Dua ya kufika unako kwenda
Imesimuliwa na Suhaib r.a, Mtume (s.a.w.w.) alisema akiutazama mji anaotaka kuingia:
اللّـهُمَّ رَبَّ السَّـمَوَاتِ السّـبْعِ وَمَا أَظْلَلْنَ، وَرَبَّ الأَرَاضِيـنَ السّـبْعِ وَما أقْلَلْنَ، وَرَبَّ الشَّيَـاطِينِ وَمَا أَضْلَلْنَ، وَرَبَّ الرِّياحِ وَمَا ذَرَيْـنَ، أَسْـأَلُـكَ خَيْـرَ هذهِ الْقَـرْيَةِ وَخَيْـرَ أَهْلِـهَا، وَخَيْـرَ مَا فِيْهَا، وَأَعُـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّها وَشَـرِّ أَهْلِـها، وَشَـرِّ مَا فِيْهَا
“Allahumma rabbas samawatis sab’i wa ma azlalna, wa rabbal ardinas sab’i wa ma aqlalna, wa rabbash-shayatini wa ma adlalna, wa rabbar riyahi wa ma zaraina, as’aluka khaira hadzihil qaryah wa khaira ahliha, wa khaira mafiha. , wa a’udzubika min sharriha wa sharri ahliha, wa sharri ma fiha.”
“Ewe Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa mbingu saba na kila wanacho kihifadhi, Mola Mlezi wa ardhi saba na wanavyo vibeba, Mola Mlezi wa mashetani na wale wanao wapoteza, Mola Mlezi wa pepo na kila wanacho kipeperusha. Ninakuomba kheri ya kijiji hiki, kheri ya wakazi wake na kheri zote zinazopatikana ndani yake na najikinga Kwako kutokana na shari ya kijiji hiki, shari ya wakazi wake na kutokana na shari zote zinazopatikana ndani yake. ”
(Mustadrak Al-Hakim)

Comments
Post a Comment