Fadhila Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan Katika Hadiyth Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

Fadhila Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan Katika Hadiyth Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Zifuatazo ni baadhi ya fadhila zilizotajwa katika Hadiyth za kusoma na kuhifadhi Qur-aan. 1. Aliye Bora Kabisa Ni Ambaye Anajifunza Na Kuifundisha Qur-aan: عن عثمانَ بن عفانَ رضي الله عنه أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلّم قالَ: ((خَيرُكُم مَنْ تعَلَّمَ القُرآنَ وعَلَّمَه)) صحيح البخاريِّ Imepokelewa kutoka kwa 'Uthmaan bin 'Affaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mbora wenu ni yule mwenye kujifunza Qur-aan kisha akaifundisha)) [Al-Bukhaariy] 2. Anayeisoma Kwa Mashaka Hupata Thawabu Mara Mbili: عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((الْمَاهِرُ بِالْقُرْآنِ مَعَ السَّفَرَةِ الْكِرَامِ الْبَرَرَةِ، وَالَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ وَيَتَتَعْتَعُ فِيهِ، وَهُوَ عَلَيْهِ شَاقٌّ لَهُ أَجْرَانِ)) البخاري ومسلم Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah...