Posts

BAADHI YA VITHIBITISHO JUU YA UKWELI WA UISLAMU

Image
 BAADHI YA VITHIBITISHO JUU YA UKWELI WA UISLAMU Mwenyezi Mungu amempa nguvu Mtume wake wa mwisho Muhammad S.A.W kwa Miujiza mingi na Ushahidi mwingi ambao unathibithisha kuwa yeye ni mtume wa kweli alietumwa na Mungu. Vile vile Mwenyezi Mungu amekipa nguvu Kitabu chake alichokishusha mwisho, ambacho ni Qur’an tukufu, kwa Miujiza mingi ambayo inathibitisha kuwa Qur’an hii ni Maneno halisi ya Mungu, aliyoyafunua, na kwa hiyo Qur’an haijatungwa na mtu yeyote . Sura hii inajadili baaadhi ya ushahidi huo. (1) Miujiza ya Kisayansi ndani ya Qur’an Tukufu  Qur’an ni maneno halisi ya Mwenyezi Mungu, ambayo aliyashusha kwa Mtume wake Muhammad S.A.W kwa kupitia Malaika Jibril (Gabriel.). Qur’an ambayo ilihifadhiwa na Muhammad S.A.W naye akawasomea Qur’an hiyo wafuasi wake. Nao, kwa zamu, waliihifadhi, kuiandika, na kuipitia pamoja na Mtume Muhammad S.A.W.  Zaidi ya hayo Mtume Muhammad S.A.W aliipitia Qur’an pamoja na Malaika Jibril kila mwaka mara moja na katika mwaka wa mwi...

UTANGULIZI

UTANGULIZI App hii ni muongozo mfupi wa kuufahamu Uislamu. Nayo ina Sura tatu. Sura ya kwanza, ‘‘ Baadhi ya vithibitisho juu ya ukweli wa Uislam ,’’ Sura hiyo inajibu baadhi ya maswali muhimu ambayo watu wanayauliza: Je ni kweli kwamba Qur’an ni maneno halisi ya Mungu, yaliyofunuliwa toka kwake ? Je ni kweli kuwa Muhammad S.A.W ni Mtume alietumwa na Mungu?  Je ni kweli kuwa Uislamu ni Dini ya Mungu ? Katika sura hii, zimetajwa aina sita za ushahidi:   Miujiza ya kisayansi ndani ya Qur’an tukufu: Sehemu hii inazungumzia (kwa picha) baadhi ya hakika (facts) za uvumbuzi wa kisasa wa kisayansi zilizotajwa katika Qur’an tukufu, ambayo ilikwishafunuliwa karne kumi na nne zilizopita. Changamoto Kuu ya Kuunda Sura Moja kama Sura za Qur’an Tukufu: Katika Qur’an, Mungu amewapa changamoto watu wote watunge sura moja iliyo kama sura za Qur’an. Tangu kufunuliwa kwa Qur’an, karne kumi na nne zilizopita, mpaka leo, hakuna mtu aliyeweza kuifikia changamoto hii, ingawa sura ndogo sana ...

DUA YA UPEPO MKALI

DUA YA UPEPO MKALI [ اللهم إني أسألك خيرها ، وأعوذ بك من شرها ] أخرجه أبو داود 4/326وابن ماجه 2/1228 [Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi nakuomba kheri ya upepo huu, na najikinga kwako na shari yake.]    [Imepokewa na Abuu Daud na Ibnu Maajah.] [ اللهم إني أسألك خيرها ، وخير ما فيها ، وخير ما أُرسلت به ، وأعوذ بك من شرها وشر ما فيها وشر ما أرسلت به ] مسلم 2/616 والبخاري 4/76 [Ewe Mwenyezi Mungu nakuomba kheri yake na kheri  ya kilicho ndani yake, na kheri ya uliyoituma ndani yake, na najikinga kwako kutokana na shari yake na shari iliyoko ndani yake na shari iliyotumwa nao.]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

DUA BAADA YA KUMZIKA MAITI

DUA BAADA YA KUMZIKA MAITI  [اللهم اغفر له اللهم ثبته] [Ewe Mwenyezi Mungu  msamehe, Ewe Mwenyezi Mungu  mfanye awe thabiti] Mtume ﷺ alikuwa akimaliza kuzika anasimama mbele ya kaburi na kisha anasema “Muombeeni msamaha kwa Mwenyezi Mungu  ndugu yenu na muombeeni kuthibitishwa kwani hivi sasa anaulizwa.      [Imepokewa na Abuu Daud na Al-Haakim]

DUA YA KUMUINGIZA MAITI NDANI YA KABURI

DUA YA KUMUINGIZA MAITI NDANI YA KABURI  [ بسم الله وعلى سُنة رسول الله ]  أبو داود 3/314بسند صحيح وأحمد [Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na kwa mwenendo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu.]   [Imepokewa na Abuu Daud na Ahmad.]

DUA YA KUMTAAZI ALIYEFILIWA

DUA YA KUMTAAZI ALIYEFILIWA  إن لله ما أخذ وله ما أعطى . وكل شيء عنده بأجل مُسمى …فلتصبر ولتحتسب :  البخاري 2/80 ومسلم 2/63 [Kwa hakika ni Chake Mwenyezi Mungu Alichokichukua, na ni chake Alichokitoa, na kila kitu Kwake kina muda maalum] (…….kisha Mtume ﷺ akimwambia:)  “basi vumilia na taka malipo kwa Allaah” ]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim.] na akisema:  [ أعظم الله أجرك ، وأحسن عزاءك وغفر لميتك ] [Ayafanye mengi Allaah malipo yako, na Akufanye kuzuri kutaaziwa (kuhaniwa) kwako na Amsamehe maiti wako.] …basi ni bora         [Tazama Al-Adhkaar ya Imam Al-Nnawawiy]

DUA YA MAITI YA MTOTO MCHANGA WAKATI WA KUMSWALIA

DUA YA MAITI YA MTOTO MCHANGA WAKATI WA KUMSWALIA  [اللهم أعذه من عذاب القبر] أخرجه مالك في الموطأ 1/288 وابن أبي شيبه في المصنف 3/ 217 والبيهقي 4/9 [Ewe Mwenyezi Mungu  mlinde na adhabu ya kaburi]        [Imepokewa na Imam Maalik na Ibnu Abiy Shayba na Al-Bayhaqiy.] اللهم اجعله فرطاً وذخراً لوالديه ،وشفيعاً مجاباً .اللهم ثقل به موازينها وأعظم به أجورهما ، وألحقهُ بصالح المؤمنين ، واجعلهُ في كفالة إبراهيم ، وقه برحمتك عذاب الجحيم ، وأبدله داراً خيراً من داره ، وأهلاً خيراً من أهله ، اللهم اغفر لاسلافنا ، وأفراطنا ، ومن سبقنا بالإيمان [Ewe Mwenyezi Mungu mjaaliye kuwa nikitangulizi na akiba kwa wazazi wake na nikiombezi chenye  kukubaliwa dua yake.  Ewe Mwenyezi Mungu kwa ajili yake zifanye nzito mizani za wazazi wake na yafanye mengi malipo yao, na mkutanishe na wema wa waumini na mjaaliye awekatika dhamana ya Ibrahim na umuepushe kwa rehema yako na adhabu ya moto, na mbadlishie nyumba bora kuliko nyumba yake, na jamaa bora kulko jamaa zake. ...