Hadithi dhaifu ( Zisizo sahihi) kuhusu swaumu na ramadhani - Sehemu ya kwanza
01
.لا تقولوا رمضان، فإن رمضان اسم من أسماء الله تعالى، ولكن قو. شهر رمضان والحديث موضوع ترتيب الموضوعات " للذهبي، " الفوائد المجموعة“ للشوكاني
“Msiuite mwezi kwa jina la Ramadhwaan; kwani Ramadhwaan ni jina katika Majina ya Allaah, lakini semeni mwezi wa Ramadhwaan.”
Hadiyth hii ni Hadiyth Mawdhwuw’ (ya kutungwa) amezuliwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) imetajwa kwenye kitabu cha Imaam Adh-Dhahabiy cha Hadiyth za kutungwa na kwenye kitabu cha Ash-Shawkaaniy pia kiitwacho Al-Fawaaid.
02
أول شهر رمضان رحمة، وأوسطه مغفرة، وأخره عتق من النار ضعيف أشار ابن خزيمة إلى تضعيفه، وقال الشيخ الألباني: إنه حديث منكر.
“Mwanzo wa mwezi wa Ramadhwaan ni rahmah, na katikati yake ni maghfirah, na mwisho wake ni kutolewa kwenye Moto.”
Ni Hadiyth Dhwa’iyf; Ibn Khuzaymah ameashiria kuwa ni Hadiyth Dhwa’iyf, na Shaykh Al-Albaaniy amesema ni Hadiyth Munkar.
03:
صوموا تصحواوهو حديث ضعيف ، وإن كان معناه صحيحاً ، وقد ذكره الشيخ الألباني في "ضعيف الجامع الصغير".
“Fungeni mtapata siha (afya).”
Ni Hadiyth dhaifu japokuwa maana yake sahihi; ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kwenye kitabu cha Dhwa’iyf Al-Jaami’ Asw-Swaghiyr.
04
لا تزال أمتي بخير ما أخَّروا السحور وعجَّلوا الفطر رواه أحمد والحديث منكر كما قال الشيخ الألباني،
Ummah wangu utaendelea kuwa katika khayr madhali wanachelewesha Suhuwr (kula daku) na wanaharakisha kufuturu.” [Ameipokea Ahmad na Hadiyth ni Munkar kama alivyosema Shaykh Al-Albaaniy]
Hadiyth iliyo sahihi kuhusu hilo, ni Hadiyth:
“Watu wataendelea kuwa katika khayr madhali watakuwa wanaharakisha kufutari.” [Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim]
05
"رجب شهر الله، وشعبان شهري، ورمضان شهر أمتي" ضعيف ، نص الشيخ الألباني على تضعيفه في السلسلة الضعيفة
“Rajab ni mwezi wa Allaah, na Sha’abaan ni mwezi wangu, na Ramadhwaan ni mwezi wa ummah wangu.”
Hadiyth Dhwa’iyf, ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kwenye Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah.
06.
لو يعلم العباد ما في رمضان لتمنت أمتي أن تكون السنة كلها رمضان... موضوع (يعني مكذوب على النبي صلى الله عليه وسلم) قال بذلك ابن الجوزي والألباني وغيرهما. وقال ابن حجر عنه: ضعيف جدا.
“Lau wangeelewa waja yaliyomo katika Ramadhwaan, ummah wangu ungalitamani iwe Ramadhwaan mwaka mzima...”
Ni Hadiyth Mawdhwuw’ (yaani amezuliwa uongo Rasuli wa Allaah Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema hivyo Ibn Al-Jawzy na Al-Albaaniy na wengineo, na amesema Ibn Hajar kuwa ni Hadiyth dhaifu sana.
07
اللهم بارك لنا في رجب وشعبان وبلغنا رمضان وقد ضعّفه الألباني في "ضعيف الجامع الصغير
“Ee Rabb Tubarikie katika Rajab na Sha’abaan na Tubalighishe Ramadhwaan.”
Ni Hadiyth Dhwa’iyf ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kwenye kitabu cha Dhwa’iyf Al-Jaami’ Asw-Swaghiyr.
08.
شعبان شهري، ورمضان شهر الله، وشعبان المطهر، ورمضان المكفر ضعّفه الألباني في السلسلة الضعيفة.
