BAADHI YA VITHIBITISHO JUU YA UKWELI WA UISLAMU
BAADHI YA VITHIBITISHO JUU YA UKWELI WA UISLAMU Mwenyezi Mungu amempa nguvu Mtume wake wa mwisho Muhammad S.A.W kwa Miujiza mingi na Ushahidi mwingi ambao unathibithisha kuwa yeye ni mtume wa kweli alietumwa na Mungu. Vile vile Mwenyezi Mungu amekipa nguvu Kitabu chake alichokishusha mwisho, ambacho ni Qur’an tukufu, kwa Miujiza mingi ambayo inathibitisha kuwa Qur’an hii ni Maneno halisi ya Mungu, aliyoyafunua, na kwa hiyo Qur’an haijatungwa na mtu yeyote . Sura hii inajadili baaadhi ya ushahidi huo. (1) Miujiza ya Kisayansi ndani ya Qur’an Tukufu Qur’an ni maneno halisi ya Mwenyezi Mungu, ambayo aliyashusha kwa Mtume wake Muhammad S.A.W kwa kupitia Malaika Jibril (Gabriel.). Qur’an ambayo ilihifadhiwa na Muhammad S.A.W naye akawasomea Qur’an hiyo wafuasi wake. Nao, kwa zamu, waliihifadhi, kuiandika, na kuipitia pamoja na Mtume Muhammad S.A.W. Zaidi ya hayo Mtume Muhammad S.A.W aliipitia Qur’an pamoja na Malaika Jibril kila mwaka mara moja na katika mwaka wa mwi...