Dua ya kuondosha maradhi
Nabii Ayyub kama alivyobarikiwa mali nyingi, ardhi na watoto. Kisha alipimwa kwa kunyang'anywa yote hayo, kutia ndani afya yake. Viungo vyake vyote vilikuwa na maradhi isipokuwa ulimi na moyo wake ambao alikuwa akimkumbuka Allah S.W.T
Watu walikata uhusiano naye kutokana na ugonjwa wake na alifukuzwa mjini akiwa na mke wake tu ambaye alikuwa akimsaidia. Nabii Ayyub alibaki mvumilivu na mwenye kushukuru licha ya hali yake. Aliomba msaada kwa Allah S.W.T kwa kusoma dua katika Sura Al-Anbiyaa’ (21:83). Dua ifuatayo ni sehemu ya Aya:
رَبِّي أَنِّي مَسَّنِيَ الضُّرُّ وَأَنْتَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ
Robbi annee massaniyad-durru wa-anta arhamur-raahimeen
Bwana wangu. Hakika imenigusa dhiki, na wewe ni Mwingi wa kurehemu kuliko wanaorehemu.

Comments
Post a Comment