Hadith Za Mtume (s) Na Ma Imamu (a) - 700-1710





1276. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s., Bihar al-Anwaar, J. 91, Uk.6:

“Ewe Mola wetu sisi kwa hamu kubwa utujaalie haki, Serikali ya Kiislam, (ambayo kwa hakika ipo uadilifu serikali ya Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s., tunamwomba Allah swt atuharakishie kudhihiri kwake). Kwa kupitia hii serikali takatifu, uihamasishe na kuipenda Islam na wafuasi wake ambao na papo hapo kuwadhalilisha unafiki na wanafiki. Na, katika kipindi hicho utuweke sisi miongoni mwa wale watu wanaowaita wengine katika utiifu wako na kuwaongoza katika njia yako utukufu; na, utujaalie heshima na ukuu katika dunia hii na Akhera. Aamin Ya Rabbal ‘Alamiin.

1277. Kuna aina nne ya watu:

1. Wale wanaokula na kuwalisha wengine
2. Wale wanaokula na kuwanyima wengine
3. Wale hawali wenyewe na wala hawawapi wengine wale
4. Wale wanaowanyan’ganya wengine ili wale peke yao

1278. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amebainisha kuwa:

“Mimi nimetumwa kuja kukamilisha maadili.

1279. Imenakiliwa kutoka kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:

“Moyo ulio msafi- halisi ni ule ambamo hakuna chochote kile isipokuwa Allah swt tu”

1280. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambamo twaambiwa:

Imani ya mtu haitokamilika hadi hapo mimi niwe mpenzi wake kuliko hata baba, mama, watoto wake, mali yake na hata kuliko maisha yake.”

1281. Allah swt abatuambia katika Qur’an Tukufu, Surah Qaaf, 50, Ayah 33:

مَنْ خَشِيَ الرَّحْمَٰنَ بِالْغَيْبِ وَجَاءَ بِقَلْبٍ مُنِيبٍ

“Na anayemuogopa ( Allah swt Mwingi wa kurehemu, na hali ya kuwa humuoni na akaja kwa moyo ulioelekea ( kwa Allah swt).” (50:33)

1282. Qur’an Tukufu, Surah Attaghaabun, 64, Ayah 11, inatuambia:

مَا أَصَابَ مِنْ مُصِيبَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّهِ ۗ وَمَنْ يُؤْمِنْ بِاللَّهِ يَهْدِ قَلْبَهُ ۚ وَاللَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ

Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye anayemwamini Allah swt huuongoza moyo wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu”

1283. Amesema Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah Ar-Raa’d, 13, Ayah 28:

الَّذِينَ آمَنُوا وَتَطْمَئِنُّ قُلُوبُهُمْ بِذِكْرِ اللَّهِ ۗ أَلَا بِذِكْرِ اللَّهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ

“Sikiliza: Kwa kumkumbuka Allah swt nyoyo hutulia.”

1284. Na vile vile mwishoni mwa Surah al-Fajr, 89, Ayah 28 twaabiwa

ارْجِعِي إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً مَرْضِيَّةً

Ewe nafsi yenye kutua”!
“Rudi kwa Mola wako, hali ya utaridhika, na umemridhisha.”

1285. Allah wt amesema katika Qur'an,Surah, Hajj , 22 , Ayah 32:

ذَٰلِكَ وَمَنْ يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّهِ فَإِنَّهَا مِنْ تَقْوَى الْقُلُوبِ
Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Allah swt, anayeziheshimu alama za (dini ya ) Allah swt, basi hili ni jambo la katika utawala wa nyoyo.

1286. Qur’an Tukufu, Surah Al Hajj, 22, Ayah 54:

وَلِيَعْلَمَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِنْ رَبِّكَ فَيُؤْمِنُوا بِهِ فَتُخْبِتَ لَهُ قُلُوبُهُمْ ۗ وَإِنَّ اللَّهَ لَهَادِ الَّذِينَ آمَنُوا إِلَىٰ صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ

Na ili walio pewa ilimu wajue kuwa hayo ni Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi na waiamini, na ili zinyenyekee kwake nyoyo zao. Na hakika Allah swt ndiye anaye waongoa wenye kuamini kwenye Njia iliyo nyooka.”

1287. Allah wt amesema katika Qur'an, Surah, Ash-Shams, 91, Ayah 9-10:

قَدْ أَفْلَحَ مَنْ زَكَّاهَا
وَقَدْ خَابَ مَنْ دَسَّاهَا

“Bila shaka amefaulu aliyeyeitakasa (nafsi yake) na bila shaka amejihasiri aliyeiviza (nafsi yake)” Qur’an Tukufu Tukufu inatuelezea:

1288. Qur’an Tukufu, Surah Al Qiyamah, 75, Ayah 1 – 2:

لَا أُقْسِمُ بِيَوْمِ الْقِيَامَةِ

“Naapa kwa siku ya Qiyamah. Tena naapa kwa nafsi inayojilaumu; (kuwa mtafufuliwa na mtalipwa)”.

