26. Wajibu Wa Waliymah (Karamu)
Mume lazima afanye karamu baada ya kufunga ndoa. Hii ni kutokana na amri ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم aliyompa 'Abdur-Rahmaan ibn 'Awf afanye na pia kutokana na Hadiyth iliyosimuliwa na Buraydah ibn Hasiyb ambaye amesema:
لَمَّا خَطَبَ عَلِي فَاطِمَةُ رَضِيَ الله عَنْهُ قال: قال رَسُولُ الله صَلَّى الله عَلَيْهِ وَسَلَّمْ: (( إِنَّهُ لاَ بُدَّ لِلْعرْس مِنْ وَلِيمَة )) وَفِي رِوَايَة ((لِلْعَرُوس))
"'Aliy alipomposa Faatwimah alisema: Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema: ((Hapana budi iwepo karamu, hapana budi bwana harusi afanye karamu)). Msimuliaji amesema: Sa’ad akasema, mimi nitaleta kondoo, na mwingine akajitokeza akasema, mimi nitaleta kadha wa kadha katika mahindi. Katika Riwaaya nyingine ma-Answaar walikusanya mahindi mengi”[1]

Comments
Post a Comment