43-Kujua Fiqhi Ya Wanawake





 الإلمام بفقه النسا

Ni kitu kinachopendeza kwa mume kujua na kufahamu au hata kujifunza hukumu za ki-Fiqh zinazohusiana na wanawake, kwa khofu ya kutoangukia katika haramu, na amfundishe mkewe kama hafahamu hukumu za twahara na Swalah na hedhi…

Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

يا أيها الذين آمنوا قوا أنفسكم وأهليكم نارا وقودها الناس والحجارة


“ Enyi mlioamini! Jiokoeni Nafsi zenu na watu wenu, na moto ambao kuni zake ni watu na mawe…” (At-Tahrym: 6)

Na ikitokea mwanamke hafahamu hukumu hizi za ki-Fiqh, au mumewe hakuweza kumfundisha ni juu yake kuwauliza Ahlu-Dhikri (wenye ujuzi) katika mabaraza ya ki-elimu yanayo jihusisha na wanawake.

 Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) amesema:


نعم  نساء الأنصار لم يمنعهنّ الحياء أن يتفقّهن في الدّين

Wabora wa wanawake ni wanawake wa ki-Answaar ambao haikuwazuia haya katika kujifunza mambo ya Dini.” (Al-Bukhaariy na Muslim)

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA NABII SULEIMAAN

The Story of Prophet Dhul Kifl

Full Story of the Prophet Ayyub