“Sha’abaan ni mwezi wangu, na Ramadhwaan ni mwezi wa Allaah, na Sha’abaan inatwahirisha, na Ramadhwaan inafuta (madhambi).”
Ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kuwa ni dhaifu kwenye Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah.
والصحيح من ذلك حديث: لَا يَزَالُ النَّاسُ بِخَيْرٍ مَا عَجَّلُوا الْفِطْرَ
09.
خمس يفطِّرن الصائم وينقضن الوضوء: الكذب، والنميمة، والغيبة، والنظر بشهوة، واليمين الكاذبة موضوع. قال ابن أبي حاتم : سألت أبي عن هذا الحديث فقال: هذا حديثُ كَذِبٍ، وقال بوضعه الشيخ الألباني في ضعيف الجامع وليس معنى هذا التساهل في هذه المحرمات ، فإنها تفطر الصائم وتوجب القضاء عند ابن حزم والإمام الأوزاعي (خلافا لجمهور أهل العلم)، وتنقص الأجر بل ربما نسفته عند بقية الأئمة، ولكن المقصود أن نسبة هذا اللفظ إلى النبي صلى الله عليه وسلم لا تجوز.
“Mambo matano yanamfunguza mwenye swawm na yanabatilisha wudhuu: Kusema uongo, kufitinisha, kusengenya, kutazama kwa matamanio, kula yamini ya uongo.”
Ni Hadiyth Mawdhwuw’.
10.
نوم الصائم عبادة" ضعيف، نص على تضعيفه الألباني في السلسلة الضعيفة
“Usingizi wa mwenye Swawm ni ‘ibaadah.”
Ni Hadiyth Dhwa’iyf, amesema hivyo Shaykh Al-Albaaniy kwenye Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah.
11.
نوم الصائم عبادة، وصمته تسبيح، وعمله مضاعف، ودعاؤه مستجاب، وذنبه مغفور وهو حديث ضعيف، ذكره الشيخ الألباني في "ضعيف الجامع الصغير".
“Usingizi wa mwenye mwenye swawm ni ‘ibaadah, na kunyamaza kwake kimya (kutokusema kwake) ni tasbiyh, na ‘amali yake ni yenye kuongezwa maradufu, na du’aa yake ni yenye kutakabaliwa, na dhambi zake ni zenye kughufuriwa.”
Ni Hadiyth Dhwa’iyf ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kwenye kitabu cha Dhwa’iyf Al-Jaami’ Asw-Swaghiyr.
12.
صائم رمضان في السفر كالمفطر في الحضر وهو حديث ضعيف، ذكره الشيخ الألباني في "ضعيف الجامع الصغير".
“Mwenye Swawm Ramadhwaan kwenye safari ni sawa asiyefunga hali akiwa mkaazi.”
Ni Hadiyth Dhwa’iyf ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kwenye kitabu cha Dhwa’iyful Jaami’ Asw Swaghiyr.
13.
يوم صومكم يوم نحركم قال عنه السيوطي في الآلئ : كذب ، لا أصل له. وسبقه إلى ذلك الإمام أحمد بن حنبل كما نقل السخاوي في المقاصد.
“Siku ya Swawm yenu (kufunga kwenu) siku ya kuchinja kwenu.”
Amesema Imaam As-Suyuutwiy: Hadiyth hii haina asli, na alimtangulia kwa hayo Imaam Ahmad bin Hanbal kama alivyonukuu As-Sakhaawiy kwenye Al-Maqaaswid.
14.
من أدرك رمضان وعليه من رمضان شيء لم يقضه، فإنه لا يقبل منه حتى يصومه ذكره الشيخ الألباني في "ضعيف الجامع الصغير".
“Mwenye kukutana na Ramadhwaan huku akiwa ana deni la Ramadhwaan hakulilipa, basi haitokubaliwa Swawm yake mpaka alipe ile anayodaiwa.”
Ni Hadiyth Dhwa’iyf ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kwenye kitabu cha Dhwa’iyf Al-Jaami’ Asw-Swaghiyr.
15.
