Umuhimu wa Dua - Kuomba na kuombeana
Assalam Alykum Warahmatullah Wabarakat
Awali ya yote hatuna budi tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia kuwa hai katika muda huu na kwa kutujaalia kuwa na afya kwa kiasi hiki, hakika hii tuliyonayo ni neema kubwa sana.
Niingie katika mada yangu niliyoikusudia kukufikishia leo Msomaji wangu Mpendwa kama kilivyo kichwa cha habari hapo juu.
Mtume Muhammad Swalla llaahu alayhi wasallam anasema
وعن النعمان بن بشير رضي الله عنهما عن النبي صلى الله عليه وسلم قال:
"الدعاء هو العبادة".
"Dua ni Ibada"
Hapa tunajifunza kuwa kufanya maombi ni ibada maana yake tukimuomba Mwenyezi Mungu tunakuwa tunamuabudu na tunapata thawabu kutokana na kitendo hicho, hivyo tukiomba kiumbe {kama vile mzimu,shetani,kaburi n.k} badala ya Kumuomba Muumbaji inakuwa shirki na anayefanya hivyo anapata dhambi.
Ieleweke kuwa dua inaweza kuwa ni kumuomba Allah akupe jambo au kitu fulani au akulinde dhidi ya kitu, Mtu, au kiumbe fulani.
KUJIBIWA DUA.
Ndugu Zangu hatukuamrishwa kumuomba Allah tu bali Allah ametuahidi kutujibu Maombi yetu kama alivyosema kwenye kitabu chake cha Qur-an
أُجِيبُ دَعۡوَةَ ٱلدَّاعِ إِذَا دَعَانِۖ
"...Ninajibu Maombi Ya Muombaji Anaponiomba"
hii ni ahadi ya Allah ambayo ni ya uhakika kuwa anayemuomba atarajie kupata majibu ya maombi yake.
KUMUOMBEA ALIYE MBALI.
Na katika hili la kumuombea dua aliyembali Kuna wasomaji wangu kutoka nchi mbalimbali wamekuwa wakiniuliza kama kuna uwezekano wa kuwaombea dua za kuondoa shida zao mbali mbali nimekuwa niwaelimisha kuwa inawezekana na
Alhamdulillah wengi wao wameelewa.
Mtume swalla llaahu alayhi wasallam amesema:-
وعنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم كان يقول: "دعوة المرء المسلم لأخيه بظهر الغيب مستجابة، عند رأسه ملك موكل كلما دعا لأخيه بخير قال الملك الموكل به: آمين، ولك بمثل" ((رواه مسلم)).
"Dua ya Muislam kwa ndugu yake aliyembali inajibiwa....."
Ndugu zangu ninawausia na kuwahimiza juu ya kuombeana dua kwa shida zetu mbalimbali na pia tujue kuwa wakati tunawaombea wenzetu na sisi pia tunaombewa na Malaika
Kuna faida nyingi za kuombeana miongoni mwazo ni kuimarisha udugu na upendo miongoni mwetu.

Comments
Post a Comment