Swalah Na Du’aa Zipi Za Kusoma Unapotaka Kutubu?



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. 

Hakika bin adam ni mwenye kukosa, na hakika bin adam mwenye aqil ni yule anapoona amekosa basi anamrudia Mola wake na kumuomba Maghfirah. Ikiwa ni miongoni mwa hao basi hilo linalokupasa  kumshukuru Allaah (Subhaanahu Wa Ta'alaa) kwa Kukuzindua ukatambua kuwa uko makosani kabla ya adhabu Yake au mauti kukufika. Yote hayo ni neema kutoka kwa Mola wako unapasa umshukuru sana kila wakati. 

Kuomba Maghfirah unaweza kuswali Rakaa mbili tu kwa nia moyoni ya kuomba Tawbah kwa Mola wako kama utakavyoona dalili katika mada za Tawbah tunazokuwekea viungo vyake chini. 

Ama du’aa, ziko mbali mbali ambazo hata Mitume waliomba walipokuwa wakifanya makosa au katika kawaida ya kumdhukuru Allaah, pamoja na adhkaar mbali mbali alizotufunza Mtume (Swallah Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)

Du’aa ifuatayo ambayo inaitwa ‘Sayyidul-Istighfaar’ (Bwana wa Kuomba Maghfirah) inapasa uisome kila mara na katika usimulizi Swahiyh ni kwamba pindi ukiisoma asubuhi ikawa ni ajali yako kuondoka duniani basi utaingia Peponi. Na pindi ukiisoma jioni ikawa usiku huo ni siku ya kuondoka duniani basi utaingia Peponi. Hivyo inampasa kila Muislamu awe anaidumisha du’aa hii kila siku asubuhi na jioni:

اللّهـمَّ أَنْتَ رَبِّـي لا إلهَ إلاّ أَنْتَ ، خَلَقْتَنـي وَأَنا عَبْـدُك ، وَأَنا عَلـى عَهْـدِكَ وَوَعْـدِكَ ما اسْتَـطَعْـت ، أَعـوذُبِكَ مِنْ شَـرِّ ما صَنَـعْت ، أَبـوءُ لَـكَ بِنِعْـمَتِـكَ  عَلَـيَّ وَأَبـوءُ بِذَنْـبي فَاغْفـِرْ لي فَإِنَّـهُ لا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْتَ .

Allaahumma Anta Rabiiy laa Ilaaha illa Anta Khalaqtaniy wa ana ‘Abduka wa ana ‘alaa ‘Ahdika  wa Wa’dika mastatwa’tu, A’uudhu Bika min sharri maa Swana’tu, abu-u Laka Bini’matika ‘alayya wa abu-u bidhanbiy, Faghfir-liy fainnahu laa yaghfirudh-dhunuuba illa Anta’

Ee Allaah! Wewe ni Mola wangu, hapana muabudiwa wa haki ila Wewe, Umeniumba mimi na mimi ni mja Wako, nami niko juu ya  ahadi Yako, na agano Lako, kiasi cha uwezo wangu, najilinda Kwako kutokana  na shari ya nilichokifanya, nakiri  Kwako kwa Kunineemesha, na nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba Unisamehe kwani hasamehe madhambi ila Wewe”

Zifuatazo pia ni du’aa chache kutoka katika Qur-aan ambazo tunazinukuu kwa wepesi wako, lakini ingia katika kiungo kifutacho utapata zaidi ya hizo:

 Du’aa aliyoomba baba yetu Aadam alipofanya makosa ya kumfuata ibliys.

رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ   

“Rabbanaa (Mola wetu)! Tumedhulumu nafsi zetu, na basi Usipotughufuria na Ukaturehemu; bila shaka tutakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”  [Al-A'araaf: 23]  


“(hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Utakasifu ni Wako, hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu).” [Al-Anbiyaa: 87]  

رَبَّنَا لاَ تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا رَبَّنَا وَلاَ تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا رَبَّنَا وَلاَ تُحَمِّلْنَا مَا لاَ طَاقَةَ لَنَا بِهِ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا أَنتَ مَوْلاَنَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ  (البقرة 286)

“Rabbanaa (Mola wetu) Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Rabbanaa (Mola wetu), Usitubebeshe mzigo kama Ulivyoubebesha juu ya wale waliokuwa kabla yetu. Rabbanaa (Mola wetu), Usitutwike tusiyoyaweza, na Tusamehe, na Tughufurie na Turehemu, Wewe ni Mawlaa (Mlezi, Mlinzi, Msimamizi) wetu, basi Tunusuru dhidi ya watu makafiri. [Al-Baqarah: 286]



 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA NABII SULEIMAAN

The Story of the Prophet Idris (AS)

The Story of Prophet Dhul Kifl