"يا أيها الناس قد أظلكم شهر عظيم ، شهر فيه ليلة خير من ألف شهر ، جعل الله صيامه فريضة ، وقيام ليله تطوعا ، من تقرب فيه بخصلة من الخير كان كمن أدى فريضة فيما سواه ، ومن أدى فيه فريضة كان كمن أدى سبعين فريضة فيما سواه ، وهو شهر الصبر ، والصبر ثوابه الجنة ، وشهر المواساة ، وشهر يزاد فيه في رزق المؤمن ، ومن فطر فيه صائما كان مغفرة لذنوبه وعتق رقبته من النار ، وكان له مثل أجره من غير أن ينتقص من أجره شيء . قالوا : يا رسول الله ، ليس كلنا يجد ما يفطر الصائم ، قال : يعطي الله هذا الثواب من فطر صائما على مذقة لبن ، أو تمرة ، أو شربة من ماء ، ومن أشبع صائما سقاه الله من الحوض شربة لا يظمأ حتى يدخل الجنة ، وهو شهر أوله رحمة ، ووسطه مغفرة ، وآخره عتق من النار ، فاستكثروا فيه من أربع خصال ، خصلتان ترضون بهما ربكم ، وخصلتان لا غنى بكم عنهما ، أما الخصلتان اللتان ترضون بهما ربكم فشهادة أن لا إله إلا الله ، وتستغفرونه ، وأما الخصلتان اللتان لا غنى بكم عنهما ، فتسألون الجنة ، وتعوذون من النار". وهو حديث ضعيف لا تقوم به حجة. رواه البيهقي ، وضعفه الألباني في "المشكاة"، وقال: منكر في " السلسلة الضعيفة"
Alitukhutubia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika siku ya mwisho ya mwezi wa Sha’abaan; akasema: "Enyi watu! Umekufikieni mwezi ‘adhimu – na kuna riwaayah nyingine ambayo pia ni ya kutungwa kumeengezwa ‘wenye baraka’ mwezi ndani yake kuna usiku ambao ni bora kuliko miezi elfu; Allaah Amejaalia Swawm yake mwezi huu kuwa ni fardhi (wajibu), na kisimamo (qiyaam) chake cha usiku wake ni tatwawwu’u (kujitolea): sio fardhi wala sio wajibu, atakayejikurubisha ndani yake ndani ya mwezi huu kwa jambo lolote lile la khayr, basi jazaa yakehuwa kama mtu aliyetekeleza fardhi katika mwezi mingine usiokuwa huu, na atakayetekeleza fardhi ndani yake ndani ya mwezi huu, basi jazaa yake huwa kama mtu aliyetekeleza fardhi sabini (70) katika mwezi mingine usiokuwa huu, nao ni mwezi wa Swabr (subira), na subira thawabu yake ni Jannah, na ni mwezi ambao ndani yake riziki ya Muumini huzidishwa, na yeyote yule atakayemfuturisha mwenye swawm ndani yake, basi jazaa yake itakuwa ni maghfirah ya madhambi yake, na kuachwa huru shingo yake na Moto, na atapata ujira kama aupatao mwenye swawm bila ya kupungua chochote katika ujira wake mwenye swawm.” Tukasema: Ee Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), sio sote tunaweza kupata cha kumfuturisha huyo mwenye swawm; Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawajibu: "Allaah Humpa thawabu hizi yule atakayemfuturisha mwenye swawm kwa funda la maziwa au kwa kokwa ya tende au kwa funda la maji; na atakayemshibisha mwenye swawm basi Allaah Atamnywesha katika hodhi funda ambalo hatopata kiu baada yake mpaka aingie Jannah; nao ni mwezi ambao mwanzo wake ni rahmah, na katikati yake ni maghfirah, na mwisho wake ni kuachwa huru kutokana na Moto. Na kuna riwaayah nyingine ambayo pia ni ya kutungwa kumeengezwa na atakayempunguzia kazi mtumishi mfanyakazi wake ndani ya mwezi huu, Allaah Atamghufuria madhambi yake na kumuacha huru na Moto; basi kithirisheni sana ndani yake mambo manne, mtamridhisha Rabb wenu kwayo na mawili mengine hamjikwasi hamna budi nayo; ama yale mawili ambayo mtakayoridhisha nayo Rabb wenu ni shahaadah (kushuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah) na mumtake maghfirah, na ama yale mawili mengine ambayo hamna budi nayo ni kuomba Jannah na kujilinda kujikinga kwake na adhabu ya Moto."