1289. Twaambiwa katika Qur’an Tukufu Surah, Ash-Shams, 91, Ayah 8:

فَأَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَاهَا

“ Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake”

1290. Qur’an Tukufu, Surah Al Baqara, 2, Ayah 283, inazungumzia kulipa kwa amana:

وَمَنْ يَكْتُمْهَا فَإِنَّهُ آثِمٌ قَلْبُهُ

“Na atakaeficha basi hakika moyo moyo wake ni wenye kuingia dhambini.”

1291. Anaelezea Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah Al Kahf, 18, Ayah 28:

وَلَا تُطِعْ مَنْ أَغْفَلْنَا قَلْبَهُ عَنْ ذِكْرِنَا وَاتَّبَعَ هَوَاهُ وَكَانَ أَمْرُهُ فُرُطًا

“Wala usiwatii wale ambao tumezighafilisha nyoyo zao wakafuata matamanio yao yakawa yamepita mpaka.”

1292. Allah swt katika Quran: :

“Na watakaokuwa na uzani khafifu, basi hao ndio waliozitia hasarani nafsi zao kwa sababu ya kuzifanyia ujeuri Aya zetu.”

1293. Amesema Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah Al Hajj, 22, Ayah 46:

فَإِنَّهَا لَا تَعْمَى الْأَبْصَارُ وَلَٰكِنْ تَعْمَى الْقُلُوبُ الَّتِي فِي الصُّدُورِ

“Kwa hakika macho hayapofuki, lakini nyonyo ambazo zimo vifuani ndizo zinapofuka.

1294. Amesema Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah Al Baqara, 2, Ayah 10:

فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ فَزَادَهُمُ اللَّهُ مَرَضًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ

“Nyoyoni mwao mna maradhi, na Allah swt amewazidishia maradhi.”

1295. Allah swt anatuambia katika Qur’an Tukufu, Surah Al I’mran, 3, Ayah 7:

فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ

“Wale ambao nyoyoni mwao mna upotofu wanafuata zile zinazobabaisha kwa kutaka kuwaharibu watu kutaka na kujua hakika yake vipi........”

1296. Amesema Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 13:

فَبِمَا نَقْضِهِمْ مِيثَاقَهُمْ لَعَنَّاهُمْ وَجَعَلْنَا قُلُوبَهُمْ قَاسِيَةً ۖ يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَنْ مَوَاضِعِهِ ۙ وَنَسُوا حَظًّا مِمَّا ذُكِّرُوا بِهِ ۚ وَلَا تَزَالُ تَطَّلِعُ عَلَىٰ خَائِنَةٍ مِنْهُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِنْهُمْ ۖ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاصْفَحْ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ

“Je! Wakati haujafika bado kwa walio amini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka Allah swt na haki iliyo teremka? Wala wasiwe kama walio pewa Kitabu kabla yao, muda wao ukawa mrefu, kwa Kwa hivyo nyoyo zao zikiwa ngumu, na wengi wao wakawa wapotovu.”

1298. Amesema Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah At Tawba, 9, Ayah 45:

إِنَّمَا يَسْتَأْذِنُكَ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَارْتَابَتْ قُلُوبُهُمْ فَهُمْ فِي رَيْبِهِمْ يَتَرَدَّدُونَ

“Nyoyo zao zina shaka; kwa hivyo wanasitasita kwa ajili ya shaka yao.”

1299. Amesema Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah Al Mut'ffifiin, 83, Ayah 14:

كَلَّا ۖ بَلْ ۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ مَا كَانُوا يَكْسِبُونَ

“Sivyo hivyo! Bali yametia juu ya nyoyo zao (maovu) waliokuwa wakiyachuma.”

1300. Twaambiwa katika hadith Tukufu kuwa:

“Mtu mwenye furaha kuu katika siku ya Qiyama ni yule atakaye yaona maneno aliyokuwa akiyatamka ‘naomba msamaha wa Allah swt’ chini ya kila dhambi alilolitenda. Kwa hivyo inambidi kila Mwislam miongoni wetu apige msasa kila ovu alilolitenda ama sivyo, Allah swt azitowazo onyo zake za upole zitabadilika na kuwa ghadhabu kubwa sana.

1301. Qur’an Tukufu, Surah Yusuf, 12, Ayah 53 kuhusu Mtume Yussuf a.s., inazungumziwa Nafsi :

وَمَا أُبَرِّئُ نَفْسِي ۚ إِنَّ النَّفْسَ لَأَمَّارَةٌ بِالسُّوءِ إِلَّا مَا رَحِمَ رَبِّي ۚ إِنَّ رَبِّي غَفُورٌ رَحِيمٌ

“Nami sijitoi Nafsi yangu; kwa hakika (kila) Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu”

1302. Amesema al-Imam Muhammad al-Baquir a.s. : Al-Kafi, j. 2, uk.330

Zipo aina tatu za dhuluma:

• Kwanza ni ile ambayo Allah swt anatoa msamaha na ya
• pili ni ile ambayo haitolei msamaha na aina ya
• tatu ni ile ambayo yeye haipuuzi.”

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA NABII SULEIMAAN

Full story of theProphet Al-Yasa

Umuhimu Wa Dua Katika Uislamu Na Njia Ya Kuomba