Dua ya Safari
Baada ya Swala yako ya Sunnah rakaa 2 kabla ya kuondoka au wakati wowote wa safari unapoelekea unakoenda, unaweza kusoma Dua ifuatayo:
اللَّهُمَّ إنَّا نَسْأَلُكَ في سَفَرِنَا هذا البِرَّ وَالتَّقْوَى، وَمِنَ العَمَلِ ما تَرْضَى، اللَّهُمَّ هَوِّنْ عَلَيْنَا سَفَرَنَا هذا، وَاطْوِ عَنَّا بُعْدَهُ، اللَّهُمَّ أَنْتَ الصَّاحِبُ في السَّفَرِ، وَالْخَلِيفَةُ في الأهْلِ، اللَّهُمَّ إنِّي أَعُوذُ بكَ مِن وَعْثَاءِ السَّفَرِ، وَكَآبَةِ المَنْظَرِ، وَسُوءِ المُنْقَلَبِ في المَالِ وَالأهْلِ
Allahumma inna nas-aluka fi safarina haza-l-birra wat-taqwa, wa minal-'amali ma tardho. Allahumma hawwin 'alaina safarana haza, watwi 'anna bu'dahu, Allahumma antas-sohibu fis-safar wal-khalifatu fil-ahli. Allahumma inni a-'uzu bika min wa'atha-is-safar, wa kabbati-manzar, wa su-i-lmunqalabi fil-mal wal-ahli.
Ewe Mwenyezi Mungu, tunakuomba katika safari yetu uadilifu, taqwa, na matendo mema unayoridhia. Ewe Mwenyezi Mungu utufanyie wepesi kusafiri, na utupunguzie umbali. Ewe Mwenyezi Mungu, Wewe ni mwenzetu katika safari na mlinzi wa familia yetu (tukiwa hatupo). Ewe Mwenyezi Mungu najikinga Kwako kutokana na taabu za safari, kuona huzuni, na kutokea kwa bahati mbaya katika mali na familia.
(Sahih Muslim)

Comments
Post a Comment