Imemjia Hedhi Dakika Tano Kabla Ya Magharibi, Akidhi Swalaah Ya Magharibi Baada Ya Kutoharika?





SWALI:

Nimefunga siku moja katika Ramadhwaan na haikubaki kitu siku hiyo isipokuwa dakika tano tu kufikia wakati wa kufuturu ikanijia hedhi ya mwezi. Je, ninawajibika kuswali Swalaah ya Magharibi kama kukidhi baada ya kutwaharika au la?

JIBU

Ikiwa hedhi imemjia kabla ya Magharibi kuingia basi haimuwajibikii kuswali Swalaah ya Magharibi wala Swalaah nyinginezo.

Na Swawm pia siku hiyo haitosihi, siku ambao imemjia hedhi kabla ya kuzama jua kwani swawm imebatilika na imemuwajibikia kulipa siku hiyo, ikiwa anajua kuwa imemjia hedhi kabla ya  Magharibi kuingia.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA NABII SULEIMAAN

The Story of Prophet Dhul Kifl

Full Story of the Prophet Ayyub