Hadiyth hii ni Dhwa’iyf haiwezi kuwa hoja wala dalili. Ameipokea Al-Bayhaqiyy na akaidhoofisha kwa kusema Dhwa’iyf Shaykh Al-Albaaniy kwenye Al-Mishkaat na akasema ni Hadiyth Munkar kwenye Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah.
16.
أن امرأتين صامتا وأن رجلاً قال: يا رسول الله إن هاهنا امرأتين قد صامتا وإنهما قد كادتا أن تموتا من العطش فأعرض عنه أو سكت ثم عاد وأراه قال بالهاجرة قال يا نبي الله إنهما والله قد ماتتا أو كادتا أن تموتا قال ادعهما قال فجاءتا قال فجيء بقدح أو عس فقال لإحداهما: قيئي فقاءت قيحاً أو دماً وصديداً ولحماً حتى قاءت نصف القدح ثم قال للأخرى: قيئي فقاءت من قيحٍ ودمٍ وصديدٍ ولحمٍ عبيطٍ وغيره
حتى ملأت القدح ثم قال إن هاتين صامتا عما أحل الله وأفطرتا على ما حرم الله عز وجل عليهما جلست إحداهما إلى الأخرى فجعلتا يأكلان لحوم الناس. الضعيفة"
“Wanawake wawili walifunga – katika uhai wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kwamba mtu alisema: Ee Rasuli wa Allaah! Hakika wanawake wawili hawa wamefunga na kwamba wao wawili walikaribia kufa kwa kiu; Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akampuuza au alinyamaza kimya; kisha – yule mtu akarejea… akasema: Ee Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)! Hakika wawili hao wamekwisha kufa au wanakaribia kufa – akitafuta wapewe rukhsa ya kufungua kwa hali yao mbaya; Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Waiteni. Akasema: Wakaja wote wawili; akasema: kikaletwa chombo na akaambiwa mmoja wao: Tapika ndani yake yale mliyokuwa mkila. Basi alitapika matapishi au damu na usaha na nyama, alitapika mpaka kile chombo kikajaa nusu yake, na kisha akamwambia yule mwengine wa pili wao: Tapika, basi na yeye alitapika matapishi na damu na usaha na nyama na mengineo mpaka chombo kikajaa, kisha – Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Hakika wanawake wawili hawa walifunga kwa kujizuilia kutokula kutokana na yale Aliyoyahalalisha Allaah, na wakafungua Swawm zao kutokana na yale Aliyowaharamishia Allaah, alikaa mmoja wa wawili hawa kwa mwenzake wakawa wanakula nyama za watu (wanasengenya).”
Ni Hadiyth Dhwa’iyf
17.
أعطيت أمتي في شهر رمضان خمسا لم يعطهن نبي قبلي أما واحدة ؛ فإنه إذا كان أول ليلة من شهر رمضان ينظر الله
عز وجل إليهم، ومن نظر الله إليه لم يعذبه وأما الثانية ؛ فإن خلوف أفواههم حين يمسون أطيب عند الله من ريح المسك وأما الثالثة ؛ فإن الملائكة تستغفر لهم في كل يوم وليلة وأما الرابعة فإن الله عز وجل يأمر جنته فيقول لها: استعدي وتزيني لعبادي، أوشك أن يستريحوا من تعب الدنيا إلى داري وكرامتي وأما الخامسة ؛ فإنه إذا كان آخر ليلة غفر الله لهم جميعا
فقال رجل من القوم: أهي ليلة القدر؟ فقال: لا، ألم تر إلى العمال يعملون،
فإذا فرغوا من أعمالهم وفوا أجورهم " وفي لفظ (تستغفر لهم الحيتان
ذكره العلامة الألباني في سلسلته الضعيفة وقال في المشكاة فيه هشام ابن أبي هشام ضعيف إتفاقا وهو متروك
“Ummah wangu umepewa mambo matano kwenye Ramadhwaan hajapewa Nabiy yeyoye yule kabla yangu; Jambo la kwanza, Unapokuwa usiku wa kwanza kwenye mwezi wa Ramadhwaan Allaah Huwatazama ummah wangu na anayetazamwa na Allaah Hatomuadhibu.
