Duo ya kuponya maumivu katika mwili
Imepokewa kutoka kwa Uthman Ibn Abi Al-'As: " Nililalamika kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu niliona maumivu niliyokuwa nayo katika mwili wangu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amkasema: “Weka mkono wako mahali unapohisi maumivu na useme: ‘Bismillah (Kwa Jina la Mwenyezi Mungu)’ mara tatu, kisha rudia mara saba: ‘A’udhu bi’izzatillahi wa qudratihi min sharri ma ajidu. wa 'uhadhiru (Najikinga kwa Mwenyezi Mungu na kwa Uweza Wake kutokana na shari inayonisibu na ninayoyashika). (Sahih Muslim)
Tunapoweka mkono wetu kwenye eneo la maumivu kwa nia ya kupata nafuu, soma yafuatayo:
بِسْمِ اللَّهِ x3
Bismillah
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu
أَعُوذُ بِعِزَّةِ اللَّهِ وَقُدْرَتِهِ مِنْ شَرِّ مَا أَجِدُ وَأُحَاذِرُ x7
'A'udhu bi'izzatillahi wa qudratihi min sharri ma ajidu wa 'uhadhiru.
Najikinga kwa Mwenyezi Mungu na kwa Uweza wake kutokana na shari inayonisibu na ninayo yashika.

Comments
Post a Comment