UTANGULIZI App hii ni muongozo mfupi wa kuufahamu Uislamu. Nayo ina Sura tatu. Sura ya kwanza, ‘‘ Baadhi ya vithibitisho juu ya ukweli wa Uislam ,’’ Sura hiyo inajibu baadhi ya maswali muhimu ambayo watu wanayauliza: Je ni kweli kwamba Qur’an ni maneno halisi ya Mungu, yaliyofunuliwa toka kwake ? Je ni kweli kuwa Muhammad S.A.W ni Mtume alietumwa na Mungu? Je ni kweli kuwa Uislamu ni Dini ya Mungu ? Katika sura hii, zimetajwa aina sita za ushahidi: Miujiza ya kisayansi ndani ya Qur’an tukufu: Sehemu hii inazungumzia (kwa picha) baadhi ya hakika (facts) za uvumbuzi wa kisasa wa kisayansi zilizotajwa katika Qur’an tukufu, ambayo ilikwishafunuliwa karne kumi na nne zilizopita. Changamoto Kuu ya Kuunda Sura Moja kama Sura za Qur’an Tukufu: Katika Qur’an, Mungu amewapa changamoto watu wote watunge sura moja iliyo kama sura za Qur’an. Tangu kufunuliwa kwa Qur’an, karne kumi na nne zilizopita, mpaka leo, hakuna mtu aliyeweza kuifikia changamoto hii, ingawa sura ndogo sana ...
Comments
Post a Comment