Jambo la pili, harufu ya vinywa vyao inapendeza zaidi kwa Allaah kuliko harufu ya miski.
Jambo la tatu, Malaika wanawaombea maghfirah kila siku mchana na usiku.
Jambo la nne, Allaah Huamrisha Jannah Yake kwa kuiambia: Jiandae na jipambe kwa ajili ya waja Wangu, karibu watapumzika kutokana na taabu za dunia na kwenda kwenye Nyumba Yangu na kwenye Karama (utukufu) Yangu.
Jambo la tano, na inapokuwa mwisho wa usiku Allaah Huwaghufuria wote. Akauliza mtu: je, huu ndio usiku wa Laylatul Qadr? – Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Sio; je, huoni kuwa wafanyakazi hufanya kazi na wanapomaliza kazi yao hulipwa ujira wao. Na katika riwaayah: Samaki huwaombea maghfirah.”
Ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kuwa ni Dhwa’iyf kwenye Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah na pia akasema kwenye Al-Mishkaat kuwa ndani yake yuko Hishaam bin Abi Hishaam ambaye ni Dhwa’iyf kwa maafikiano na ni Matruwk (aliyeachwa Hadiyth zake).
18.
إذا كان أول ليلة من شهر رمضان نظر الله عز وجل إلى خلقه، وإذا نظر الله عز وجل إلى عبده لم يعذبه أبدا، ولله عز وجل فى كل ليلة ألف ألف عتيق من النار
موضوع (يعني مكذوب على النبي صلى الله عليه وسلم) قال بذلك ابن الجوزي، والألباني في السلسلة الضعيفة
“Inapokuwa usiku wa mwanzo wa mwezi wa Ramadhwaan Allaah Huwatazama viumbe Wake, na Allaah Anapomtazama mja Wake Hatomuadhibu abadan; na Allaah Huwatoa Motoni katika kila usiku elfu elfu.”
Ni Hadiyth Mawdhwuw’ ya kutungwa amezuliwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema hivyo Ibn Al-Jawziy na Al-Albaaniy katika Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah.
Atakupokeeni na nyinyi mtampokea” mara tatu, ‘Umar bin Al-Khattwaab akasema: Ee Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)! Ni Wahyi umeteremshwa? Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Sio. ‘Umar bin Al-Khattwaab akasema: Je, ni adui amehudhuria? Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Sio. ‘Umar bin Al-Khattwaab akasema: Basi nini? Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Hakika Allaah Anawaghufuria katika usiku wa mwanzo wa Ramadhwaan kwa kila mmoja wa katika kabila hili.”
Ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kuwa ni Munkar kwenye Dhwa’iyf At-Targhiyb wat-Tarhiyb.
20.
إن للصائم عند فطره دعوة لا ترد ضعيف ، أشار إلى ضعفه ابن القيم في زاد المعاد، ونص على تضعيفه الشيخ الألباني في تمام المنة وغيره، وفي الصحيح غنية، فقد صح أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال :( ثلاثة لا ترد دعوتهم: الصائم حتى يفطر والإمام العادل ودعوة المظلوم) صححه الألباني في السلسلة الصحيحة ، وشتان بين اللفظين.
“Hakika kwa mwenye Swawm wakati wa kufutari du’aa hairejeshwi (haikataliwi).”
Ni Hadiyth Dhwa’iyf, ameashiria hayo Ibn Al-Qayyim kwenye Zaad Al-Ma’aad na pia Shaykh Al-Albaaniy kwenye Tamaam Al-Minnah na na kwengineko, na katika Sahihi kuna zenye kutosheleza, imethibiti kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“(Watu) watatu du'aa zao hazirudi: Mwenye Swawm hadi afuturu (afutari), Kiongozi muadilifu na du’aa ya aliyedhulumiwa…” [At-Tirmidhiy]
Amesema Al-Albaaniy ni Hadiyth Sahihi kwenye Silsilat Al-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah, umbali ulioje baina ya lafdhi mbili hizi.

Comments
Post a Comment