11 : Kukanusha Wale Wanaoigawa Bid’ah Kwenye Makundi Mawili: Bid’ah Nzuri Na Mbaya
Kukanusha Wale Wanaoigawa Bid’ah Kwenye Makundi Mawili: Bid’ah Nzuri Na Mbaya
Baadhi wanasema ya kuwa kuna bid’ah nzuri na kuna bid’ah mbaya.[1]
Sema, kama inakuridhisha, “Bidah nzuri na bid’ah mbovu, lakini kumbuka haya: Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema,
“Kwa uhakika kila bida’ni upotovu, na kila upotovu ni Motoni.”
Bid’ah zote; ziwe ni nzuri na au mbaya na zote unazoweza kutaja ziko chini ya “yote/kila”, ambayo ilitajwa na Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Ilisimuliwa ya kuwa Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisimulia,
“Kila bid’ah ni upotevu, hata kama baadhi ya watu watachukulia kuwa ni nzuri.”[2]
Mtu anaposema huu si wakati wa kukataza bid’ah bali ni bora kupiga vita madhehebu zinazokiuka maadili, hayuko sawa – kutokana na sababu zifuatazo:
1. Kwa kutokataza bid’ah, hawatoeneza tu bali wataziongeza, pamoja na hayo, Sunah nyingi (Sunan) zitafutwa. Hali hii itapelekea kuenea kwa upotofu na makosa, kwa sababu, lazima tukumbuke, kila bid’ah ni upotofu (dhwalaalah).
2. Kila Muislamu anawajibu, kama anaweza, kuzuia na kukataza maovu. Iwapo mtu ataona kitendo kiovu kinafanywa mbele ya macho yake, lazima akikataze, bila kujali udogo wake, ukilinganishwa na maovu makubwa yaliyoenea (yaliyo shamiri) – kama vile Ukomunisti, umasonia (Masonry), na itikadi zote potofu.
Vivyo hivyo, kuwepo kwa madhehebu zilizopotoka kusiwazuie Wanachuoni kuwakumbusha watu juu ya maonyo ya kutowaasi wazazi, kusema uongo, kula Ribaa na vitendo vyote viovu.
3. Ukosefu wa elimu katika jamii, pamoja na bid’ah kunasababisha na kueneza upotovu wa madhehebu. Lakini Maswahaba ambao walisimamisha jamii kinyume na ile tuliyoielezea, walikuwa baidi (mbali) na bid’ah, kwa hakika, walianzisha jamii safi, ambayo haikuwa na madhehebu zilizopotoka.[3]
4. Hebu tujaalie kuwa tunaelewa vema imani ya makundi mbali mbali yaliyoparaganyika - je, tutafanya nini baada ya hapo? Jibu, bila shaka, ni kuwa tuna haja ya kufafanua kukengeuka kwao, lakini inatubidi tuwe na maarifa, fiqh na mwongozo. Pamoja na hayo, elimu hiyo lazima iwe sahihi na halisi kwa sababu mihemko na ushupavu havitoshi kukanusha waliokengeuka na waliopotoshwa. Yule anayeifahamu Dini ana uwezo mzuri wa kuchanganua upotofu wa madhehebu zilizopotea, na ana uwezo wa kuwakusanya Waislamu kwa lile lililo sawa, katika Imani, Fiqh na mwenendo mzuri.

Comments
Post a Comment