyn]

 40-Kusafishwa Damu Ya Mafigo (Dialysis)

Hukmu Yake: Inabatilisha na inampasa alipe Swawm yake. [Ibn Baaz]

41-Maongezi Maovu Ya Haramu

Hukmu Yake:  Hayabatilishi lakini thawabu zitapunguka  na kama yanahusiana na haki ya mtu (Kumtusi mtu), basi itampotezea kabisa thawabu za Swawm. [Ibn Baaz]

 42-Kumeza Mate

Hukmu Yake: Haibatilishi. [Ibn Baaz]
 
43-Kumeza Maji Wakati Wa Wudhuu

Hukmu Yake: Haibatilishi ikiwa si kwa kukusudia. [Al-Lajnah Ad-Daaimah]

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA NABII SULEIMAAN

The Story of Prophet Dhul Kifl

Full Story of the Prophet Ayyub